kalacha mateo
Senior Member
- Sep 27, 2021
- 119
- 240
SHIRIKISHO la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), limesema katika miaka miwili ya uongozi wa Rais Dk Samia Suluhu Hassan amewafanyia mengi wafanyakazi ikiwa ni pamoja na kuongeza mishahara watumishi wa kima cha chini kwa asilimia 23.3.
Katibu Mkuu wa Tucta, Hery Mkunda alisema hayo mjini Morogoro jana kwenye ufunguzi wa kikao cha Baraza Kuu la Tucta uliofanywa na Rais wa shirikisho hilo, Tumaini Nyamhokya.
Mkunda alisema wafanyakazi wamekuwa na matumaini makubwa kwa serikali ya Rais Samia kwa kuwa pia amepandisha madaraja ya watumishi wa sekta mbalimbali za umma.
“Katika kipindi hiki cha miaka miwili alichopo madarakani, mambo mengi ya wafanyakazi ameyagusa na wanatarajia kupata mambo mazuri zaidi katika kipindi ambacho anaendelea kuwa madarakani,” alisema na kuongeza:
“Kweli ukiangalia uwezo wa serikali kwa mambo ambayo iliyaahidi kipindi kilichopita, mengi yamefanyika kwa kiwango kikubwa sana na tunatarajia katika kipindi hiki mambo mengine mengi zaidi yatafanyika.”