Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
Kuna clip inazunguka mitandaoni ikieleza mengi kuhusu Tanganyika.
Kubwa linaloshtua watu wengi ni kusema imani kuu nchini ni Ukristo.
Nimeandika makala hiyo hapo chini kutanabaisha kuhusu historia ya Tanganyika nikijaribu kueleza imekuwaje tumefikia hali hii:
Alikuwa Dr James Kwegyir Aggrey, Mwafrika kutoka Ghana ndiye mtu aliyemtia Kleist hamu ya kuingia katika siasa. Dr Aggrey alikuja Tanganyika mwaka 1924.
Dr Aggrey alikuwa katika Phelps-Stokes Commissions iliyokuwa imeundwa kuchunguza elimu ya Waafrika.
Ilikuwa katika kipindi hiki akiwa ndani ya kamisheni hii ndipo alipokuja Tanganyika. Dr Aggrey alikataliwa kupanga New Africa Hotel kwa kuwa alikuwa mtu mweusi.
Ikabidi Gavana Donald Cameron amtafutie chumba Government House ajisitiri kwa malazi.
Wakati huu alipokuwa Dar es Salaam ndipo Dr Agrrey alipokutana na Kleist.
Dr Aggrey alimtunukia Kleist moja ya vitabu vyake na akakitia sahihi yake.
Hakuna hata mtoto mmoja wa Kleist ambae anakumbuka jina la kitabu hiki.
Kleist alikithamini kitabu hiki na kilipamba shubaka lake la vitabu kwa miaka mingi.
Mwaka wa 1929 Kleist na baadhi ya rafiki zake wa karibu kama Mzee bin Sudi, ambaye wazazi wake walikuwa Wamanyema kutoka Belgian Congo, Ibrahim Hamis - Mnubi ambaye baba yake alitoka Daffur nchini Sudan, Zibe Kidasi, Ali Said Mpima - Mzaramo, Suleiman Majisu, Raikes Kusi, Rawson Watts na Cecil Matola - Myao kutoka Masasi walianzisha African Association, Matola akiwa President na Kleist Secretary.
Historia ya uhuru wa Tanganyika iligeuzwa ikawa historia ya Julius Kambarage Nyerere.
Historia ya TANU ikawa historia ya mtu mmoja.
Hili lilifanikiwa kwa kuwa tulikaa kimya lau kama walikuwapo wazalendo wenyewe walioupigania uhuru kwa hali na mali zao.
Sasa tueleze harakati za uhuru wapi zilianzia.
Tunaweka picha ya Dictionary of African Biography (DAB).
Kinawekwa kipande kifupi kinachomweleza Dr. Kwegyir Aggrey (1875 - 1927) kisha ndani ya Kamusi hilo hilo tunatoa na kumwekea mtazamaji wa clip yetu kipande kifupi cha Kleist Abdallah Sykes (1894 - 1949).
Wazalendo hawa waliotajwa ndani ya Kamusi hilo tunaeleza hawamo katika historia rasmi ya Tanganyika.
Mazungumzo kati ya Waafrika hawa wawili Dar-es-Salaam mwaka wa 1924 ndiyo yalisababisha Kleist kuunda African Association mwaka wa 1929 kisha kuunda Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika (Umoja wa Waislam wa Tanganyika) mwaka wa 1933.
Vyama vyote hivi viwili vilitawaliwa na Waislam.
Watafute wazalendo hawa katika historia ya Tanganyika hutowakuta popote.
Jambo la kusikitisha ni kuwa watu waliamini kuwa ile historia iliyokuwa ikisomeshwa ndiyo historia ya kweli.
Kleist Abdallah Sykes
Dr. Kwegyir Aggrey
Dictionary of African Biography
(DAB)
Picha ya juu ni Kleist Abdallah Sykes, inayofuata ni Dr. Kwegyir Aggrey na chini ni Dictionary of African Biography.
Ninaposomesha historia ya utaifa wa Tanganyika huanza kwa kuwapa wanafunzi wangu rejea katika Dictionary of African Biography (DAB) niwaambia wamsome Dr. Aggrey wakimaliza wamsome Kleist Sykes.
Kipande hiki nimekipa jina: ''Meeting of the Minds.''

MEETING OF THE MINDS