Tonytz
Senior Member
- Jul 18, 2022
- 159
- 1,142
UTANGULIZI
Kwanza napenda kumshukuru Mungu kwa pumzi ya uzima na uwezo wa kuniongoza katika kuandika Makala hii yenye kuleta tija hapa nchini Tanzania na duniani kwa ujumla.
Pia, nawashukuru na kuwapongeza JF kwa kuweka shindano hili na jukwaa hili ili kuinua vipawa vy vijana wengi hapa nchini. Pia nazidi kuwashukuru wasomaji wetu na wapiga kura wetu kwa msaada wenu wa kutupigia kura.
DHANA YA LUGHA YA KISWAHILI.
Lugha ya Kiswahili ni lugha iliyotokana usanifishaji wa lahaja ya kiunguja, ambapo kukawa na msawazo wa maneno na herufi ili kuifanya lugha hii kuwa na utajiri wa misamiati na maana katika utumizi na kuwa chombo cha mawasiliano kwa upwa wote wa Afrika Mashariki.
Lugha ya Kiswahili ni lugha ya kimawasiliano nchini Tanzania na nchi nyingine duniani haswa upwa wote wa Afrika Mashariki ambapo kwa sasa Kiswahili kinazidi kupasua anga kimatumizi katika mawasiliano. Lakini pamoja na kuwa mataifa mbalimbali yanatambua umuhimu wa lugha ya Kiswahili lakini bado kwa wazawa imekuwa tofauti kwa kuona Kiswahili kama hakina hadhi kulinganisha na lugha zingine.
Hii ni kutokana na ukweli kuwa baadhi ya nyaraka za kiserikali, mikutano, warsha, seminar, mikataba na taarifa mbalimbali za miradi na mengineyo hapa nchini kwetu kuandikwa kwa lugha za kigeni na kuendeshwa kwa lugha za kigeni, ambapo siyo sawa kwa wazawa na hudidimiza haki za wazawa wa lugha, hapa Watanzania.
Hapa tujiulize swali la kujifunza, kwanini tutumie lugha za kikoloni katika mikataba na nyaraka baadhi za kiserikali au mashirika binafsi? Ikiwa idadi kubwa ya wazawa wanakifahamu Zaidi kukisoma, kukiandika Kiswahili, kwanini tusikitumie kwenye sehemu hizo ili kuleta tija kwa watumiaji wa lugha ya Kiswahili?
Je, ni kweli tuna uhuru wa lugha yetu ikiwa bado tunafungwa na lugha za kikoloni? Kuna haja ya kuongeza jitihada Zaidi kwa ushirikiano wa serikali na wananchi. Unaweza kujiuliza kuwa kwanini kidumishwe kwa maendeleo endelevu?
UMUHIMU WA KUDUMISHA LUGHA YA KISWAHILI.
Kwanza, huchochea maendeleo, kwani huwa ni nyenzo kuu ya mawasiliano miongoni mwa watumiaji wa lugha hii.
Pili, huchochea kujua haki zetu na kudai haki zetu, hii ndiyo maana ni vema mikataba na nyaraka za kiserikali kuandikwa kwa lugha ya Kiswahili.
Tatu, uhimarisha uhusiano mzuri pamoja na kujenga Amani miongoni mwa watumiaji wake na wazawa wote.
Nne, ni nyenzo kuu ya kufundishia, kwa sasa Kiswahili kinatumika sana katika ujifunzaji na ujifundishaji, hii ni tija ambayo mpaka sasa kuna mjadala kuwa Kiswahili kiwe lugha ya kufundishia hapa nchini kwetu. Hizo ni faida kadhaa tu za kudumisha Kiswahili miongoni mwa faida lukuki zinazofahamika.
TUNAWEZAJE KUDUMISHA LUGHA YA KISWAHILI NA KUKIFANYA KUWA NYENZO YA KUDAI HAKI ZETU NA KICHOCHEO CHA MAENDELEO ENDELEVU?
Ni jukumu letu sote kudumisha lugha hii ya Kiswahili ili kuleta maendeleo endelevu na kuwa nyenzo ya kudai haki. Pengine unaweza kujiuliza itawezekanaje?
Ni rahisi sana. Ikumbukwe tu kuwa mabadiliko yanaanzia ndani kisha kusambaa nje. Hivyo serikali ikiwa ndiyo kiungo kikuu cha kutuongoza katika kutimiza haya kwa kuwa mfano anuani wa haya yote, kwa pamoja yatupasa kufanya haya;
Kwanza, kukiidhinisha kuwa lugha ya kufundishia, hii naomba ifahamike kuwa kukifundishia tu haitoshi bali na mifumo ya maisha katika Nyanja hii iendane na matakwa ya lugha. Hapa yatupasa kujidhatiti kwa kuwafanya kila Nyanja isistize matumizi ya lugha ya Kiswahili. Hii itaimarisha maana ya kukifanya kuwa lugha ya kufundishia.
Pili, kwenye suala la mikataba ya ajira na kazi zingine ni vema iandikwe kwa lugha ya Kiswahili. Kwanini hii ni muhimu? Ni muhimu kwa kuwa itamwezesha mwajiriwa kujua masharti na vigezo vya ajira yake kwa urahisi na bila kuhitaji ufafanuzi mkubwa.
Mikataba inapoandikwa kwa lugha za kigeni ni dhahiri kuwa ni hali ya kufinya haki za mwajiriwa ambaye pengine hana ujuzi mkubwa na lugha ya kigeni iliyotumika, hivyo anaweza kukubali chenye athari kwake.
Tatu, taarifa za miradi mbalimbali inayotekelezwa hapa nchini kwetu ziwe katka lugha ya Kiswahili, hii itamfanya mzawa kuelewa kwa urahisi kinachoendelea.
Nne, nyaraka za wizara mbalimbali ziwe katika lugha ya Kiswahili, hii itadumisha na kukifanya Kiswahili kuwa nyenzo ya kudai haki.
Tano, usahili wa ajira (interview) uendeshwe kwa lugha ya Kiswahili, hili litaleta tija sana, mtu anaweza akakosa nafasi ya kazi kwa kisa cha kutojua vema kiingereza kwenye kuongea na kuandika. Mimi ni Mtanzania mzawa wa lugha ya Kiswahili, iweje unisaili kwa lugha ya kigeni? Hapa hakuna haki.
Sita, katika vitu na vifaa ambavyo tunavitumia kama vile, madawa maelekezo yake yatolewe kwa Kiswahili, hii itadumisha lugha yetu na kupelekea maendeleo makubwa. Siyo wote wenye uwezo wa kuelewa lugha za kigeni katika maelekezo ya vitu vya kutumia.
HITIMISHO
Haya ni baadhi tu ya mambo ya kuzingatia katika kukifanya Kiswahili kuwa nyenzo ya kudai haki na kuchochea maendeleo katika nchi yetu. Naipongeza serikali kwa jitihada zake za kukifanya Kiswahili kithaminike ndani na nje ya nchi yetu.
Jitihada hizi zimejidhihirisha kwa kuweka kipaumbele kwenye mikopo kwa wanafunzi watakaosoma Kiswahili, kuwepo na mianya ya ajira nje ya nchi kwa walimu wa Kiswahili kutoka vyuoni mwetu.
Kuwepo na warsha na makongamano ya Kiswahili nchini, kama hii haitoshi, kuwepo na siku ya Kiswahili duniani tarehe 7/7 kila mwaka inafungua mwanya Zaidi kwa mataifa kuona ukubwa wa lugha hii ya Kiswahili, kuwepo na vyuo nje ya nchi vinavyofundisha lugha ya Kiswahili ni harakati tosha za kudumisha lugha lugha hii inaonesha ni kweli kuwa Kiswahili ni TUNU yetu.
Chanzo: Picha mtandaoni.

Upvote
113