lazima tuseme yaliyotokea, Latina tutoke misikitinina makanisani,turudie ibada yet u ya kweli
Ngoja nikupe simulizi refu la mfano labda utaelewa kupitia hilo kuona kile mnacho maanisha......
Ni sawa na watu ambao wapo safarini lakini kwa bahati Mbaya
Basi walilotumia kusafiria likapata hitilafu katikati ya Mbuga na ni Usiku
Hofu ikatanda kati yao_na wenye hekima kati yao wakatoa ushauri kwa watu wote kutojaribu kutoka nje maana ni usiku
Kwa kuhofia ugumu wa kutoa msaada kwa mtu anayeweza kudhurika na hayawani mwitu hata na watu wabaya kama majangiri.
Halafu wakiwa katikati ya usiku wanaona kama kuna ishara ya taa za gari zikimulika karibu yao.
Wanajawa na shauku.........!!??
Kukawa na mpasuko kati yao wengine wakidhani yawezekana ikawa ni gari inayoweza wapatia msaada..!
Na wengine wakihofu kuwa yawezekana ikawa ni Gari ya watu wabaya..! wenye nia mbaya nao
Lakini wakiwa katikati ya maulizo hayo.! Wanaona kuna baadhi ya watu wakiwakabili wakitokea upande ule ambao walihisi uwepo wa Gari.
Baadhi wakapatwa na hofu kulingana na shuku yao kuhusu watu wabaya na kuanza kijihami
Na wengine wakawa wakiwatuliza wenzao kulingana na muelekeo wao wa kuhisi kuwa yawezekana ni watu wa msaada..
wakasemezana;
"Ngoja na watukaribie na tutajua kama kweli ni watu wenye nia njema nasi ama La"
Lakini wakiwa katikati ya hali hiyo baadhi wakahoji kwamba
"Tuliona kama ishara ya gari..! Lakini mbona hawa wanakuja kwa miguu.!? Kweli wanaweza wakawa ni watu wa msaada".!?
Wakaendelea wakisema "hakikisheni milango ya gari imefungwa barabara na madirisha ya gari pia, na Taa na zizimwe wasije wakatuhesabu na wakatukabili kirahisi..Na kama wakihitaji kuwasiliana nasi tutatumia Upenyo wa dirishani na watakao semezana nao ni wanaume Tu".
Wale watu_kweli wakakaribia lile Gari na kutoa salamu kwa uchangamfu Tu 'za saa izi ndugu wajameni'....watu kimya.
"Hivi ni kweli hamuitaji Msaada.!? Mbona twawasalimu lakini Hamjibu Mna tatizo Gani.!?
Wakaendelea
"Kama manahitaji msaada basi na shukeni Garini Mwenu na Tuongozane Twende Tukapande gari yetu ya Uhakika na imara na Tunawahakikishia mtafika kwa wakati.. kuliko kukaa hapa usiku kucha bila msaada na hatari hizi".
Hapo Mmoja wa kwenye gari akashindwa kujizuia_akahoji. "ikiwa kweli mnataka kutupatia msaada kwanini msingeileta gari yenu karibu nasi ili tuwe na uhakika wa mnayoyasema"..!?
Ngoja niishie hapa usije ukachoka kuisoma na kuimalizia..ila ukitaka niendelee nitaendelea