Kuna jambo moja unapaswa kulielewa hata kama hautalikubali....Mtoto aliyezaliwa na Mariam aliitwa Yeshua hilo ndio jina lake halisi na amekua akiitwa kwa majina tofauti kulingana na mila na tamaduni za sehemu tofauti bila kupotosha maana ya jina lake la kiebrania,,, maana ya Yeshua kwa kiebrania ni mwokozi na kwa lugha ya kiarabu Issa ina maana hiyohiyo.
Kwahiyo Issa ndio huyohuyo Yesu ila kwenye Biblia imemuelezea zaidi maisha yake kuliko kwenye Quran, na Wakristo wengi wanaamini huyo ni Mungu,,,waislam na wayahudi wanamtambua kama mtume wa Mungu na sio Mungu mwenyewe.
Sasa kama wayahudi wenzake wamemkana kwamba sio Mungu,,,kuna ajabu gani waislam wakimtambua kama nabii na sio Mungu mwenyewe?