Huihui,
Umezungumza kuhusu ubaguzi.
Somo zuri na tunaweza kujadili lakini kwanza usome rejea hizi: Bergen (1981), Sivalon (1992) na Njozi (2002).
Bila ya wewe kusoma rejea hizo huwezi kufanya mjadala wa maana.
Nimeandika historia ya uhuru wa Tanganyika kuanzia 1929 sijakutana na Wapagani.
Angalia waasisi wa AA: Cecil Matola, Kleist Sykes, Mzee bin Sudi, Suleiman Majisu, Ali Said Mpima, Zibe Kidasi, Ibrahim Hamisi, Raikes Kusi na Rawson Watts.
Hakuna Mpagani.
1950 wajumbe wa TAA Political Subcommittee: Dr. Vedasto Kyaruzi, Abdul Sykes, Hamza Mwapachu, Mufti Sheikh Hassan bin Ameir, Sheikh Said Chaurembo, John Rupia na Steven Mhando.
Waasisi wa TANU 1954 hao hapo chini:
Hakuna Wapagani.
Waliohudhuria mkutano wa kwanza wa TANU Ukumbi wa Arnautoglo hao hapo chini:
Julius Nyerere, Abdulwahid na Ally Sykes, Dossa Aziz, John Rupia, Mshume Kiyate, Makisi Mbwana, Jumbe Tambaza, Juma Waziri, Clement Mtamila, Rajabu Diwani, Schneider Abdillah Plantan, Marsha Bilali, Rashid Ally Meli, Frederick Njiliwa, Iddi Faiz Mafongo, Iddi Tulio, na Denis Phombeah.
Hakuna Wapagani wala Baniani.
Ikiwa hawakupo wataandika kitabu gani?
Waliokuwapo hao hapo chini na historia yao ndiyo hii tunajadili hapa:
Kuna Wapagani hapo?
Ati historia yangu ni ya uongo.
Kitabu kimechapwa mara nne tunakwenda toleo la tano.
Historia za uongo vitabu vyake vyote vimekufa.
Kitabu changu sasa kina umri wa miaka 25 na bado hadi leo tunakijadili.