Tuelimishane hapa kuhusu hii bahati na sibu ya BIKO

Habari wanaJf!

Kama kichwa cha habari kilivyo, Tatu Mzuka na Biko yote ni michezo ya bahati nasibu kupitia simu yako hapa Tz, kama tunavyo sikia/angalia matangazo yao kwenye vyombo vya habari.

Mara ya kwanza nilianza kuusikia huu Mchezo wa BIKO, lakini juzi tu hapo nikasikia tena kuna mchezo mwingine tena unaitwa TATU MZUKA.

Swali langu mimi je kuna mtu alishawahi kushinda kwenye hii michezo? Maana nasikia ukiweka dau unashinda mara 200 ya dau lako.

Na ni mchezo gani ni rahisi kushinda?

Kwa yeyote mwenye ushuhuda na hii michezo aje atujuze ili na sisi wengine tuanze kucheza kama kuna unafuu, maana maisha mtaani ni magumu.

......Nawasilisha.....
 
Biko mimi nimecheza mara kadhaa.
Kushinda droo kubwa ya milioni 20 probability ni 0.000001%.
Droo ndogo za siku kushinda ni kama 0.02% kwa kila buku unayocheza.
Ni vyema kujaribu bahati ila angalia usitumie fedha ulizozitenga kwa ajili ya mambo mengine.
Ni heri kwenda kucheza premier betting game la odds au farasi kule hakuumizi sana mie nilicheza huko zamani wakati naishi kwa kuungaunga.
Sasa nimeacha, mimi na wife kwa sasa tunacheza biko siku tunapopata pesa isiyo katika bajeti zetu.
 
duh! hizo asilimia za makadirio ya ushindi, zimeniacha hoi kabisa
 
Biko Ni Sawa Na Tola Mla Gizani Hata Droo Huoni Likichezeshwa Au Point Zako.
ha ha ha!!! ume nikumbusha mbali sana, Mzeetola!!... Lakini mbona zote mi naona kama zinafanana kwa uchezaji wake
 
Biko nani anapata million1 au elfu 20,angalau million20 tunadanyika kwa kuwaona washindi
 
Mimi sijawahi kuicheza ila jamaa yangu huwa anacheza na kupatia sema hii michezo siiamini sana bora ukafanya betting
 
Biko nani anapata million1 au elfu 20,angalau million20 tunadanyika kwa kuwaona washindi
tangu nime anza kuisikia hii michezo sijawahi ona hata mmtu mmoja anakuja kutoa ushuhuda, hata kwenye huu uzi sioni
 
Ukisikiliza hizi radio mbao utaona tatumzuka rahisi kumbe hata hawa watangazaji wanaoipromote hawaelewi au wanapotosha makusudi jinsi ambavyo mtu anashinda, ikanibidi nijaribu kuitafuta hii taasisi yenye dhamana ya tatu mzuka,maajabu sikuona hata website yao bali nilipelekwa kwenye Facebook page,kule nilibahatika kusoma maelezo ndio nilipogundua kuwa ukiwa na akili huu mchezo ni mgumu sana kushinda maana ili ushinde lazima namba zote tatu zitoke ndio wanazidisha Mara 200 ya hela uliyoweka, ila zikitoka 2 wanazidisha Mara 2 ikitoka moja nahisi umepigwa hawakuweka wazi.

Kwa kifupi bora ubet unaona Chelsea na Arsenal wanatoa Gg unapata hela kuliko upatu huu unaoanzishwa hata hauonyeshi nani mmiliki hata website ya kuelemisha hamna.

Nani alaumiwe? Napeleka lawama gaming board hawafuati standard kabisa kampuni zinajianzisha kiholela tu,haiwezekani serikali iruhusu wananchi wacheze mchezo hawajui nani custodian wa hela zao eti simply tu kwavile unatangazwa na radio.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kweli mkuu...makampuni husika hayajatoa elimu ya kutosha kuhusiana na hii michezo, yani wameandika juujuu tu
 
Ni heri kununua mbwa kwamba waweza kumtumia kuwinda visungura.
kama ni hivyo basi bora nikacheze kamali ya makato (kalata) ingawa hii kamali inapigwa marufuku sana wakati na yenyewe ni ya bahati nasibu
 
Back
Top Bottom