King Kong III
JF-Expert Member
- Oct 15, 2010
- 56,205
- 79,515
Waachiwe wale ambao ushahidi hakuna miaka nenda miaka rudi.....Mtu anakaa miaka zaidi ya mi5 DPP anasema hana ushahidi sasa huo si uonevu? Jinai haifi kama hana ushahidi muachie huru ukishapata ushahidi utamkamata tena.Nina wazo.
Wazo linaloendana na uwezo wa kiakili wa mbeba maboksi.
Ni hivi: tuanze moja. Tuachie wafungwa wote walio magerezani na walio rumande bila masharti yoyote yale.
Au tufanye hivi: tumuulize kila mfungwa aliye gerezani na aliye rumande kama yupo humo kwa kuonewa na kubambikiwa kesi.
Kila atayesema ‘ndiyo’, tunamwachia huru bila masharti yoyote yale.
Tukifanya hivyo utakuwa ni mwanzo mzuri sana.
Magereza yetu hayapendezi yakiwa yamejaa watu waliobambikiwa makesi.
Naamini 99% ya wafungwa wote walibambikiwa kesi zao.
Achia huru wafungwa wote haraka iwezekanavyo!
NB: Au tufanye hivi. Wafungwa wote waliofungwa kati ya Oktoba 2015 na Machi 2021, wote waachiwe huru haraka iwezekanavyo bila masharti yoyote yale.
Wale waliohukumiwa waendelea kukaa lupango otherwise kama wana room ya kukata rufaa kama vigezo na msharti wametimiza kesi zao zitasikilizwa upya na kama wakiwa hawana hatia walisingiziwa wataweka ushahidi ubaoni.