Tuendako hali inatisha. Sasa maharage yanakimbilia kilo moja elfu 4 (4,000)

Nimempa ushauri afanye option nyingine zaidi ya maharage sababu zipo mboga bei nafuu zaidi ya maharage...
Kuna ambao tunapenda maharage. Options zipo lakini kupanda kwa bei lazima kusemwe.
Je na hizo Options nyingine zikipanda bei itakuaje? Kila chakula kina umuhimu wake
 
Hatari na nusu mwaka huu chupi lazima zivuke imagine una wake wanne na watoto 10 halafu huna mishe za kueleweka lazima usaidiwe kutoa dozi maana nguvu za mashaka.
... kuna mtu ana watoto 10 na wake wanne karne hii? Kuna mahali pana biashara ya kuuza watoto?
 
Kuna ambao tunapenda maharage. Options zipo lakini kupanda kwa bei lazima kusemwe.
Je na hizo Options nyingine zikipanda bei itakuaje? Kila chakula kina umuhimu wake

Hatuwezi kuzuia kupanda bei ya vyakula, hata serikali haiwezi kuzuia kwa kuwa uzalishaji umeshuka kutokana na uhaba wa mvua, hata serikali hai...

Sasa sisi kama walaji yatupasa tutafute vyakula mbadala tu hakuna jinsi...

La hasha nunua stock nyingi weka ndani wakati ambao bei ni nafuu, lakini hatari ya kustock vitu vikavu muda mrefu ndio hiyo nilitaja uwezekano wa kula sumu kuvu...
 
Hatuwezi kuzuia kupanda bei ya vyakula, hata serikali haiwezi kuzuia kwa kuwa uzalishaji umeshuka kutokana na uhaba wa mvua, hata serikali hai...
Duh kwahio haya mambo ya uhaba wa Mvua na Ukame ni mambo mageni ? , Kwamba Mvua na hizi tabia nchi sio za kutegemea ?, Kwanini Serikali isijitayarishe for the worse ?!!!
Sasa sisi kama walaji yatupasa tutafute vyakula mbadala tu hakuna jinsi...

La hasha nunua stock nyingi weka ndani wakati ambao bei ni nafuu, lakini hatari ya kustock vitu vikavu muda mrefu ndio hiyo nilitaja uwezekano wa kula sumu kuvu...
Individually tuna wajibu wa kujisaidia ila Serikali pia watumishi wetu tunaowalipa inabidi waje na njia mbadala...,

Mfano kuhakikisha kuna maghala hence storage ya kutosha kunapokuwa na over supply (mfano mwaka juzi tu wakulima wamekosa soko kwa kuwa na bidhaa nyingi hadi kuozea mashambani) hence kipindi hicho wangenunua kwa bei nafuu na kuyahifadhi kipindi hiki kwenye scarcity wakatoa mzigo ili kubalance bei.....

Sasa kama hawawezi kufanya hata hili wapo pale kufanya nini ?, Mfanyabiashara yupo pale ku-make as much profit as possible huwezi kumtegemea...
 
Wewe akili zipo sio wale wanaolazimisha bidhaa ishushwe bei kwa kufunga mipaka bila kumjali mwenye bidhaa.
 
Dagaa, samaki, nyama, mchicha, ndio chakula kizuri nakuunga mkono maharage naona msaada wake ni mdogo maana yanajaza gesi tumboni tu
 
(mfano mwaka juzi tu wakulima wamekosa soko kwa kuwa na bidhaa nyingi hadi kuozea mashambani)
Malalamiko, lishwalishwa hawakuishinikiza serikali kununua kwa bei nzuri wahifadhi ili mkulima asipate hasara wanatokwa na mishipa bei ikiwa nzuri tu.
 
Mnajitahidi sana kumtetea mama yenu sisi yetu macho.
 
... kuna mtu ana watoto 10 na wake wanne karne hii? Kuna mahali pana biashara ya kuuza watoto?
Wapo wengi tu kama wewe una nguvu za kiume za mashaka sema tuje tukusaidie endapo kama una hitaji watoto wengi.
 
Mnapoambiwa mzae kidogo mnaiambia serikali na kutukana mabeberu eti mnatafuta soko la ndani.

Wenye familia ndogo hata hawawaz kuhusu msosi,

Endeleeni kuleta vibarua duniani.
Kwa akili yako ilivyo ndogo unafikiri waathirika wa huu mfumuko wa bei ni kwa wenye familia kubwa pekee.Kama mwanafunzi au bachela alikuwa anaweza kuishi kwa 4500/= kwa siku, sasa inabidi awe na bajeti isiyopungua 8000/= sababu chakula kwa mama ntilie sio buku jero tena na kipato chake hakijaongezeka.
Mwafrica ni kiumbe wa ajabu sana, yani unamdharau na kumthihaki mwenzako kwakuwa wewe upo kwenye nafasi ambayo madhira hayo hayakupati, tena inawezekana ukawa unakula bure tu nyumbani au marioo ndiomana unaona wengine kama kenge wasiojitambua😎
 
Kula kitu kingine mkuu si lazima maharage.

Kwanza ulaji wa mara kwa mara wa hayo mazao makavu kunaleta udumuvu, mengi huwa na sumu kuvu na madawa ya uhifadhi nafaka.
Ukila kachumbari na mboga za majani ndio balaa kwa madawa....nyanya, kitunguu, spinach, mchicha...balaa tupu. Mpaka pilipili wanaweka mbolea na wanapiga dawa.
Tule nini sasa.
Au tunywe maji ya moto tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…