Tufanye nini na hizi clip zinazopotosha Historia ya Tanzania?

Tufanye nini na hizi clip zinazopotosha Historia ya Tanzania?

Huihui,
Muhammad Ali katika kitabu chake, "The Greatest My Own Story," anasema ulifika wakati akiwaonea huruma wapinzani wake na kutamani muamuzi amalize pambano ili mpinzani wake asiendelee kutabika.
Ningekuona wa maana kama ungepigania hoja ya Waafrika walivyopambana na Wakoloni kupata uhuru wao. Lakini kutetea hoja za kidini kwa karne hii ya 21 it's too low.

Nyie ndio wale mara nyingine mnadhania na nyinyi ni waarabu kwa vile tu ni Waislamu. Nawashangaa sana Waafrika wenzangu. Pengine hapo ulipo unalaani kwa nini Mungu alikuumba na ngozi nyeusi ukazaliwa Tanganyika. Yawezekana unatamani ungezaliwa Yemen au Afghanistan.

Be proud you are an African hizi sentiments za kidini unajidhalilisha tu hata kama ungeandika vitabu vikajaa Maktaba ya Taifa pale barabara ya Bibi Titi Mohamed
 
Kalamu yangu haijapata kunidhalilisha.

Kalamu hii imeniingiza Library of Congress nikiwa na umri mdogo sana.

Kalamu hii imenifungulia milango mingi.

Hili si jambo la udini.

Kuandika historia ya Dedan Kimathi, Wakikuyu na Mau Mau si ukabila ni historia iliyokuwapo.

Kuandika historia ya Waislam katika kupigania uhuru wa Tanganyika haijakuwa udini.

Hii ni historia ya jamii ya Kiislam iliyobaguliwa na wakoloni na jinsi walivyopambana kuwatoa Waingereza Tanganyika.
 
Ukabila na udini ni vitu vinachelewesha maendeleo na kuleta vurugu tu.

Watu kama wewe Mzee ni sumu kwa Taifa letu Sijui ulikuwa unataka muishi Waislamu peke yenu?

Somalia ina dini moja tu ya Kiislamu, lakini angalia jinsi ilivyosambaratika kwa miaka zaidi ya 30. Watu wamepoteza maisha, uchumi umerudi nyuma kisa ubaguzi wa kiukoo. Ubaguzi wowote huangamiza Taifa, na ubaguzi huanza taratibu kwa falsafa ya mtu mmoja kisha huenea kwa Taifa zima.
 
Huihui...
Utaleta hoja hiyo hiyo nami nitakupa jibu hili hili.

Msome Bergen (1981), Sivalon (1992) na Njozi (2002).

Angalia post #119.
 
Huihui...
Utaleta hoja hiyo hiyo nami nitakupa jibu hili hili.

Msome Bergen (1981), Sivalon (1992) na Njozi (2002).

Angalia post #119.
Kamwe siwezi kupoteza muda wangu kusoma vitabu vinavyoshabikia ubaguzi. Mimi ni kukemea tu. Wewe ni adui wa taifa, na kwa maneno ya J K Nyerere wewe ni wa kuogopwa kuliko ukoma. Wabaguzi siyo watu
 
Hapana tatizo ikiwa hutosoma kwani, "ignorance is bliss."

Hutosoma na utabakia humjui nani mbaguzi.

Wabaguzi wenyewe walipotambua kuwa Bergen (1981) na Sivalon (1992) wameandika kuhusu ubaguzi haraka sana walivitoa vitabu hivi katika mzunguko visisomwe.

Kitabu cha Njozi (2002) kiliandikwa baada ya Rais Mkapa kusema anataka ushahidi kuwa Waislam wanabaguliwa na serikali.

Kitabu kilipowasili uwanja wa ndege kilizuiliwa kisiingie nchini kisha serikali ikakipiga marufuku.

Wakuogopwa kama ukoma walikuwa wamefichuliwa kwa majina yao na katika nafasi zao katika uongozi wa.nchi.

Njozi alitoa ushahidi wa kile Waislam tukikieleza kila siku.

Lakini Rais Mkapa alitaka ushahidi na ushahidi akapewa.

Nini kilimtia hofu?
 
Gill,
Kitabu kinaeleza, "The Untold Story of the Muslim Struggle Against British Colonialism."

Ni kweli kuwa historia hiyo haikupata kuelezwa?

Jibu ni ndiyo.

Ni kweli kulikuwa na Muslim Struggle?
Jibu ni ndiyo.

Ikiwa hayo si kweli ukweli ni upi?

Umesema kulikuwa na makundi mengi yaliyodai uhuru.

Makundi gani hayo na nani viongozi wa makundi hayo?

Ikiwa unaona historia ya Ukoo wa Sykes si historia ya uhuru wa Tanganyika mimi sina tatizo na mawazo yako.

Ninachojua mimi ni kuwa African Association iliundwa na Kleist Sykes na watu wengine na chama hicho kilienea kwingi Tanganyika.

Ninachojua ni kuwa watoto wa Kleist wote watatu Abdulwahid, Ally na Abbas ni waasisi wa TANU na TANU imeundwa kutokana na TAA.

Kitabu nilichoandika kina nafasi ya pekee katika vitabu vyote vilivyopata kuandikwa kuhusu Julius Nyerere na historia ya TANU.

Si kweli kuwa kitabu hiki si lolote si chochote.

Nakupa taarifa.

Toka 1989 kipochapwa Uingereza hadi leo kimechapwa mara nne na kimetafsiriwa kwa Kiswahili mwaka wa 2002.

Kitabu kimebadili historia yote ya uhuru iliyokuwapo kabla.

Kitabu kimefanyiwa book review na mabingwa watatu wa African History: John Iliffe, Jonathon Glassman na James Brennan review zote hizi zimechapwa kwa wakati tofauti katika Cambridge Journal of African History.

Kutokana na kitabu hiki nimeshirikishwa katika uandishi wa vitabu kadhaa vya historia.

Halikadhalika nimealikwa kutokana na kitabu hiki kuzungumza kwenye vyuo vikuu Marekani, Ulaya na Afrika.

Mambo mengi haya yanakutosha kukujibu.

Sasa kama mzee wetu ameandika kuhusu Waislam, na wewe Andika kuhusu Wakristo mbona case solved, mwingine aandike kuhusu Wapagaji, wengine Hindu na Buddha. Mambo madogo sana
 
Huihui,
Hapana tatizo ikiwa hutosoma kwani, "ignorance is bliss."

Hutosoma na utabakia humjui nani mbaguzi.

Wabaguzi wenyewe walipotambua kuwa Bergen (1981) na Sivalon (1992) wameandika kuhusu ubaguzi haraka sana walivitoa vitabu hivi katika mzunguko visisomwe.

Kitabu cha Njozi (2002) kiliandikwa baada ya Rais Mkapa kusema anataka ushahidi kuwa Waislam wanabaguliwa na serikali.

Kitabu kilipowasili uwanja wa ndege kilizuiliwa kisiingie nchini kisha serikali ikakipiga marufuku.

Wakuogopwa kama ukoma walikuwa wamefichuliwa kwa majina yao na katika nafasi zao katika uongozi wa.nchi.

Njozi alitoa ushahidi wa kile Waislam tukikieleza kila siku.

Lakini Rais Mkapa alitaka ushahidi na ushahidi akapewa.

Nini kilimtia hofu?
Njozi ndiyo nani sasa?
 
Mohamed, mbona awali ulikana maneno hayo? Maneno ambayo yanaweka wazi kuwa kwako wewe Nyerere na wakristu wenzake walikuwa "supporting act" ya ndugu na jamaa zako. Unajua kusema kuwa uliambiwa na Profesa Othman kuwa kitabu chako ndicho kilichomfanya Mwalimu akubali historia yake iandikwe. Mimi binafsi sijawahi kukupinga kwenye suala la kuandika historia ya ndugu zako. Ninachokupinga ni wewe kufanya historia yao ndio historia ya nchi yangu. Naamini kuwa historia ya Tanganyika sio ya waislamu peke yao, bali ni historia ya wale wote ambao bila kujali dini, kabila, rangi, utaifa ( kuna wakenya, waingereza, wamarekani, waghana, waganda,na wanyasaland wengi tu waliochangia historia ya hii nchi) na jinsia zao. Wakina Abdul Wahid hawakushirikiana na wakina Julius kwa sababu walitaka waislamu waongoze nchi hii. Ni wewe ndio unaowavisha hilo joho la udini. Hao wakina mama waliomsindikiza mkatoliki airport (na unajua hawakuwa peke yao) hawakufanya hivyo kwa sababu ya uislamu wao bali kwa utanganyika wao. Hapo airport walikuwepo watu wa dini zote.

Kwenye hili la udini nitakupinga siku zote. Kunijibu au kuninyamazia ni uamuzi wako. Mimi kila ninapoweza nitakujibu.

Amandla...
Kumbe walitaka waifanye kuwa Islamic empire?
 
Huyu mzee Mohamed Said ni mpumbavu sana. Lazima tumdhibiti asilazimishe historia ya wazazi wake iwe historia ya nchi. Nashukuru umeliweka vizuri sana mkuu
 
Njozi ndiyo nani sasa?
Huihui...
TITLECITED BYYEAR
Mwembechai killings and the political future of Tanzania
HM Njozi
602000
Muslims and the State in Tanzania
HM Njozi
192003
The sources of the Qur'an: a critical review of the authorship theories
HM Njozi
71991
Utilitarianism Versus Universalism in Dangarembga's Nervous Conditions
HM Njozi
Nordic Journal of African Studies 14 (1), 14-14
62005
The Mission of the Muslim University of Morogoro in Tanzania: Context, Promises, and Challenges
HM Njozi
Muslim Institutions of Higher Education in Postcolonial Africa, 95-105
42016
Critical artistry in Utenzi wa Shufaka
HM Njozi
Nordic Journal of African Studies 8 (1), 13-13
41999
Utendi wa Mwanakupona and Reception Aesthetics
HM Njozi
Kiswahili 57 (1)
32020
Portrait du héros dans l’Utenzi wa Rasi’lGhuli
HM Njozi, X Garnier
Études littéraires africaines, 15-19
22017
Usishike shauri la mwanamke: Irony in Kiswahili folktales
HM Njozi
Journal of African Cultural Studies 11 (1), 59-71
21998
The social context of Utendi wa Mwanakupona
HM Njozi
Frankfurter Afrikanistische Blätter, 83-90
21993
The Flood Narrative in the Gilgamesh Epic, the Bible and the Qur'ān: The Problem of Kinship and Historicity
HM NJOZI
Islamic studies 29 (3), 303-309
21990
El Origen del Corán
HM Njozi
Riyadh: IIPH
12003
Concepts of the hero in Hikayat Amir Hamzah and in Utenzi Wa Rasi'lghuli
HM Njozi
UKM, Bangi; Institut Alam dan Tamadun Melayu; Takiah Mohd. Iskandar
11996
" Utendi wa Masahibu": A Parable of Truth and Justice
HM Njozi
Research in African Literatures 34 (1), 31-43
2003
Sure-footed slaughter (The Mwembenchai killings and the political future of Tanzania)
HM Njozi
INDEX ON CENSORSHIP 29 (5), 111-111
2000
The uses of ambiguity in Al-Inkishafi
HM Njozi
Afrika und Übersee 81 (2), 227-238
1998
East Africa and the US: Problems and Issues: the Second East African American Studies Colloquium
HM Njozi
Institute of Kiswahili Research, University of Dar es Salaam
1997
Hikayat Amir Hamzah and the Song of Roland: A Comparison
HM Njozi
1995
The popular reception of a Kiswahili poem, Utendi wa Mwanakupona'among the Swahili women
FA Blätter, HM NJOZI
Frankfurter afrikanistische Blätter, 83
1993
Text and Context in Translation: The Phenomenological Approach.
HM Njozi
1991
 
Luku...
Nasikitika kuwa umeamua kuleta matusi badala ya hoja.

Katika miaka ya 1970 Organisation of Islamic Conference (OIC) ilitaka kujenga Chuo Kikuu Tanzania.

Serikali ilikataa kutoa kibali na chuo hicho kikajengwa Mbale, Uganda.

Mwaka wa 1997 Darul Imam kutoka Saudi Arabia ilitaka kujenga Chuo Cha Ufundi Kibaha.

Baada ya kila kitu kukamilika ikazuka vurugu kubwa Darul Iman ikaondoka kwa nia ya kupeleka mradi ule nchi nyingine ya Kiafrika iliyo tayari kupokea msaada ule.

Aboud Jumbe aliingia kati kwa hoja kuwa ikiwa Tanganyika haiwezi kupokea msaada ule basi uletwe Zanzibar.

Hili lilifanikiwa na ndiyo kikajengwa Chuo Kikuu Tunguu badala ya Shule ya Ufundi iliyokusudiwa Kibaha.
mwinyi,kikwete,samia wanazuia hivyo vyuo kujengwa?

halafu wewe mbona unajitoa kuonyesha mchango wako katika ujenzi wa shule na chuo?

kwanini unasubiri hadi ufanyiwe na wageni?

hao matajiri wa kkoo wapo katika kuwapa tende na kufuturisha tu?

kwanin wasijenge hivyo vyuo?
 
Ningependa kwanza uielewe historia ya kuvunjwa kwa EAMWS wakati inajenga Chuo Kikuu na uelewe ni watu gani walihusika.

Baada ya haya kueleweka tunaweza kujadili hayo mengine.
 
Huyu mzee Mohamed Said ni mpumbavu sana. Lazima tumdhibiti asilazimishe historia ya wazazi wake iwe historia ya nchi. Nashukuru umeliweka vizuri sana mkuu
Huihui...
SAID CHAMWENYEWE YEYE NDIYE ALIYELETA WANACHAMA WA KWANZA WA TANU KUTOKA RUFIJI

Abdulwahid na Ally Sykes walikuwa wakimsubiri Nyerere nyumbani kwa Ally Mtaa wa Kipata.

Nyerere alikuwa na habari mbaya.

Serikali ilikuwa imekataa kuisajili TANU.

Nyerere aliwaambia kuwa serikali ilikataa kutoa usajili kwa sababu za kiufundi.

Msajili alitaka kuona ''register'' yenye majina ya wanachama wa TANU.

Nyerere hakuwa na ''register.''

Serikali ilidai kuwa TANU haikuwa na wanachama.

Baada ya kufahamu kuwa serikali imekataa maombi ya TANU kwa kuwa ati haikuwa na wanachama wa kutosha, mithili ya onyesho la mchezo wa kuigiza unaokwenda haraka, Abdulwahid alitumia hekima na mara moja akamuomba Said Chamwenyewe aende nyumbani kwao Rufiji kusajili wanachama kwa ajili ya TANU.

Said Chamwenyewe alitumia baiskeli kwenda Rufiji na njiani kote akipita vijijini akiwaeleza watu kuhusu TANU na azma yake ya kudai uhuru wa Tanganyika.
 
Back
Top Bottom