Tuendako hali inatisha. Sasa maharage yanakimbilia kilo moja elfu 4 (4,000)

Tuendako hali inatisha. Sasa maharage yanakimbilia kilo moja elfu 4 (4,000)

Nunua yale madude ya cement ya kupandia maua. Badala ya maua panda nyanya chungu, hoho, mnafu, pilipili, na mboga zingine. Kama una eneo kubwa panda mti wa kisamvu. Nyanya chungu, tunda na majani yake vyote mboga. Mti wa kisamvu ukiumwagilia ni mboga siku zote. Jiongeze.
 
Dah kuikweli Hali ni mbaya kila kitu kinapanda Bei tunakoenda hata Kodi za pango zitaongezeka ....hapo hapo unakuta majitu yanajipitisha Mara hela ya ulinzi shirikishi Mara hela ya taka siku....wanaowatuma siku watakuja waokote mizoga yao mtaani ...watu wamechoka
 
Achana na maharage kula mchicha,figiri...mnafu.Chinese,njegere mbichi...viaz...
 
Mnapoambiwa mzae kidogo mnaiambia serikali na kutukana mabeberu eti mnatafuta soko la ndani.

Wenye familia ndogo hata hawawaz kuhusu msosi,

Endeleeni kuleta vibarua duniani.
Kwamba tunazaa vibarua...[emoji28][emoji28][emoji2297][emoji2297]
 
Jana nafika dukani usiku kununua maharage kilo naambiwa 3,800 na kesho huenda tukapandisha kuwa elfu 4 kamili.

Nimeshindwa kuelewa shida ipo wapi maana mwezi wa nne yalikuwa 1,700 yakapanda 2,000 hadi 2,400 sasa huku tunapoenda tutakula tu ugali na kachumbari. Vitu vyote vimekuwa juu mno, kama unaishi kwenu huwezi kulijua hili.

Ukienda sokoni unaweza kuzimia, maana nazi nzuri inaanza 1,400 mihogo ndio usiseme, viazi vitamu ndio usiulize hata bei mana ndoo ndogo ilikuwa elfu 5 hadi 7 sasa hivi ni elfu 12.

Hii nchi tunapoenda tutauana kwa njaa, watu hawashibi ndio maana wana kuwa na stress za hapa na pale.

Note, nadhani wakulima mwaka huu watajenga maghorofa kama madalali sio wanaopandisha bei.
Hakuna mkulima ananufaika hapo mkuu. Walanguzi na madalali wameshanunua mazao ya wakulima kwa bei chee......wanasafirisha mazao nje na kusababisha uhaba, na serikali inawapetipeti wakifikiri wakulima ndo wanaokula shavu, nchi ishakuwa bora liende...​
 
Ukianza kuona 10000 unakwenda nayo Dukani na unarudi na Vitu vi 2 au vi3 Tu na hakuna Chenji na mangi Dukani anakudai hapo lazima kichwa kiwake moto
 
Kula kitu kingine mkuu si lazima maharage.

Kwanza ulaji wa mara kwa mara wa hayo mazao makabu kunaleta udumuvu, mengi hiwa na sumu kuvu na madawa ya uhifadhi nafaka.
Umeshawahi kula wali maharage wewe? Au unaongea tu?
 
Athari zitokanazo na mabadiliko ya tabia nchi ni janga la kidunia, ndiyo maana mfumuko wa bei umeathiri dunia nzima. Kukabiliana na changamoto hizi, inahitaji mabadiliko ya kisera, ili kuruhusu miradi ya umwagiliaji zaidi ili kukabiliana na hali ya tabia nchi
 
Ukilima kipindi hiki inakula kwako. Issue ni kuwa na mtaji alafu kununua kidogokidogo kwa wanaolima.

Wengi hawapati kitu kwa kuwa Hali ya hewa sio nzuri.

Sasa hivi kwa ekari kutoa hata gunia 5 tu imekua mtihani.
Jinga ww kwahy wote wakifuata huu ushauri wako hao wajinga wenzako watanunua wap muwe mnatumia akili

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jana nafika dukani usiku kununua maharage kilo naambiwa 3,800 na kesho huenda tukapandisha kuwa elfu 4 kamili.

Nimeshindwa kuelewa shida ipo wapi maana mwezi wa nne yalikuwa 1,700 yakapanda 2,000 hadi 2,400 sasa huku tunapoenda tutakula tu ugali na kachumbari. Vitu vyote vimekuwa juu mno, kama unaishi kwenu huwezi kulijua hili.

Ukienda sokoni unaweza kuzimia, maana nazi nzuri inaanza 1,400 mihogo ndio usiseme, viazi vitamu ndio usiulize hata bei mana ndoo ndogo ilikuwa elfu 5 hadi 7 sasa hivi ni elfu 12.

Hii nchi tunapoenda tutauana kwa njaa, watu hawashibi ndio maana wana kuwa na stress za hapa na pale.

Note, nadhani wakulima mwaka huu watajenga maghorofa kama madalali sio wanaopandisha bei.
TULIENI Kwanza KIKOSI KAZI kinakuja na MAPENDEKEZO ya BEI ya MAHARAGE
 
Back
Top Bottom