Jambo hili Lina madhara hasi zaidi kwa nchi kuliko faida.
Taasisi za Serikali ambazo zinapaswa kulaumiwa kwa kuliingiza Taifa kwenye majanga makubwa kutokana na kitendo cha kutoa kiholela Uraia wa Tanzania kwa wageni ni:-
1. Jeshi la Uhamiaji.
2. TISS.
3. Jeshi la Polisi.
Kuna hatari kubwa sana kutoa uraia kiholela kwa Watu wa nje. Hivi wanajua sababu mahsusi ambazo Rais wa Marekani Donald Trump katika awamu yake ya kwanza aliamua kuwapiga marufuku Raia wa Tanzania kupewa Viza au Uraia kwa njia ya GreenCard kwenye nchi hiyo? Wanazijua sababu zake?
Uhamiaji, TISS na Polisi wanajaribu kuweka rehani usalama wa umma wa waTanzania, ni hatari kubwa sana. Hivi ni kwa nini hasa Serikali ya Tanzania inakataa kuwaruhusu diaspora wa Tanzania kuwa na uraia pacha lakini wakati huo huo inaruhusu kiurahisi kabisa bila ya kufuata Sheria kuwapa uraia wageni ambao kamwe hawakuwahi kuwa na vinasaba kabisa na nchi ya Tanzania?