Tufanye nini na hizi clip zinazopotosha Historia ya Tanzania?

Tufanye nini na hizi clip zinazopotosha Historia ya Tanzania?

Sawa. Imani kubwa hapa nchini ni Uislamu. Waislamu ndio waliongoza mapambano yote ya kudai uhuru. Ukoo wa Sykes ulikuwa na nafasi ya kipekee katika mapambano hayo. Kinachosikitisha ni kuwa Nyerere aliwasahau kabisa baada ya uhuru na maisha yao kama ilivyokuwa kwa waislamu wengi yalikuwa duni.

Kabla ya uhuru waislamu walikuwa na shule na hospitali nyingi ambazo Nyerere alizitaifisha ili kuwapa nafasi wakristu wenzake wafikie kiwango cha elimu na ustaarabu wa waislamu. Hakuishia hapo, alihakikisha kuwa maksi zote za vijana wa kiislamu katika mitihani zilikuwa zinabadilishwa na kupewa wakristu. Nyerere huyo huyo alitaifisha mali za waislamu na kuwapa wakristu.

Hali hiyo iliendelezwa na Mkapa ambae aliondoa mazuri yote yaliyofanywa na Mwinyi. Mkapa alifikia hatua ya kuchukua chuo kikuu cha taasisi ya serikali na kukikabidhi kwa wakristu wenzake. Hali ilikuwa nzuri kidogo wakati wa Jakaya lakini John alipoingia aliharibu tena. Sasa hivi kidogo inaenda vizuri baada ya Mheshimiwa Samia kuwa Rais. Hawa wakristu hasa wakatoliki sio watu wa kuwafanyia masihara kabisa.

Amandla...
... Mzee, fasihi ulisomea wapi wewe?
 
Hapo kwanza ncheke. Mzee unalalamika kukosewa adabu kuitwa Mudi kifupi cha Mohammed huku wewe ukiwa ni bingwa wa kufupisha majina ya watu humu.

Mfano tu hapo Lukubuzo unayemlalamikia umemwita Luku.. ni ni unatakataa na nini unafanya?
Tai...
Nimefupisha Luku.

Yeye kama anataka kufupisha inatakiwa aandike "Moh" si Mudi.

Umefanya haraka kucheka.
Umefanya haraka sana kunijibu.

Kabla hujaandika unatakiwa kusoma kwa utulivu uelewe ndipo unajibu.

Kama ni swali la mtihani umekosea.
Ushapoteza alama.

Kama usaili wa kazi...
 
Kuna clip inazunguka mitandaoni ikieleza mengi kuhusu Tanganyika.
Kubwa linaloshtua watu wengi ni kusema imani kuu nchini ni Ukristo.
Nimeandika makala hiyo hapo chini kutanabaisha kuhusu historia ya Tanganyika nikijaribu kueleza imekuwaje tumefikia hali hii:

MEETING OF THE MINDS​

Alikuwa Dr James Kwegyir Aggrey, Mwafrika kutoka Ghana ndiye mtu aliyemtia Kleist hamu ya kuingia katika siasa. Dr Aggrey alikuja Tanganyika mwaka 1924.

Dr Aggrey alikuwa katika Phelps-Stokes Commissions iliyokuwa imeundwa kuchunguza elimu ya Waafrika.

Ilikuwa katika kipindi hiki akiwa ndani ya kamisheni hii ndipo alipokuja Tanganyika. Dr Aggrey alikataliwa kupanga New Africa Hotel kwa kuwa alikuwa mtu mweusi.

Ikabidi Gavana Donald Cameron amtafutie chumba Government House ajisitiri kwa malazi.

Wakati huu alipokuwa Dar es Salaam ndipo Dr Agrrey alipokutana na Kleist.
Dr Aggrey alimtunukia Kleist moja ya vitabu vyake na akakitia sahihi yake.

Hakuna hata mtoto mmoja wa Kleist ambae anakumbuka jina la kitabu hiki.

Kleist alikithamini kitabu hiki na kilipamba shubaka lake la vitabu kwa miaka mingi.

Mwaka wa 1929 Kleist na baadhi ya rafiki zake wa karibu kama Mzee bin Sudi, ambaye wazazi wake walikuwa Wamanyema kutoka Belgian Congo, Ibrahim Hamis - Mnubi ambaye baba yake alitoka Daffur nchini Sudan, Zibe Kidasi, Ali Said Mpima - Mzaramo, Suleiman Majisu, Raikes Kusi, Rawson Watts na Cecil Matola - Myao kutoka Masasi walianzisha African Association, Matola akiwa President na Kleist Secretary.

Historia ya uhuru wa Tanganyika iligeuzwa ikawa historia ya Julius Kambarage Nyerere.

Historia ya TANU ikawa historia ya mtu mmoja.

Hili lilifanikiwa kwa kuwa tulikaa kimya lau kama walikuwapo wazalendo wenyewe walioupigania uhuru kwa hali na mali zao.

Sasa tueleze harakati za uhuru wapi zilianzia.
Tunaweka picha ya Dictionary of African Biography (DAB).

Kinawekwa kipande kifupi kinachomweleza Dr. Kwegyir Aggrey (1875 - 1927) kisha ndani ya Kamusi hilo hilo tunatoa na kumwekea mtazamaji wa clip yetu kipande kifupi cha Kleist Abdallah Sykes (1894 - 1949).

Wazalendo hawa waliotajwa ndani ya Kamusi hilo tunaeleza hawamo katika historia rasmi ya Tanganyika.

Mazungumzo kati ya Waafrika hawa wawili Dar-es-Salaam mwaka wa 1924 ndiyo yalisababisha Kleist kuunda African Association mwaka wa 1929 kisha kuunda Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika (Umoja wa Waislam wa Tanganyika) mwaka wa 1933.

Vyama vyote hivi viwili vilitawaliwa na Waislam.

Watafute wazalendo hawa katika historia ya Tanganyika hutowakuta popote.
Jambo la kusikitisha ni kuwa watu waliamini kuwa ile historia iliyokuwa ikisomeshwa ndiyo historia ya kweli.

332955155_3398442657098751_5156298518240527622_n.jpg

Kleist Abdallah Sykes
333027833_3114434315528253_5075425198623726105_n.jpg

Dr. Kwegyir Aggrey

332914989_1164916214133995_6225086038975879163_n.jpg

Dictionary of African Biography
(DAB)​

Picha ya juu ni Kleist Abdallah Sykes, inayofuata ni Dr. Kwegyir Aggrey na chini ni Dictionary of African Biography.

Ninaposomesha historia ya utaifa wa Tanganyika huanza kwa kuwapa wanafunzi wangu rejea katika Dictionary of African Biography (DAB) niwaambia wamsome Dr. Aggrey wakimaliza wamsome Kleist Sykes.

Kipande hiki nimekipa jina: ''Meeting of the Minds.''
WEKA HIYO CLIP HAPA. ILI ISIONEKANE MANENO MANENO YA KILA SIKU. WEKA CLIP HAPA IJADILIWE.
 
... Mzee, fasihi ulisomea wapi wewe?
Dudus,
Sidhani kama ni fasihi peke yake.
Nimepita na madrasa.

Madrasa wanafunza mengi sana kwa mtindo tofauti na shule.

Huwezekana sababu ni hiyo.
Kwa nini umeniuliza?
 
So issue hapa ni kuwa Kuna Dini nyingine haijatajwa? Hivi ikitokea mimi nimeandaa Documentary nikasema team kubwa Yanga. Nyie wa Simba mnakuwa mmeondoshwa au mnaanza kukosa kitu gani katika maisha? Maana malalamiko mengine tusionekane tu tuna asili ya kulalamika. Hii Wakristo wakijitaja inawakosesha nini Waislamu? Hawataenda Mbinguni? Dini yao itafutika?
 
Mtu ukiwa na roho ya ulalamishi mwishowe unadharaulika tu maana unalalamika hata visivyo na maana. Hiyo documentary imetaja watu maarufu ambao wengine hata siwafahamu. But siwezi anzisha uzi kulalamika. SIYO DOCUMENTARY YA SERIKALI. SIYO RASMI. BUT SIONI CHA KULALAMIKA KILA WAKATI. MALALAMIKO YAMEKUWA MENGI SANA MPAKA SASA MTU UNADHARAULIKA.
 
Yaani Babu yangu mzee Mohammed kwa udini wewe huwezekani na bahati mbaya umeshazeeka hata kushaurika ni ngumu.

Mungu akusaidie utambue thamani ya watu kupitia utu wao na sio dini maana hakuna namna unaweza shauriwa kwa umri wako huo.
Dp...
Kwa umri wangu wa miaka 71 wewe ni mwanangu.

Kikwetu mimi nikikuchukua kama mjukuu nitakuwa nimekupandisha daraja ya kuweza hata kunikalia kichwani.

Kwa ajili hii basi una haki ya hata kunifanya mimi babu yako kichekesho.

Huu utangulizi nia yake ni kukuweka mahali pako kama mwana ili uwe na adabu kwangu.

Ikipatikana adabu tutafanya mjadala wenye tija.

Udini kuandika "corrective political history ya Tanganyika?"

Au kwako hii ni dini?

Swali la umri halina uhusiano na historia ya uandishi wangu kwani nimeanza kuandika nikiwa kijana na walitokea watu kupingana na mimi.

Naamini tumeelewana.
Angalia picha hiyo katika makala yangu katika New African (London):

1677561101820.jpeg

Na hujakosoa kuwa lugha kuu Kiarabu kimo. Badala ya Kiswahili na Kiingereza. Maana ndiyo Lugha zenye wazungumzaji wengi. Hilo hukuona kuwa ni kosa. Ile video nadhani wametengeneza makusudi kupima uelewa wa watu 😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂
 
Mtu ukiwa na roho ya ulalamishi mwishowe unadharaulika tu maana unalalamika hata visivyo na maana. Hiyo documentary imetaja watu maarufu ambao wengine hata siwafahamu. But siwezi anzisha uzi kulalamika. SIYO DOCUMENTARY YA SERIKALI. SIYO RASMI. BUT SIONI CHA KULALAMIKA KILA WAKATI. MALALAMIKO YAMEKUWA MENGI SANA MPAKA SASA MTU UNADHARAULIKA.
Mtu...
Inawezekana huoni mambo nionavyo.
Kweli wewe huoni tatizo katika hiyo clip.

Mimi na wengine wengi tumeona tatizo katika clip hiyo.

Watu wamepishana katika ufahamu.
Mimi sijalalamika.

Rejea niliyoandika.
 
Na hujakosoa kuwa lugha kuu Kiarabu kimo. Badala ya Kiswahili na Kiingereza. Maana ndiyo Lugha zenye wazungumzaji wengi. Hilo hukuona kuwa ni kosa. Ile video nadhani wametengeneza makusudi kupima uelewa wa watu 😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂
Mtu...
Kawaida yangu ni huwa siandiki kila kitu.

Hupenda kuandika kile ninachokiona muhimu.

Unisamehe kwa hili.
 
Siku zote history huandikwa na wanaotawala hakuna historia sahihi asilimia 100%
Sidhani Kila mtu aliyepigania uhuru amendikwa kwenye kitabu cha historia na cha msingi watanganyika kwa umoja wao ndio waliodai Uhuru haijalishi sana dini.
Sasa kwa Nini unataka kubinafisisha hii history iwe ya waislam peke Yao?
 
Sawa. Imani kubwa hapa nchini ni Uislamu. Waislamu ndio waliongoza mapambano yote ya kudai uhuru. Ukoo wa Sykes ulikuwa na nafasi ya kipekee katika mapambano hayo. Kinachosikitisha ni kuwa Nyerere aliwasahau kabisa baada ya uhuru na maisha yao kama ilivyokuwa kwa waislamu wengi yalikuwa duni.

Kabla ya uhuru waislamu walikuwa na shule na hospitali nyingi ambazo Nyerere alizitaifisha ili kuwapa nafasi wakristu wenzake wafikie kiwango cha elimu na ustaarabu wa waislamu. Hakuishia hapo, alihakikisha kuwa maksi zote za vijana wa kiislamu katika mitihani zilikuwa zinabadilishwa na kupewa wakristu. Nyerere huyo huyo alitaifisha mali za waislamu na kuwapa wakristu.

Hali hiyo iliendelezwa na Mkapa ambae aliondoa mazuri yote yaliyofanywa na Mwinyi. Mkapa alifikia hatua ya kuchukua chuo kikuu cha taasisi ya serikali na kukikabidhi kwa wakristu wenzake. Hali ilikuwa nzuri kidogo wakati wa Jakaya lakini John alipoingia aliharibu tena. Sasa hivi kidogo inaenda vizuri baada ya Mheshimiwa Samia kuwa Rais. Hawa wakristu hasa wakatoliki sio watu wa kuwafanyia masihara kabisa.

Amandla...
We niwa kupuuzwa. Waislam walikuwa taasisi ipi iliyotaifishwa na serikali? Taasis zilitaifishwa ni za kanisa. Mkapa aliwapa waislamu chuo cha TANESCO Morogoro bure kabisa ndio chuo kikuu pekee cha waislamu. Waislamu hawana uwezo hata wa kujenga chuo chao. Niambie zaidi ya kile chuo kikuu chenu qameongeza nini. Hata kufungua tawi Dsm wameshindwa. Ni watu wavivu, walalamishi, wa kupenda kupendelewa.
 
Mtu...
Kawaida yangu ni huwa siandiki kila kitu.

Hupenda kuandika kile ninachokiona muhimu.

Unisamehe kwa hili.
Mudi, nilikupa tu mfano wa makosa makubwa mengi katika hiyo makala. But mi sijaona la kuhangaika nalo. Mi kuna mambo nasema hayana haja ya kuumiza kichwa na kulalamika lalamika kila wakati.
 
Siku zote history huandikwa na wanaotawala hakuna historia sahihi asilimia 100%
Sidhani Kila mtu aliyepigania uhuru amendikwa kwenye kitabu cha historia na cha msingi watanganyika kwa umoja wao ndio waliodai Uhuru haijalishi sana dini.
Sasa kwa Nini unataka kubinafisisha hii history iwe ya waislam peke Yao?
Gambo...
Una hakika kuwa ''siku zote'' historia inaandikwa na wanaotawala?

Zipo historia na ni nyingi ambazo zimeandikwa na watu huru.

Huwezi kuandika ''kila mtu'' lakini wapo ambao wakiachwa watu watauliza.

Unaweza kuandika historia ya TANU bila kumtaja Sheikh Hassan bin Ameir?

Sijabinafsisha historia ya TANU kuwa ya Waislam peke yao.
Waislam walifutwa katika historia ya uhuru.

Mimi nimewarejesha.

Nimewarejesha si Waislam tu bali na wengine ambao na wao pia walifutwa.

Mfano wa Denis Phomgeah, Dome Okochi Budohi, Clement Mtamila, Dr. Michael Lugazia, Dr, Vedasto Kyaruzi, Dr. Luciano Tsere kwa kuwataja wachache.

Haya ndiyo yaliyofanya kitabu hiki kivutie wasomaji wengi.

1677561945188.jpeg

Dr. Luciano Tsere
1677562192807.jpeg

1677562245565.jpeg

Denis Phombeah

Eti!? Huyu Kleist asili yake ni wapi!?
 
Back
Top Bottom