Dunia haiko kama unavyoiona, Kuna agenda ya siri sana, na wahanga wakubwa watu, weusi, lazima uamke ili uione picha kubwa...ukifanya hivyo, utajikuta uko vitani mtu mweusi, karibu tuko hapa maaskari wenzio kukufungua macho yako....uamke kutoka msukuleni. Hapa tunakufunulia mambo yaonekanayo ndivyo hivyo, kumbe sivyo ndivyo
lengo kuu la uzi huu, ni kukufikisha mahali ndugu msomaji ukajihoji binafsi, na yale yanayoendelea duniani, kukuchochea we kutokubali mambo kwenye sahani
Kwenye dunia iliyojawa ushahidi wa uongo, kutokuwepo ushahidi ndio Ingekuwa ushahidi, hii hasa pale watawala, wenye mamlaka juu ya vyanzo vya taarifa, wanapokuwa ndio watuhumiwa wenyewe. Ishu ya Michael Jackson, ni mfano mdogo tu, mjadala ni mpana kuliko hapo.
mada yet u inahoja Za msingi zifuatazo:
1. Mweusi binadamu wa Kwanzaa
2. Mweusi mwanzilishi wa ustaarabu duniani ikiwa ni pamoja na dini
3. mweupe kwa sababu ya wivu na chuki akaleta Sera ya ubaguzi
4. Kupitia ubaguzi amejaribu na kufanikiwa mno kufuta ya misingi mikuu iliyowekwa na mtu mweusi, kisiasa, kitaaluma, kitamaduni
5. Ustaarabu wa mweupe leo ni mwigo wa ustaarabu mkongwe zaidi wa mweusi kwa kila namna
* Kama una ushahidi kupinga haya tuyasemayo, tuletee hapa
Tuamke, tuwaamshe mizimu wetu, katika nyakati za hatari watusaidie
Asanteni
Mheshimiwa Fatima Binti Hemedi, yaani kichwa cha habari na mada yako mbona naona kama umetumwa kukanganya jamii? Hayo maswali siyo ya HISTORIA? Mimi nikakimbilia kuchungulia neone UKOMBOZI unatujia nakutana mada za mwalimu wa historia, wakati kuna MATATIZO lukuki yanatuzidi kimo hatuyaweki wazi tujadili! nakupa mada za mfano ambazo nadhani zingeendana na kichwa chako cha habari;
1. Tatizo la kukua kwa kasi ya ajabu ya KANSA hasa ya MLANGO WA KIZAZI kwa akina mama linatishia ustawi wa jamii na kizazi kijacho, je nini hasa ni CHANZO na nini hasa kinaweza kuwa suruhisho? [ zingatia kelele za Glyphosate ya kwenye PAMBA kutokana na matumizi ya dawa ya ROUNDUP wakati wa kilimo cha pamba katika maeneo mengi duniani sasa]
2. Kwanini PESA YETU inashuka thamani BILA MAELEZO wakati nchi ina UTAJIRI MKUBWA [MINERAL AND NATURAL [ASSETS] wa madini na rasilimali nyingine ambazo zinapaswa KUILINDA THAMANI yake?
3. Takriban VIJANA CHINI YA MIAKA 40 wanawakilisha asilimia sabini [70%] ya wanachi katika bara la Afrika, je hii KERO YA KUTOTENGENEZA AJIRA kwa ajili ya kuitumia na kuilinda hii nguvu kazi siyo tishio kwa ULINZI NA USALAMA wa nchi zetu? na NINI KIFANYIKE ili tuliokoe hili kundi kwa haraka ipasavyo?
4. Nchi yetu ina MIUNDO MBINU mingi, kama vile MWENDO KASI, RELI, BARABARA, NDEGE, je ni vipi hizi rasilimali zinaweza kutuokoa KUJIKWAMUA NA MAKUCHA haya ya unyonyaji kwa kutumia UBUNIFU WA WATU WETU KUFUNGAMANISHA [integrated strategic planning and execution] ili kujiletea maendeleo na kukwepa UTEGEMEZI ULIYOVUKA MIPAKA?
5. Mafuta na Gesi ni BIDHAA ILIYOVUTIA WATEJA KWA KASI SANA katika miaka mitano iliyopita, je sisi ambao tayari tunavyanzo kiasi vya hii rasilimali TUFANYE NINI ili tuweze KUVUNJA HUU UKILITIMBA WA MAGHARIBI, tunaoushabikia kama MBWA NA CHATU, kwa kuingia katika UBIA WA KIMKAKATI [ strategic partnership] na MTEJA MWENYE NGUVU za kutosha atuvushe toka hapa tuliponasa KIMKAKATI, TEKINOLOJIA NA KIFEDHA?
Haya sasa twende kazi!
View attachment 805894 View attachment 805895 View attachment 805897