je parle
JF-Expert Member
- Nov 28, 2018
- 2,022
- 3,919
Jana nafika dukani usiku kununua maharage kilo naambiwa 3,800 na kesho huenda tukapandisha kuwa elfu 4 kamili.
Nimeshindwa kuelewa shida ipo wapi maana mwezi wa nne yalikuwa 1,700 yakapanda 2,000 hadi 2,400 sasa huku tunapoenda tutakula tu ugali na kachumbari. Vitu vyote vimekuwa juu mno, kama unaishi kwenu huwezi kulijua hili.
Ukienda sokoni unaweza kuzimia, maana nazi nzuri inaanza 1,400 mihogo ndio usiseme, viazi vitamu ndio usiulize hata bei mana ndoo ndogo ilikuwa elfu 5 hadi 7 sasa hivi ni elfu 12.
Hii nchi tunapoenda tutauana kwa njaa, watu hawashibi ndio maana wana kuwa na stress za hapa na pale.
Note, nadhani wakulima mwaka huu watajenga maghorofa kama madalali sio wanaopandisha bei.