Stuxnet
JF-Expert Member
- Feb 12, 2011
- 13,417
- 23,310
Bado hakuna uhusiano wa dini na uhuru wa Tanganyika ni kulazimisha tu kuwa Uislamu ndiyo ulileta uhuru.Stux...
Uislamu umewatisha wengi katika uandishi wa historia ya uhuru wa Tanganyika.
Katika kitabu alichohariri John Iliffe kuna sura kaandika: Daisy Sykes Buruku, ‘The Townsman: Kleist Sykes’, in Iliffe (ed) Modern Tanzanians, Nairobi, 1973, pp. 95-114.
Katika kitabu hiki Kleist Sykes ananukuliwa akisema katika historia ya maisha yake na ndiyo historia ya kuundwa kwa African Asociation 1929 na Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika !933 kuwa waasisi wangi wa AA walikuwa Waislam kwa kuwa Wakristo walikuwa wakionywa na kanisa wasijihusishe na siasa.
Unaniuliza kama Abdul Sykes alisukumwa na Uislam kugombania uhuru wa Tanganyika.
Swali lako lingekuwa hivi: ''Je, baba yake Abdul, Mzee Kleist alisukumwa na Uislam kuasisi AA na kisha Al Jamiatul Islamiyya?''
Wakati wazalendo wa Southern Province Suleiman Masudi Mnonji, Salum Mpunga na Yusuf Chembera wanaunda TANU Lindi wakajikuta wako Waislam watupu kwa sababu Wamishionari kutoka Peramiho walikuwa wanawatisha waumini wao kujiweka mbali na TANU wakidai kuwa TANU ilikuwa inatayarisha vita vingine vya Maji Maji dhidi ya Waingereza.
Hiki ni kisa cha kusisimua nimekieleza kwa kirefu katika kitabu cha Abdul Sykes.
Si mimi niliyelazimisha Uislam uwe mbele katika kupigania uhuru wa Tanganyika.
Kwa nini kiongozi wa juu kabisa wa Waislam Sheikh Hassan bin Ameir alikuwa mstari wa mbele katika kupigania uhuru akiuza kadi za TANU misikitini wakati Kadinali Rugambwa hakuonekana popote katika harakati hizi?
Hizi ni changamoto za ukoloni.
Yapo mengi katika ''Islam as a field of enquiry'' tunayoweza kujadili.
Hapo ndipo nilipochukua ukurasa mmoja na kufanya utafiti kutaka kujua kwa nini ilikuwa hivi?
Hivi ndivyo nilivyojua kwa nini Uislam unawatisha watafiti wengi katika historia ya Tanganyika.
Wewe ukiwa mmoja wa hao.
Ni hoja dhaifu sana ambazo kwa karne hii kuzitetea ni kupoteza muda. J K Nyerere alitengeneza misingi mizuri ya Taifa kwa kuondoa feelings za kikabila na kidini.
Wacha hizi utopia, hazina maana