PreGE2025 TUCTA Rukwa yawataka wananchi na wafanyakazi wote kushiriki uchaguzi

PreGE2025 TUCTA Rukwa yawataka wananchi na wafanyakazi wote kushiriki uchaguzi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Mpepetaji

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2025
Posts
346
Reaction score
213
Shirikisho la vyama vya wafanyakazi (TUCTA) mkoni Rukwa limetoa wito kwa wafanyakazi na wananchi kwa ujumla kushiriki kikamilifu katika zoezi la uchaguzi ili kupata viongozi bora watakaojali maslahi ya wafanyakazi na kuleta maendeleo ndani ya nchi.

Hayo yamebainishwa na mratibu wa TUCTA mkoani Rukwa ndugu Messe Max wakati wa maadhimisho ya siku ya wafanyakazi ambayo kwa ngazi ya mkoa yamefanyika katika wilayani Kalambo mkoani Rukwa na kuwataka wafanyakazi kushiriki kikamilifu katika uchaguzi ili kupata viongozi watakaothamini haki na maslahi yao ikiwemo kuhudhuria mikutano ya kampeni, kusikiliza sera za wagombea ili waweze kupima na kuwachagua siku ya kupiga kura.

 
TUCTA ilikuwa ya mzee Mgaya peke yake hii ya mapandikizi ya fisiemu haijawahi kutetea lolote yanakenua meno tu ndio yale yale ya Tume huru ambayo sio huru,
 
Nani ashiriki kiini-macho.

Tushawashitakia kwa Muumba, majibu yameshajibiwa, yanafika soon
 
Back
Top Bottom