Binadamu anapozaliwa tu, anajikuta yupo chini ya utawala wa Mama.
Mama anaamua amnyonyeshe au la, na kama hivyo ni muda gani.
Mama ndiye anayeamua akunyonyeshe hadi ushibe au kabla.
Mama ndiye Malkia na kamwe binadamu huyo mdogo hawezi kujitoa chini ya utawala wa huyo Malkia.
Yeye ataamua binadamu huyu ni muda gani, alale,aamke, ale, aoge, avae nk.
Hapa inapita miaka kadhaa kabla ya kujikuta chini ya utawala wa Malkia na Mfalme Baba.
Hawa watawala watammiliki huyu binadamu kwa kipindi fulani pia.
Katika kipindi hicho binadamu inampasa kufuata sheria zote anazopangiwa na hao ma mjamaa, la sivyo kuna adhabu zitamfika, kama kuchapwa viboko, makofi, kufinywa, kunyimwa chakula, kutishwa na hawezi kujinasua nao.
Binadamu huyu anazidi kukua, Baba na mama wananza kuona kuwa kijana anapata uwezo unaolingana na wao, wanaanza kuogopa kumchapa kama hatafuata wanavyotaka, wanaamua jambo lingine nalo ni kumkabidhi kwa Jamii.
Kijana anakabidhiwa kwa Jamii au taasisi zake.
Anaanza kupelekwa Shule, ili kafunzwe ustaraabu zaidi, hapo akiwakosea wazazi hawamchapi tena, wanamwogopa, watachukua hatua ya kumuonya na ikishindikana wanampeleka Polisi.
Juhudi zote hizo wanataka kijana afuate sheria fulani fulani ambazo zinazunguka ndani ya jamii husika.
Kijana kwakuwa sasa anapaswa kuwaacha wazazi na kwenda Shule, au taasisi nyingine ya kijamii, ambako atakutana na watu wenye mafundisho mengine, wazazi wanaamua kumlinda kwa kumkabidhi kwa taasisi za Ki imani.
Ili kuirutubisha akili yake isimtume kijana kufanya matendo ambayo hayakubaliki na jamii hiyo.
Kijana anapokuwa mtu mzima haraka haraka anakabidhiwa wake wa jinsia nyingine kwa Amri ya Ndoa ili asilale peke yake, asije akalala Bar.
Katika ndoa nako kuna sheria kibao za kuzifuata, kijana analazimika kusaini mkataba wa ndoa, na anaambiwa kabisa hakuna kuvunja ndoa kirahisirahisi. Kwa kujiamlia tu asubuhi unapoamka.
Hapo mke au mume anakuwa sio mpenzi tu, bali Polisi pia.
Polisi wa kumlinda kijana ili asikengeuke
Kijana lazima umsirikishe huyu Mpenzi Polisi katika kila jambo unalo amua kufanya.
Hata ukitaka kuondoka nyumbani lazima umuage huyu Mlinzi wako.
Ni lazima umtii huyu Mpenzi kumbe ni Mlinzi.
Na kwakuwa mko peke yenu lazima na nyinyi wote mlindwe na Mlinzi Mwingine msije mkakengeuka wote wawili ikawa badala ya kulala Nyumbani mjalala Kasino.
Hapa sasa mnakabidhiwa kwa walinzi wawili, Jirani na Serikali.
Mkigombana tu mlinzi wa kwanza anawajia ( jirani) atajaribu kuwa suluhisha mkiwa wabishi anaripoti kwa mlinzi wa tatu, Polisi, Serikali.
Hapo ukiendelea kuwa mbishi Polisi anajua pa kukupeleka, na unaweza ukapotea moja kwa moja kama hutajirekebisha.
Sasa basi
Tunaona kila hatua ya binadamu kuna ulinzi unamfuatilia, upo nyuma yake ambao tunauona kwa macho.
Swali linalobaki huyu mlinzi atalindwa na nani ?
Ili kumfanya asimwonee binadamu anapo taka, yaani mlinzi, mke au mume, mlinzi jirani, mlinzi polisi, mlinzi Serikali, nk.
Ili mlinzi mmoja asimwonee mwenzake hapa ndipo anapojitokeza mlinzi mkuu.
Jamii inampa cheo, cha Uungu, huyo ndiye Mungu, huyo anajulikana kuwa ni Alfa na Omega. Muweza wa yote, Almighty.
Katika kila jamii ukiitembelea ina Mungu wake.
Nenda Uchina, nenda Brazil nenda kokote duniani utamkuta huyo Mungu ambaye jamii inamwogopa na kumheshimu sana sana, na kulazimika kumtii kwa kila anachosema.
Ukikosea kimtii jamii inaweza kukuadhibu, sehemu nyingine unakatwa kichwa kabisa kwa kumkose, au Kumkufuru, huyo Mungu.
Tanaona hadi leo, Serikari ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ikitaka kuanza kutunga sheria zake Bungeni, lazima kwenye ufunguzi wa kikao kuna Kusali uli kupata baraka zake, huyo Mungu.
Ref. Sala ya Bunge.
Iko pia sala ya Taifa, ambayo inajulikana kama Wimbo wa Taifa.
Humo Mungu hutajwa sana, ili aibariki Nchi, Viongozi na Watu wake.
Yaani vyoote hivyo ni vyake, mali yake, yeye ndiye aliyevitengeneza, na hana mshirika.
Leo tunaona Viongozi wa Serikali wakiwa wanawaonea Raia wanaowaongoza, wanakaripiwa vikali na Wafanyakazi wa huyo Mungu, wanaojulikana kama Watumishi wa Mungu.
Wana vyeo kama vile, Shehe, Imamu, Padri, Askofu, Mchungaji nk.
Wanaionya Serikali kwa Nyaraka na Matamko, na kuitisha kuwa wataishitaki kwa Mungu, nayo Serukali inaogopa na kujirekebisha kiasi fulani fulani.
(Hapa nilikuwa nadadavua uhalisia wa kimaisha wa Binadamu)
Binadamu anazungukwa na walinzi kila kona. Kila dakika kila sekunde, walinzi wanaoonekana na wasioonekana.
Uhuru wa wa kifikra utapatikana wapi kwa binadamu ?
maana ukiwa huru kifikra unakuwa huru kimatendo pia.
Toka anazaliwa hadi anakufa Binadamu hayuko huru kuamua au kutenda anachotaka mwenyewe binafsi.
Kwa mfano.
Hapa Tanzania mtu akiamua kutumia madawa ya kulevya anakamatwa, akitaka kupanda Bangi shambani mwake ili aitumie anakatazwa na hata kutishiwa kufungwa na Mlinzi Serikali.
Hapo uhuru uko wapi ?
Bangi navuta mimi wewe
Inakuhusu nini ?
Mbona unaiingilia uhuru wangu mimi binafsi ukichukulia sivuti hadharani bangi yangu ?
Mwenyewe napenda kuvuta huku nikiimba
" Bangi Nibangue nilime hadi kuleee "
Bangi usiyovuta yakuwashiani ?
Kuna uhuru hapo ?
Uhuru gani wa kulazimishwa kutii sheria alizotunga mtu
mwingine ? Au Mungu ?
Maana ya Uhuru ni Kuwa Huru Kifikra na Kimatendo pia.
(To Be Total Free)
Je unaweza kujikomboa kwenye mikono ya hawa walinzi wote nilio wataja ukianzia na Mama mzazi ?
Anafuata, Mke au Mume, Jirani, Serikali, na Mungu ?
Au unataka usimtii mmojawapo kati ya hao walinzi ?
Ndipo ujulikane kuwa uko huru ?
Hit.
Binadamu hawezi kuwa huru,
kwani analazimika kutii sheria alizowekewa na waliomtangulia, la sivyo atakumbana na adhabu kali zinazoweza hata kumtoa uhai wake, kama ataendele kuwa mkaidi.
Hello to Free Men.