Yapo ya kujifunza toka kwa Raila, lakini huyo siyo mfano mzuri hata kidogo. Bahati yake ni moja tu kwamba analo kundi la watu wa kabila lake waliko nyuma yake kufa na kupona. Hapa watu kama hao hawapo.
Kwa hali ilivyo sasa hivi hapa nchini, kutokana na kudidimia kulikofikiwa na CCM, CHADEMA wanayo nafasi nzuri kuliko wakati mwingine wowote wa kuwaondoa madarakani.
Kinachotakiwa tu, ni kwa CHADEMA kujipanga vizuri.
Kuna mfano mzuri wanaoweza kuuangalia wakitazama nyuma kidogo ya historia yao na kuanzia hapo.
Wakati ule wa Kikwete walipopata wabunge wengi zaidi Bungeni, pamoja na kwamba palikuwepo na mazingira magumu katika uchaguzi ule.
Warudi nyuma, waangalie walichofanya wakati ule, na kuweka mikakati ya kuzidisha zaidi na kuiondoa CCM.
Inawezekana sana safari hii kuiondoa CCM madarakani. Wananchi wenyewe wapo tayari kwa hilo..
Ndiyo maana tunawahimiza, wajizatiti tokea sasa kwa kuweka mikakati itakayowezesha hayo yatokee.
Haya siyo maneno matupu, wafungue tu akili na kuwa tayari kupokea ushauri na kuufanyia kazi.
Binafsi nimeandika mada kadhaa kwa nini Raila ni mfano mzuri wa kujifunza. Ya msingi:
1. Raila ana uzoefu wa kuipambania haki kwa miongo mingi.
2. Raila kapigania haki tangia enzi ymza chama kimoja, tume za uchaguzi zisizokuwa huru hadi kwenye tume zilizo huru.
3. Raila amewahi ku prevail mahakamani kuhusiana na uchaguzi mkuu.
4. Raila kapambana tokea nje ya chama tawala, ndani ya chama tawala, na pia akiwa na rais aliyeko madarakani madarakani.
5. Raila anajua maana ya agenda ya kudumu, dhidi ya marafiki na maadui katika siasa.
6. Raila anajua kuhamasisha umma. Kudhania kundi lake ni la wajaluo tu itakuwa kutojitendea haki.
Ikumbukwe pamoja naye Raila leo ni Uhuru Kenyatta, Martha Karua, Kalonzo Musyoka na vigogo wengi wengine na vyama vyao ambapo wala si wajaluo.
"Ngoma hii inapendeza kuzicheza kutokea ndani si kutokea nje. Ni Imani yangu aghalabu, yetu kutokea ndani; kuwa hadi leo hakuna lisilofahamika ndani ya Chadema."
Ideas?! Hapana! Ninadhani tatizo kubwa ni kutokukubaliana na Hali halisi.
Niliwahi kuandika mada yenye msingi huu kuwa ilipo Chadema haihitaji mawazo tena. Inahitaji kuchukua hatua tu ndicho kilichobakia.
Ni aibu kuwa chama chenye wanachama 8m+:
a) kinashindwa vipi kufanya maandamano au migomo yenye madanikio?
b) kinashindwa vipi kuzuia uchafuzi wa chaguzi?
c) kinashindwa vipi kushinikiza agenda zaje?
d) nk.
Kwenye chama hiki la kwanza sasa la kufanya ilikuwa ni kupanga safi sahihi za uongozi kidemokrasia na kwa uwazi kabisa kupitia primaries kama kwake Beberu.
Ni muhimu viongozi wenye uthubutu wakakabidhiwa chama, wenye kusita wakapisha damu mpya. Damu mpya ipo na haitakaa kwisha.
"Tusiandike kuwashauri Chadema sisi kama outsiders. Tuandike kujishauri wenyewe kama wenye shughuli."
Utamu wa Ngoma .... tena yakhe!