Tuanze moja: Tuachie wafungwa wote walio magerezani na walio rumande bila masharti

Tuanze moja: Tuachie wafungwa wote walio magerezani na walio rumande bila masharti

Nyani Ngabu

Platinum Member
Joined
May 15, 2006
Posts
94,296
Reaction score
122,540
Nina wazo.

Wazo linaloendana na uwezo wa kiakili wa mbeba maboksi.

Ni hivi: tuanze moja. Tuachie wafungwa wote walio magerezani na walio rumande bila masharti yoyote yale.

Au tufanye hivi: tumuulize kila mfungwa aliye gerezani na aliye rumande kama yupo humo kwa kuonewa na kubambikiwa kesi.

Kila atayesema ‘ndiyo’, tunamwachia huru bila masharti yoyote yale.

Tukifanya hivyo utakuwa ni mwanzo mzuri sana.

Magereza yetu hayapendezi yakiwa yamejaa watu waliobambikiwa makesi.

Naamini 99% ya wafungwa wote walibambikiwa kesi zao.

Achia huru wafungwa wote haraka iwezekanavyo!

NB: Au tufanye hivi. Wafungwa wote waliofungwa kati ya Oktoba 2015 na Machi 2021, wote waachiwe huru haraka iwezekanavyo bila masharti yoyote yale.
 
Bila Katiba Mpya haya yataendelea tu kwa sababu Katiba iliyopo ndiyo inayompa nguvu DPP, DCI, polisi na Hakimu kufanya wanavyotaka.

Tukitaka tuanze upya Katiba Mpya ndio mwarobaini wa yote maana kila kiongozi atawajibishwa kwa matendo yake, kuanzia Rais hadi mtendaji wa Kata including IGP, DPP, Hakimu nk.
 
Ingependeza zaidi kama ungesema wale ambao wako ndani na uchunguzi wa kesi dhidi yao bado haujakamilika zaidi ya miezi sita ndio waachiwe.

Kama kuna mashtaka dhidi yao mahakamani yamefutwa basi waachiwe na mahakama, kama bado yamebaki mashtaka mengine dhidi yao yasikilizwe na mahakama tujue mwisho wake, sio kuachiwa ghafla tu.

Lakini ukisema waulizwe kila atakayejibu amebambikiwa kesi aachiwe hapo utakuwa unatania, sheria zipo lazima zifuatwe.
 
Ingependeza zaidi kama ungesema wale ambao wako ndani na uchunguzi wa kesi dhidi yao bado haujakamilika zaidi ya miezi sita ndio waachiwe, lakini ukisema tu waulizwe kila atakayejibu amebambikiwa kesi aachiwe hapo utakuwa utani.
Well said
 
Kwani happy siunamtetea yule kijana machachari,alive ndani ya nyavu,hapo Mimi sikubaliani na wewe.
 
Ingependeza zaidi kama ungesema wale ambao wako ndani na uchunguzi wa kesi dhidi yao bado haujakamilika zaidi ya miezi mitatu ndio waachiwe.

Kama kuna mashtaka dhidi yao mahakamani basi waachiwe na mahakama baada ya kesi kusikilizwa, sio DPP baada ya kutoa pesa.

Lakini ukisema tu waulizwe kila atakayejibu amebambikiwa kesi aachiwe hapo utakuwa utani.
Wafungwa wote waachiwe bana!

Waachiwe ASAP!

Na waachiwe bila masharti.

Mama ni mtu mwema sana.
 
Ww endelea kubeba box mzee Tanzania tuachie sie tunaoishi humo...ww unaebeba box nje ulikuwa unapata taarifa za mazuri tu mdio maana huwezi jua kwanin Magufuli aliharibu nchi.
 
Na tutakuwa tunaanza upya kila baada ya muda gani? Au Baada ya kuanza upya sasa hatutaanza upya tena?

Issue ni kuhakikisha makosa hayafanyiki mwanzo (labda kwa bahati mbaya) Na ikionekana kwamba makosa yalifanyika na kama ni kwa makusudi wale walioyafanya wawajibishwe bila huruma..., hata kama wameshakwenda mbele ya haki (the record should indicate so...)
 
Back
Top Bottom