Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mzee wangu heshima yako, ninayo dhamira haswa ya kufanya mahojiano na wewe kwenye online tv. Nipo tayari kupokea maelekezo toka kwako.Von...
Nimeeleza hapa mara nyingi kuwa hili si jambo la dini ila historia ya uhuru wa Tanganyika ilivurugwa kwa makusudi kupoteza mchango wa wazee wangu katika kupigania uhuru.
Nimekaa kitako nimeiandika na sasa ni historia mashuhuri.
Historia hii sikuiandika leo.
Nimeiandika nikiwa kijana sana katika umri wa miaka 30.
Hakika historia yetu imebebwa na udugu.
Nitakuwekea hapa picha kama ushahidi wa udugu huu na nitakuachia wewe kuweka caption ya picha hizo.
Hakika hapakuwa na hoja ya dini kwani lingekuwako suala la dini Sheikh Hassan bin Ameir Mufti wa Tanganyika katika miaka ya 1950 asingemuunga mkono Nyerere kuchukua uongozi wa TAA 1953 kisha uongozi wa TANU 1954.
Kwa kuhitimisha ningependa unieleze imekuwaje na nini kimetokea leo tuko katika hali hii?
Von...
Hapakuwa na sababu ya kunikejeli kuwa ''nazeeka vibaya.''
Wewe kijana lakini katika maandishi yako sikuona fikra pevu ila kejeli dhidi yangu.
Picha hizo hapo juu za historia ya maisha ya Julius Nyerere alivyoishi na wazee wetu.
Nakuachia wewe kutuweka maelezo ya picha hizo.
Ukishindwa sema mimi nitaweka maelezo.
Baadhi ya wazee hao mimi nimewafahamu nakua Dar es Salaam ya 1960s napata akili nawaona na wengine niliwadiriki katika uhai wao na nikazungumzanao wakati naandika historia ya uhuru.
Wote wazee hawa niliozungumzanao waliniombea dua njema nikamilishe historia yao katika kuligania uhuru wa Tanganyika.
Asta...Mzee wangu heshima yako, ninayo dhamira haswa ya kufanya mahojiano na wewe kwenye online tv. Nipo tayari kupokea maelekezo toka kwako.
Babu...We mzee kalale sasa, unajua nyie wavaa kobazi ni majuha kupindukia,
We kila muda unazungumzia vitabu vitabu, Udini udini, Sykes blaah blaah sijui nilikua Wapi na wapi wakati huko watu wapo kila siku.
Embu usilete upumbavu.
Mwl Julius Nyerere ni baba wa taifa hili.
Sasa hata heshima yako hapa inateketea kwa ajili ya mambo yako ya ajabu ajabu na Udini.
Na Chuki zako kwa dini zingine.
Im Pagan anyway
Massa,Mzee sheikh Mohammed unazani kuna umuhimu wa familia za wapigania uhuru wa Tanzania ambao wengi ni waislam kupewa tuzo? Au wapewe zawadi yoyote kwa kuthamini mchango wao ni kuombwa samahani baada ya Nyerere kutowathamini? Au nini kifanyike maana kizazi cha sasa ndo kabisa hawajui hayo mambo na wanaenda kufutika kweli hao wadai wa uhuru OG
Dudu...
Historia ya uhuru wa Tanganyika na historia ya Nyerere katika harakati hizo ni changamoto kubwa kwa wasomi na wanahistoria wetu.
Siwalaumu.
Inahitaji mtu shujaa kweli kweli kueleza historia hii kwa ukweli wake unaostahili.
Unaelezaje mchango wa Waislam maarufu waliounda African Association 1929 lakini wamefutwa katika historia ya TANU?
Unaelezaje kupigwa marufuku na serikali EAMWS na kuundwa BAKWATA wakati ilikuwa inajenga Chuo Kikuu mwaka wa 1968?
Unajibu nini utakapoulizwa nini ilikuwa nafasi ya Julius Nyerere katika matatizo yote haya?
Nimeandika kitabu na yote haya nimeyaeleza kama yalivyostahili kuelezwa.
Kitabu hiki naamini unakijua au umepata kukisikia kimebadili si historia ya uhuru wa Tanganyika na TANU bali hata historia ya Julius Nyerere.
Kitabu kinakwenda toleo la tano toka kuchapwa mara ya kwanza 1989.
Haya si mambo ya maskhara, kejeli na kufanya utani.
Mzee mohd una busara sana ila hapo kwenye hiyo mantiki unakera.Babu...
Tatizo ni historia ya uhuru ilifutwa na mimi nikaandika kitabu kuisahihisha.
Historia Sykes haijawa blah, blah.
Mimi baada ya kuieleza sasa iko katika Dictionary of African Biography (DAB).
Kufanya hivi si chuki.
Chuki unayo wewe ambaenl umenitukana.
Massa,
Hayo si yangu mimi kuamua.
Nililofanya mimi nimesahihisha historia iliyokuwa na makosa na kuandika historia ya kweli.
Sidhani kama hili ni tatizo.
Babu...Mzee mohd una busara sana ila hapo kwenye hiyo mantiki unakera.
Jaribu kutupa ilimu vijana wako bila kuingiza mambo ingine.
Tunalo la kujifunza toka kwako,
Lakini mtu akikusoma unazungumzia usilamu sijui nini na nini tunashangaa.
Kuna history nzuri tu huwa unaandika mbona mtu anasoma bila mawaa.
Wengine hatuna dini.
Sorry kwa kauli ingine huko juu
Jiwe...Wewe ni mgonjwa wa akili,inferiority complex ndio inakusumbua,hii nchi wengi tu wametoa mchango wa uhuru,akiongoza mapambano JKNyerere,itabaki hivyo milele na milele. Poleni kwa sababu matarajio yenu yalifeli,Nyerere aliweka misingi imara sana ya umoja na amani katika nchi hii kwa kila jamii iliyopo hapa tz,hichi ndicho kinachowauma sana ulitamani hii nchi ivae hijabu na bharagashia.
Umepuuzwa na utaendelea kupuuzwa hata ujitutume vipi mzee ushafeli,hiyo historia utasoma wewe na wajukuu zako tu ila historia ya Tanganyika ilishaandikwa.
Hamna shida mzee wangu mwaga nondo hapahapa.Babu...
Kwanza si kweli kuwa huna dini.
Pili katika historia ya kupigania uhuru wa Tanganyika ukithubutu kutakaku kukwepa Uislam tayari ushaipoteza historia yenyewe.
Hili swali ni zuriMzee sheikh Mohammed unazani kuna umuhimu wa familia za wapigania uhuru wa Tanzania ambao wengi ni waislam kupewa tuzo? Au wapewe zawadi yoyote kwa kuthamini mchango wao ni kuombwa samahani baada ya Nyerere kutowathamini? Au nini kifanyike maana kizazi cha sasa ndo kabisa hawajui hayo mambo na wanaenda kufutika kweli hao wadai wa uhuru OG
Babu...Hamna shida mzee wangu mwaga nondo hapahapa.
Sykes hawa wa mwisho si tushakaa nao sana socialy sijawai kuwaskia kuongelea dini wala kugusia mambo ya siasa.
Ni watu ambao hawana mambo hayo.
Mtaongea, kucheka na kutaniana hawajawai hata kutaja jina la baba yao
Wala politic, wala Nyerere, wala kitu chochote cha baba zao.
Ina maana hawajui?
No ni kwamba hawataki mambo mengi.
Vitabu vyako ni vizuri kusoma kujifunza
Ila ukiingiza Udini mtu anakosa interest hata kununua.
Hapo uwe Neutral.
Mtu akikutana na mawaidha yako huko kitabuni kashanunua atasoma au apite hizo kurasa.
Lakini haya mambo hapa sio mahali pake
Utakosa washabiki.
Ingawa kiukweli maandishi yako yanafundisha mengi tu.
Licking...Hili swali ni zuri
Massa,Sheikh Mohammed unazani vitabu vyako licha ya kutafasiliwa mara nne je vimesomwa na watu wengi? Hasa kwa watanganyika sisi. Na kama ni hapana unampango gani kuvifanya viwafikie watu wengi ili kuweza kujua history ya kweli ya uhuru wa tanganyika?
Massa,
Mimi ni mwandishi.
Shughuli ya kusambaza kitabu ni ya publisher na wauzaji vitabu.
Kitabu ni mali ya publisher yeye ndiye aliyewekeza fedha zake kukichapa na ndiye mwenye fungu kubwa katika mauzo.
Kitabu kinafanya vyema kinakwenda toleo la tano.
Massa,Kitabu kina kwenda vema kimauzo jambo zuri sana sheikh. Ila walengwa hasa wa kitabu ni wazungu au watanganyika? Ambao ndo inabidi tujue ukweli hasa wa jinsi uhuru ulivyopatikana. Kitabu kinapatina wapi na kwa bei gani. Usione vibaya kuwasaidia publisher kupush mauzo maana lazima unapata percentage kwa kila Kitabu kinachouzwa
Siyo lazima utaje uislamu katika historia hiyo ni FALSE HYPOTHESIS!! Wataje tu akina Abdulwahid Sykes kama Watanganyiaka walioasisi mapambano ya uhuru, inatosha. Usiulazimishe UISLAMU. Hapo ndipo mzee Mohamed Said unaharibu.Babu...
Kwanza si kweli kuwa huna dini.
Pili katika historia ya kupigania uhuru wa Tanganyika ukithubutu kutaka kukwepa Uislam tayari ushaipoteza historia yenyewe.
Stux...Siyo lazima utaje uislamu katika historia hiyo ni FALSE HYPOTHESIS!! Wataje tu akina Abdulwahid Sykes kama Watanganyiaka walioasisi mapambano ya uhuru, inatosha. Usiulazimishe UISLAMU. Hapo ndipo mzee Mohamed Said unaharibu.
Na kama huo ndiyo msingi wa vitabu vyako basi tambua umeandika trash kwa kuwa umewagawa Watanzania.
Jubu swali hili. Je Abdulwahid Sykes alisukumwa na Uislamu kugombania uhuru? Au alisukumwa na exposure aliyoiona baada ya kuwa askari wa jeshi la mkoloni kwenye World War 1 & 2?