Kuweka mizania sawa kwa minajili ya ulinganifu tuiangalie Tanzania dhidi ya wengine EA.
Nchi zote hapa kuna lugha rasmi za kibeberu yaani kiingereza au kifaransa. Kwingine kasoro Tanzania si ajabu kukuta watu wa kawaida wakiwamo boda boda, vinyozi, maseremala nk wakizimudu vilivyo lugha hizo za kujifunzia ukubwani.
Hali ni tofauti mno hapa kwetu. Tumeyaona kwa madaktari na hata maprofesa.
Yote hayo ni dalili tu ya mvua.
Kwa wenzetu mifumo ya elimu ni rafiki yenye kuwavutia wote katika jamii kujiendeleza. Kwa wenzetu si ajabu kukuta wasomi wabobezi wakifanya shughuli zinazooonekana kwetu kuwa ni za kawaida. Humo wakiwamo boda boda, madereva, wakulima, vinyozi nk.
Kwa wenzetu si ajabu kwa kada yoyote mfano boda boda, mkulima, dereva nk kujiendeleza kielimu kutokea alipo kufikia ngazi.yoyote.
Matokeo yake wenzetu ni jamii ya walioelimika juu hadi chini.
Tujilinganishe vipi nao? Mengine kwetu ni yatokanayo.
Ubora wetu kwenye u Simba na Yanga, kwenye hadithi za ngono na vikorombwezo vyake nk ni yatokanayo tu.
Ubora wetu kwenye kushabikia wanapokamuliwa wengine wasiotuhusu ni mwendelezo huo huo wa yatokanayo.
Kwa mfumo wetu huu wa elimu, kwa hakika bado tupo tupo sana.