mtoa mada, asante kwa ushauri, ila naomba kusaidiwa mambo yafuatayo kama utayaweza.
1.kwanza ugonjwa kama huu ulio msumbua mheshimiwa rais, unasababishwa na nini?
2.Pili ni dalili gani mgonjwa anaweza kuzipata akiwa na ugonjwa huo?
3.Mwisho ungonjwa huo ni mbaya sana kiasi kwamba mtu akizembea unaweza kuleta madhala makubwa? na kama ni ndio ni madhala gani? tatizo uku bongo siasa nyingi habari za afya zetu hatuzingatii sana!!
Kwa niaba ya mtoa mada nitajibu maswali yako hapo juu.
1. Kwanza ugonjwa wenyewe unaitwa
BENIGN PROSTATIC HYPERPLASIA (BPH),i.e
. an enlargement of the prostate gland (kuvimba au kuongezeka kwa tezi ya kibofu.
-Sababu (causes) mara nyingi haijulikani,ingawa unawezakusababishwa na mabadiliko ya homoni (androgens) inayoenda sambamba na utu uzima (hasa kati ya miaka 50+...)
2. Dalili anazowezakuzipata mgonjwa:
-Urine retention (kushindwa kukojoa) sababu uvimbe huwa unaziba njia ya mkojo
-Nocturia (kukojoa mara kwa mara wakati wa usiku)
-Kuhisi kama mkojo haujaisha kwenye kibofu baada ya kujisaidia (sensation that the bladder has not completed emptied).
-Anaweza kupata U.T.I sababu ya urine stasis
-Anaweza kupata hata hydronephrosis (Matatizo ya figo) n.k
Hizo ni baadhi ya dalili ambazo ni common,lakini kwakweli zipo nyingi.
3.Sasa madhala kama mtu akizembea ni pamoja na hilo nilisema hapo juu,yaani Hydronephrosis.
-Mengine ni kama uharibifu (damage) wa kibofu cha mkojo,muscles zinalegea hata kushindwa ku-control flow ya mkojo kutokana na pressure inayoongezeka kwa sababu ya mkojo kushindwa kutoka.
-U.T.I n.k
Nadhani umenielewa kidogo mkuu.