Tubadilishe mnyama wa Taifa asiwe Twiga

Simchezo

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2012
Posts
460
Reaction score
373
Taifa kuchagua mnyama fulani kama Nembo ya Taifa kuna madhara yake! Taifa hilo litabeba kwa kiasi fulani tabia za huyo mnyama/ndege.

Tanzania mnyama wetu ni Twiga, nimefuatilia baadhi ya tabia zake, nikaogopa! Hizi ni baadhi ya sifa/tabia zake;
1. Ni mpole kupita kiasi.
2. Atoi sauti inayojulikana (bubu).
3. Pamoja na nguvu na ukubwa wake ni muoga, anaweza kimbizwa na mtoto.
4. Wana tabia za homosexuality

Hizi ni baadhi ya sifa mbaya ambazo zinaweza kuliganda Taifa! Turekebishe kwenye katiba. Afadhali tumtumie Simba mangu (Caracal)

Asanteni.
 
Taifa kuchagua mnyama fulani kama Nembo ya Taifa kuna madhara yake! Taifa hilo litabeba kwa kiasi fulani tabia za huyo mnyama/ndege.
Moja kwanza tuanze hapo kwenye hio premise unaweza uka-jenga hoja kubwa, ndefu na nzito ila kama zimesimamia msingi hafifu / usio na nguvu hoja hizo zinakuwa Void Ab Initio.....

Ukimaliza kujibu hilo niite niendelee kupangua Hoja zako kama unadhani one to one Man amano - Simba anaweza kumdhibiti Twiga
 
Simba mangu ni Caracal!!! sio Lion.
 
Simba mangu ni Caracal!!! sio Lion.
Na ushaona hawa wanawawinda Twiga ?

A giraffe can kick in any direction and in a manner of ways, and its kick can not only kill a predator, but has even been known to decapitate. Unsurprisingly, very few predators bother an adult giraffe.
 
Twiga ni mnyama wa amani, maridadi na mwenye uwezo wa kuona mbali.

Atabaki kuwa nembo ya taifa letu. 🦒
 
Ukamuulize simba kama twiga ni mpole, akusimulie mateke yake
 
Usiturudishe Nyuma Kujadili Mijadala Iliyofungwa Zamani Sana
Jamhuri Ya JF Tulikubaliana Zamani Kuhusu Kamanda Nyegere Awekwe Pale Haraka
Twiga Atupishe, Ametuchelewesha Kwenye Mambo Mengi Sana Ya Maendeleo



Hata Tanesco Wamuondoe Tuepuke Umeme Kukatika Hovyo Hovyo
 
Tuchague huyo mwamba😂
 

Attachments

  • Animals-With-the-Toughest-Skin-Honey-Badger-768x401.jpg
    51.3 KB · Views: 5
mi napendekeza yafuatayo
1.mnyama awe fisi kwa sababu watanzania ni waoga na hawatosheki (wezi wa mali za umma)

2.Nembo ya bibi na bwana yule bibi aongezewe wowowo!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…