Tuchukue tahadhari sana Corona sasa ipo DRC congo!

Tuchukue tahadhari sana Corona sasa ipo DRC congo!

Duh Noana hata Australia na Wahindi pia, sema hao hawapigi makelele sana kama Marekani na Uropa.
Sababu ni kuwa kiasi cha wanaoambukizwa Marekani kulinganisha na kile wanachopona ni ndogo. Pia Ulaya watu wanaishi karibu karibu tofauti na Urusi, hivyo kuna hatari kubwa ya maambukizi. Ukiangalia wataliano, wao wanautamaduni wa kusikanashikana sana, huenda imesababisha wao kuupata wengi.

Nimekokotoa hapo chini asilimia za waliopona kwa walioathirika.

China 76%
Iran 33%
Australia 19%
Urusi 15%
Italia 7%
India 7%
Marekani 0.7%
 
hivi yule mwanamziki mkongo aliyekuja kuimba mayenu hapa
alihakikiwa virusi vya corona
 
Hii kitu iliyotua nchini Congo(bbc)leo asubuhi unaenea kwa kasi kubwa ulaya na sehem nyingine huko.

Bongo bado watu hawachukui tahadhari. Kwenye daladala namuona mteja mwenzangu amenunua mahindi anakula kwenda mbele. Anapukuchua anatafuta kama karanga.

Cha ajabu wengine pembeni tamaa zinatushika, na kutamani tununue, namuona mwingine mzee wa makamo ananunua, yeye analiweka kwenye meno lote, anang'ata mtindo wa kinyaninyani.

Cha kushangaza, kama tujuavyo tunatakiwa kunawa mikono mara kwa mara, sasa sijui wazee kama wamenawa wapi.

Daladala imejaa vby. Hapa tusipojiongeza wenyewe, tutapotea
 
Ukiingia hapa Dsm,tutahitaji neema ya Mungu kwa sababu sidhani kama tutachomoka maisha yetu tunayajua wenyewe hasa kwenye usafiri wa umma na masokoni. Yaani me ningekuwa na uwezo ningefunga mipaka hadi hali ya ugonjwa itakapotulia
 
Wengine Australia huko wametwangana baada ya mmja kukohoa bila kuziba mdomo ndani ya chombo cha usafiri, yan Tanzania tunavopenda kusalimiana na mikono sijui tutachomoka vp
 
sirikirusi,
We are impact/results oriented people, ngoja kwanza lije alafu tuone watu wanadondoka kama wamepigwa shorts za umeme gafla buu chini ndipo tutachukua hatua.

Kwani majanga nchini kama mafuriko mabondeni, kwenye migodi na pale jangwani si yanatuathiri kila mwaka? Je kuna hatua stahiki za kukabiliana na hali hiyo miaka ijayo ambazo imechukuliwa? Hapo ndipo utajua je kweli miradi inayofanyika ina malengo ya kutengezea sustainable people's welfare au ni miradi ya kutafutia kura katika chaguzi zijazo.

Maendeleo ya kweli sio vitu bali watu kwanza then vitu vitafuata.

Reference case: Ethiopia
 
Back
Top Bottom