Tuanze moja: Tuachie wafungwa wote walio magerezani na walio rumande bila masharti

Tuanze moja: Tuachie wafungwa wote walio magerezani na walio rumande bila masharti

Wafungwa wote waachiwe bana!

Waachiwe ASAP!

Na waachiwe bila masharti.

Mama ni mtu mwema sana.
Hiki kinachofanyika sasa kisije kuleta picha Tanzania now all is well, hawa wakubwa wataanza kutupiga vizuri tusipokuwa makini, vyema waachiwe kama hawana hatia.

Lakini uwepo msisitizo wa kutii na kufuata sheria, vinginevyo tutarudi kule kwa zamani jela zitabakia kwa wezi wa kuku na simu tu, wakubwa watalindana kesi zao zitaishia juu kwa juu, hapa umakini unahitajika.
 
Ingependeza zaidi kama ungesema wale ambao wako ndani na uchunguzi wa kesi dhidi yao bado haujakamilika zaidi ya miezi mitatu ndio waachiwe.

Kama kuna mashtaka dhidi yao mahakamani yamefutwa basi waachiwe na mahakama, kama bado yamebaki mashtaka mengine dhidi yao yasikilizwe na mahakama tujue mwisho wake, sio kuachiwa ghafla tu.

Lakini ukisema waulizwe kila atakayejibu amebambikiwa kesi aachiwe hapo utakuwa unatania, sheria zipo lazima zifuatwe.
Hujamuelewa, jamaa anamaanisha hapendezwi na hii hali ya kuwatoa hawa mahabusu
 
Hujamuelewa, jamaa anamaanisha hapendezwi na hii hali ya kuwatoa hawa mahabusu
Nimemuelewa, mahabusu lazima watolewe kama mahakama itajirishisha hakuna ushahidi wa kutosha wa mashtaka dhidi yao, lakini sio kuwaachia tu hiyo itakuwa vurugu.
 
Uchunguzi wa kutoonekana kwa Ben Saanane na Azori Gwanda unaanza lini?

Bila kusahau kuhusu kushambuliwa kwa Tundu Lissu mchana kweupe tena eneo lenye ulinzi hatukuwahi kuzoea hayo mambo Tanzania
 
Kama ulikua rumande kwa kupiga dili kubwa kubwa unaachiwa. Kama ulipiga dili ndogo ndogo unaendelea kula msoto.

Moral of the story: Mwenye nacho huongezewa, asiyenacho atanyang'anywa hata kile kidogo.
 
Mfumo wa sheria hautumii vipimo vya hisia bali haki kutokana na ushahidi.

Kuwaachia huru watuhumiwa wa makosa ni kulitusi jeshi la polisi kuwa halifanyi kazi kiuadilifu. Lakini pia kuna taasisi zisizo za kiserikali ambazo hudeal na haki za raia sijaona kupewa nafasi kuwatetea wale ambao hii misamaha haiwagusi sababu ya hali zao kifedha.

So hili swala lifanywe kwa umakini. Jela si pahala kwa watu wema bali wanaovunja sheria kwa kusudi.

Sent from my JKM-LX1 using JamiiForums mobile app
 
Kuna watu wanafikiri kwamba mama anakurupuka kuachia watu

Mafaili yote yapo ikulu na mwenyewe anayaona

Ukweli unajulikana kabisa watu wengi sana wamebambikiwa kesi

Mbona wakina Babu Seya waliachiwa na hamkupiga kelele?

Hatuwezi kujaza magereza kwa kesi fake halafu hatuwezi kuachia wauaji wao waendelee kusota tu.
 
Kuna watu wanafikiri kwamba mama anakurupuka kuachia watu

Mafaili yote yapo ikulu na mwenyewe anayaona

Ukweli unajulikana kabisa watu wengi sana wamebambikiwa kesi

Mbona wakina Babu Seya waliachiwa na hamkupiga kelele?

Hatuwezi kujaza mahlgereza kwa kesi fake halafu hatuwezi kuachia wauaji wao waendelee kusota tu.
Hawa Sukuma Genge wanajisikia fedheha kwa kuachiwa watu waliokuwa na kesi za kubambikiwa
 
Kuna mfungwa aliachiwa kwa msamaha wa Rais Samia sikukuu ya muungano, hajakaa kitaa mwezi kafanya zali tena!

Tuweke process tu ya kuhakiki kesi zilivyoendeshwa na haki itolewe.

Lakini huu msamaha unaotaka utaleta majanga.
Hii si mara ya kwanza na msitake kuifanya hoja na kutudanganya wafungwa waliotoka jela kwa msamaha wa Rais wameanza kirudia makosa wakati wa Samia. Acheni upotoshaji nyie Push Gang. Semeni mengine lakini ukweli KWAMBA utawala wa Magufuli ulikuwa utawala dhalimu hata muufunike kwa lami utaibuka tu.
 
Back
Top Bottom