Tuamke, tuwaamshe mizimu wetu, katika nyakati za hatari watusaidie

Kwani MUNGU hayupo? Njia alizotumia kuumba Ulimwengu na vyote vilivyomo mbona zimeandikwa kwenye Vitabu? Mbona kuna watu wamewahi kuisikia sauti ya MUNGU akiongea? Au kwa vile wewe hujaisikia sauti yake ndiyo maana unasema hayupo?

Hao wanasayansi wanasema eti kiumbe hai wa kwanza alitokana na "cell" ambayo ilitokea baada ya kitu wanaita Big-Bang kutokea. Sasa hebu nikuulize, hivi hiyo cell moja inawezaje kujibadilisha ikawa mwanadamu na mwili wake ukiwa na viungo tofauti tofauti, cell hiyo hiyo ijibadilishe iwe samaki, ng'ombe, simba, mjusi, kipepeo, nyani, nyoka, nzi, mbu, paka, bakteria, virus, miti, mimea n.k.???

Hivi kweli haikuingii akilini kwamba hivi viumbe vyote kila kimoja kwa jinsi yake viliumbwa kama vilivyo kwa ustadi mkubwa sana na yule mwenye nguvu na uwezo wa ajabu ambaye ni BWANA MUNGU?

Wanasayansi hao hao wanatudanganya eti mwanadamu ametokea kwenye evolution, hebu nikuulize swali, tangu mwanadamu apate maarifa ni takriban miaka 2000 sasa imepita, je ni nani amebadilika kwa kipindi hicho cha miaka 2000 iliyopita? Mwanadamu anaishi kwa miaka 70, akizidi sana labda miaka 120, sasa hebu tuambie ni mzee yupi wa miaka 120 amebadilika kwa kuota hata mapembe tu sababu evolution ni mabadiliko yanayotokea kidogo kidogo, je nani amebadilika?

Kama kweli hakuna MUNGU, na wanadamu pamoja na viumbe wengine tumetokea baada ya evolution basi mpaka leo hii tungekuwa tunashuhudia hiyo evolution ikifanya kazi yake, wanadamu tungeanza kubadilika labda hata tungekuwa na mabawa turuke kama ndege baada ya kutembea ardhini kwa miaka yote hiyo.

Tusidanganyane mkuu, MUNGU yupo na kila kiumbe alikiumba au kukitengeneza kwa jinsi yake na namna yake tofauti, kila kiumbe alikitengeneza kwa ufundi tofauti.

Cc Kiranga
 
Huyo kiranga mkuu si ndo kabisa,haamini lolote
 
hatupingi kuwepo kwa Mungu, ila tunawasiwasi na ngano za wayahudi kumuhusu
 
hahaha ..."" mkuu nishushe tafafhali "" umeshaanza kuhubiri ""... ngoja tuendelee kujadili mada iliyopo mezani "" tusimharibie "" Fatima Uzi wake ""...!
 
Hujathibitisha Mungu yupo.

Thibitisha Mungu yupo.

Vitabu unavyosema vimeandika habari za huyo Mungu ni vipi?

Vitaje tuvichambue.
 
hahaha ..."" mkuu nishushe tafafhali "" umeshaanza kuhubiri ""... ngoja tuendelee kujadili mada iliyopo mezani "" tusimharibie "" Fatima Uzi wake ""...!
Tatizo ukiwaambia wathibitishe Mungu yupo, wanahubiri .

Tena kijumlajumla, bora haya ingekuwa rejareja.
 
Kiranga.. na Dini wapi na wapi hahaha
 
Lengo letu hasa la kuishi ni nini??according na hiyo imani??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…