Fundi...
Hakika historia ya kupigania uhuru wa Tanganyika ni historia ya Waislam na kitabu changu kimesema hivyo: "The Life and Times of Abdulwahid Sykes (1924 - 1968) The Untold Story of the Muslim Struggle Against British Colonialism in Tanganyika."
Mimi sitaabishwi na vipi utatafsiri maneno yangu.
Naweza nikipenda nikakunyamazia kama baadhi ya watu wanavyonishauri.
Hii ni historia ya wazee wangu na nimeiandika kwa msaada wao wengine wameushi na kukiona kitabu na wengine wametangulia mbele ya haki kabla ya kazi kukamilika.
Ninachoshukuru ni kuwa Mwalimu Nyerere kakidiriki kitabu na kakisoma.
Kutokana na kitabu hiki ndipo alipomkubalia Prof. Haroub Othman atengeneze jopo waandike maisha yake.
Mazungumzo ya Mwalimu Nyerere na Prof. Haroub Othman ninayo nimeyahifadhi kama nilivyoyapokea kutoka kwake.
Nilikuwa mmoja wa watu waliochangia kitabu hicho katika kueleza historia ya Mwalimu Nyerere alivyopokelewa na wazee wangu alipofika Dar es Salaam mwaka wa 1952.
Nalishukuru jopo hili kwa kueleza kuwa Maktaba yangu ni katika maktaba tatu bora zilizohifadhi kumbukumbu nyingi za Babu wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Maktaba nyingine ni ya Salim Ahmed Salim na ya Brig.General Hashim Mbita.
Picha hiyo hapo chini TBC 1 wakinihoji kuhusu Nyerere Biography
View attachment 2532175
Kulia ni Bi. Chiku bint Said Kisusa (mke wa Shariff Abdallah Attas), Bi. Titi MOhamed na kushoto ni Bi. Tatu bint Mzee, Julius Nyerere ni huyo hapo wakimuaga safari ya kwanza UNO 1955.