Benjamin9911
Member
- Mar 8, 2018
- 6
- 10
''Fikira au Fikra (kutoka neno la Kiarabu) ni ujumbe uliotumwa kutoka akilini kwa ajili ya viumbe hai ili kujua kutenda jambo bila kukosea.
Fikra husaidia na maamuzi: wanyama(mfano mifugo n.k) mara nyingi huishi bila ya kufikiri, yaani kujua nini kesho atafanya, lakini wanadamu hutumia fikra na kufikiria na kuvumbua vitu ambavyo vinahitajika. Bila fikra za mawazo, dunia isingeendelea sana''. Hii ni tafsiri rahisi ya neno Fikra kutoka
Sasa sisi Watanzania kama tunataka kutoka hapa tulipo ili tuzifikie nchi tunazoziita "Developed Countries" yaani Nchi zilizoendelea yatupasa kubadili Fikra na mitazamo yetu ya kuwa sisi ni tegemezi hivyo kuzinyima fursa fikra zetu kuamua kwa usahihi na mwisho kujitoa kwenye utumwa huu wa fikra, na kuiendea Dunia inavyokimbia sasa kwenye MAPINDUZI YA NNE YA KITEKNOLOJIA, ambayo kwa ukweli kabisa sisi Tanzania na Afrika ndio wenye Malighafi zinazosaidia kwa asilimia kubwa maendeleo haya. Malighafi nyingi za kutengenezea vifaa vya umeme ikiwemo Talakilishi (Computer), simu na vifaa vingine vya kielectroniki. Nchi za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Madagascar, Burundi, Tanzania zimegundulika kwa mda mrefu kuwa na madini adhimu ambayo yanatumika kwenye Nyanja ya TEKNOLOJIA, madini hayo Ikiwemo Graphite, Silicon, Nguvu Adimu za Dunia (Rare Earth Elements - REE).
Nitatoloea Mfano wa Graphite ambayo kwa Tanzania tunayo na inapatikana maeneo ya kusini mwa Tanzania haswa Mkoa wa Lindi, kule Ruangwa. Kuna mgodi mkubwa unaitwa LINDI JUMBO LTD, ambao wenyewe wanajihusisha na uchimbaji wa madini haya ya Graphite, ambapo uwekezaji huu umefanywa na Mwekezaji wa nje, bila shaka watakaokuwa kwenye ngazi za uongozi kwenye Mgodi huu ni watu kutoka nje. Hivyo kwa maelezo haya sasa ni kuwa Malighafi karibia zote za kuendesha Mapinduzi ya Nne ya viwanda zinatoka Africa ikiwemo Nchi yetu.
Sasa Fikra zetu tutazibadili vipi na kuweza sisi wenyewe kuwekeza kwenye maeneo yetu, kuchimba na kuongeza thamani ya madini haya na mwisho wa siku tuweze kutengeneza vifaa vinavyotokana na madini tuliyonayo kama taifa. Inawezekana kabisa Tanzania tukatengeneza Betri za magari wenyewe, inawezekana kabisa Tanzania tukatengeneza Vifaa vya kielektroniki kutokea hapa na vyenye ubora wa hali ya juu vitakavyokidhi viwango kimataifa, yaani inawezekana kabisa tukawa "Exporters".
Lakini tu kama tutabadilisha fikra zetu kutoka kwenye kusoma kukukariri ili tufaulu mtihani na kupata vyetu, na kuibadilisha elimu yetu kuwa ya kusoma ili tuelewe na tufanye kwa vitendo zaidi yaani tutumie muda mwingi kufanya kwa vitendo. Mfano mzuri ni vyuo vyetu vya VETA. Watu wengi huwa wanadharau vyuo hivi na kuonekana ni vyuo vya walioshindwa lakini ukweli ni kuwa Vyuo vya VETA vinatoa elimu inayomfanya mwanafunzi ajiamini na awe amekamilika. Unaweza kufanya jaribio kwa kumchukua Mwanafunzi aliyemaliza Degree ya kwanza ya Uhandisi umeme (Miaka 4) na Mwanafunzi wa VETA kwa fani ya umeme (Miaka 3), wape "Motor" ambayo nzima pamoja na vifaa na chanzo cha umeme, kisha waambie "Motor" hiyo iwake ndani ya dakika 45. Wapime kuanzia jinsi ya kujiamini kufanya, matumizi ya muda, utumiaji wa vifaa n.k. majibu utayapata.
Mfano mwingine mchukue tu Mhandisi wa Umeme kutoka Taasisi kubwa ya masuala ya Umeme hapa nchini kwetu, na Mhandisi wa Umeme kutoka Nchi za Magharibi halafu wape kitabu chenye maelezo ya taratibu zinazotumika kupima na kuipata Nguzo ya Umeme yenye ubora unaohitajika kwa matumizi hayo. Halafu uone nani atafuata maelekezo ya kitabu na kuwa na msimamo kile kilichoandikwa na nani atakupa sababu za uzoefu kwa kufanya kazi kwa mazoea huko alikotoka. Hii ni mifano michache tu ya kwanini tubadilishe Fikra zetu kama kweli tunataka kukimbia mbio sawa na Dunia inavyokwenda kwenye Nyanja ya Teknolojia.
Tanzania tunapaswa kujitafakari na kuchukua hatua haraka zaidi ili tuondokane na utegemezi, vijana wengi wanamaliza elimu za juu na wanabaki kuwa tegemezi tena kwa wazazi na jamii, wanaona hakuna tumaini tena wanajiingiza kwenye mambo yasiyofaa. Vijana wengi hivi sasa wamejiajiri kwenye "Betting" ukimfuata ukamuuliza atakwambia ana Shahada ya "Mineral Processing" au Uhandisi Kompyuta. Kwa sababu hata kwenye soko la ajira la ndani hawafai, soko la nje ndio kabisa hawawezi hata kuitwa kwenye Usaili wa Mchujo. Yatupasa tuwape elimu ambayo itamtoa kijana mwenye kujiamini na kujua nini anafanya, kuanzia shule za msingi mpaka vyuo vikuu Wanafunzi wanapaswa kutumia muda mwingi maabara, kwenye karakana kufanya vitu kwa vitendo yani kama wanavyofanya TAASISI YA TEKNOLOJIA DAR ES SALAAM kwa baadhi ya "Course" yaani Mwanafunzi anapimwa kwa Nadharia 40% na Vitendo 60% yaani "COMPETENCE BASED CURRICULUM".
Hapa tutafanikiwa kuwapa vijana wetu uwezo wa kufanya vitu vikubwa, na watu hawa hawatawaza kumaliza chuo waanze kukimbizana na Ajira chache zilizopo. Watu hawa watawaza kutengeneza ajira kwa wengine kwa sababu watakuwa na uwezo wa kufanya vitu vinavyoonekana na vyenye kugusa wengi, kwa sababu kwa sasa TEKNOLOJIA NDIO UCHUMI. Ukienda Hospitalini, Taasisi Nyeti kama Majeshi, Biashara kubwa zinafanya kazi kwa Teknolojia na Bunifu zilizobuniwa na Wanafunzi waliowatengeneza, sisi tunaishia kununua Teknolojia hizi kwa gharama kubwa.
Madhalani mifumo kadhaa inayotumika kwenye baadhi ya Taasisi zetu ni mifumo ambayo imetengenezwa nje na sisi tumeuziwa tu. Lakini ukiangalia tunao Mabingwa wa kufanya "Computer Programming" hapa nchini lakini hawawezi kuaminika kufanya hizo kazi, matokeo yake tunatangaza Tenda na makampuni ya nje yanashinda.
Utashangaa chuo kinatoa "Course" ya Uhandisi ujenzi ngazi ya Stashahada na Shahada ya Kwanza na ukiangalia mazingira ya Chuo mvua zikinyesha maji yanajaa eneo zima la chuo hakuna pa kupita. Kwa nini hatuwezi kuwapa wanafunzi tunaowazalisha, kazi ndogo ndogo za ujenzi watumie yale maarifa wanayopata darasani kuziondoa Changamoto zinazowazunguka. Tusipowaamini sisi nani atawaamini?. Inawezekana kabisa tukaweka mfumo vizuri, kuwa mwanafunzi akifika mwaka wa pili mathalani fani za Uhandisi Ujenzi, Uhandisi Umeme, Mitambo, Computer, Mawasiliano Angani n.k yaani fani zile za Ufundi na Teknolojia, wakaunda vikundi na kusajili kama Kampuni zisizo na usajili wa kudumu, wakawa wanapokea Tender za ujenzi na ukarabati, ambazo zinatolewa na vyuo vyao. Hii itawaongezea ujuzi na pia itawapa uthubutu kwenye kile wanachofanya.
Baada ya kukaa kusubiri mafunzo ya vitendo viwandani ndo wakapate ujuzi ambayo ni muda Mfupi tu haizidi miezi Mitatu (3), Bahati mbaya kuna baadhi ya sehemu hawataki kabisa kupokea Wanafunzi. Pia tuweke Mkazo kwa Bunifu wanazofanya ili ziwe ndio Ajira zao baada ya kumaliza vyuo.
Tubadilishe Fikra na Mitazamo yetu, tuondokane na utegemezi, tuukimbize uchumi wa Dunia kupitia maendelea ya Viwanda kwa kasi ya 6G (100Gbps).

Upvote
3