Tuambizane ukweli, hivi ulishakutana na bonge mwenye roho mbaya au chuki zisizoeleweka?

Tuambizane ukweli, hivi ulishakutana na bonge mwenye roho mbaya au chuki zisizoeleweka?

Tuwe wakweli jamani, mie binafsi sikumbuki kama nilishakutana na bonge mwenye roho mbaya au chuki na visirani visivyoeleweka.

Hata kwa wanawake, mabonge hawanaga baya (Mungu awatunze sana)

Sasa vimbaumbau, yaani iwe kazini au mashuleni, wale waalimu au viranja au maboss wembamba ni hatari. Wana viroho visivyoeleweka.

Huu ni utafiti binafsi.
Mabonge tumefikiwa binafsi naupenda huu ubonge wangu na maintain kilo zangu 85

Binafsi sijawai KUTAMANI kua mwembamba Sana kwa Sasa ni hayo TU.
 
Tuwe wakweli jamani, mie binafsi sikumbuki kama nilishakutana na bonge mwenye roho mbaya au chuki na visirani visivyoeleweka.

Hata kwa wanawake, mabonge hawanaga baya (Mungu awatunze sana)

Sasa vimbaumbau, yaani iwe kazini au mashuleni, wale waalimu au viranja au maboss wembamba ni hatari. Wana viroho visivyoeleweka.

Huu ni utafiti binafsi.
Idi Amin
 
kwanza nikubali kuwa mimi binafsi ni mbonge wakutosha!
sio kwamba tuna roho nzuri hapana.
uvivu wetu wa kumiliki mwili mkubwa ndio unasababisha tuwe hivyo
hatutaki kukumbana na changamoto na hii inawezekana na changamoto tulizonazo (japo si kwa ushuhuda wa daktari lakini kwangu hili ndilo linaeza kuwa sahihi)
yaani kwa kifupi ni uvivu si kuongea na wakati mwingine kushindana katika maamuzi hatuna pumzi ya ubishi kivile.
inawezekana pia flow ya damu katika mfumo wa fahamu unaweza kuchangia mafuta mingimingi.
hivyo inawezekana hatufanyi kwa hiyari yetu.
 
Hicho kisirani hata awe nacho safari ya kutoka moyoni kipenye Yale manyama mpaka kikufikie kiemshachoka na kukata tamaa
 
Dah we jamaa umewaza nini!? Kwelii sijawahi ona bonge mwenyewe roho mbaya

Zaid ya mabonge wengi ni wachekeshaji sana yan wacheshi
 
Kwahiyo mwanamke mwembamba akija kunenepa tabia nayo itabadilika? Au kibonge akikonda naye atabadilika tabia? Mie naona tabia/roho ya mtu na muonekane wake hata haviendani.
Mrs Van bana. We unafikiri Nyamaza Akisoni wa jengo kubwa kule Dodoma kuna siku atakuja kunenepa? Kuna vimbaumbau dizaini fulani hivi hata kawe kanaishi kwenye pipa la extra virgin olive oil gredi wani na kawe kanafakamia kitimoto daile kamwe hakanenepi ng'o. Halafu msosi kanafukia hatari mpaka unaweza kushangaa msosi huwa unapotelea wapi. Na chooni mzigo kanashusha wa uhakika. Ndo hivi sasa tunavyovisema hapa. Ujichanganye ubebe ka hivi haki ya nani andika wosia mapema tu maana miaka 50 hutafikisha. Halafu kawe Kanyaki sasa maweeee!

Hata binti akiwa kimbaumbau wanaoweza kunenepa huko mbele ya safari wanajulikana hata kwa kumwangalia tu. Mifupa minene. Guu proposhono na mwili, kitako fulani hivi ameizingi, collarbone na hata mifupa ya usoni itakupa clue. Mabinti wa hivi huwa ni wapole na wavumilivu sana labda tu ukimtibua. Ila tuvimbaumbau twenyewe pyua dizaini ya akina Nyamaza Akisoni aisee ni hatari sana - wivu wa kijinga, makelele, hasira za mkizi, kujishebedua, kutokujiamini, hekaheka, mizozo, kusutana, uchoyo, kwenda kwa waganga ali mradi vurugu tupu! 😂
 
Back
Top Bottom