Tufanye nini na hizi clip zinazopotosha Historia ya Tanzania?

Tufanye nini na hizi clip zinazopotosha Historia ya Tanzania?

Fundi...
Hakika historia ya kupigania uhuru wa Tanganyika ni historia ya Waislam na kitabu changu kimesema hivyo: "The Life and Times of Abdulwahid Sykes (1924 - 1968) The Untold Story of the Muslim Struggle Against British Colonialism in Tanganyika."

Mimi sitaabishwi na vipi utatafsiri maneno yangu.

Naweza nikipenda nikakunyamazia kama baadhi ya watu wanavyonishauri.

Hii ni historia ya wazee wangu na nimeiandika kwa msaada wao wengine wameushi na kukiona kitabu na wengine wametangulia mbele ya haki kabla ya kazi kukamilika.

Ninachoshukuru ni kuwa Mwalimu Nyerere kakidiriki kitabu na kakisoma.

Kutokana na kitabu hiki ndipo alipomkubalia Prof. Haroub Othman atengeneze jopo waandike maisha yake.

Mazungumzo ya Mwalimu Nyerere na Prof. Haroub Othman ninayo nimeyahifadhi kama nilivyoyapokea kutoka kwake.

Nilikuwa mmoja wa watu waliochangia kitabu hicho katika kueleza historia ya Mwalimu Nyerere alivyopokelewa na wazee wangu alipofika Dar es Salaam mwaka wa 1952.

Nalishukuru jopo hili kwa kueleza kuwa Maktaba yangu ni katika maktaba tatu bora zilizohifadhi kumbukumbu nyingi za Babu wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Maktaba nyingine ni ya Salim Ahmed Salim na ya Brig.General Hashim Mbita.
Picha hiyo hapo chini TBC 1 wakinihoji kuhusu Nyerere Biography

View attachment 2532175
Kulia ni Bi. Chiku bint Said Kisusa (mke wa Shariff Abdallah Attas), Bi. Titi MOhamed na kushoto ni Bi. Tatu bint Mzee, Julius Nyerere ni huyo hapo wakimuaga safari ya kwanza UNO 1955.
Kwenye hio picha huonekani kama mdini kabisa ,kweli usijaji kitabu kwa kuangalia kava
 
Nimeogopa sana kusikia imani kubwa Tanzania ni uislamu, Afrika inaangamia kwenye huu uzombi.
 
Kwenye hio picha huonekani kama mdini kabisa ,kweli usijaji kitabu kwa kuangalia kava
Ujoka,
Historia ya TANU imeandikwa na imekuwako miaka yote ikiwa na makosa kwa kuwaacha nje wazalendo wengi sana.

Huu si udini.

Udini ni pale mimi nilipokuja kuandika kitabu cha Abdul Sykes na kusahihisha makosa yaliyokuwapo kwenye hustoria hiyo.
 
Mimi sizungumzii kitabu chako ambacho kwa kweli sina mpango wa kukisoma.

Nazungumzia ulichoandika humu leo katika kurasa za JF.

Amandla....
Fundi...
Kitabu cha maisha ya Abdul Sykes kilishtua mabingwa wa African History katika vyuo vikuu Marekani na Ulaya: John Iliffe, Jonathon Glassman na James Brennan.

Wote hawa walifanya book review na reviews zao zilichapwa Cambridge Journal of African History.

Hapa Afrika ya Mashariki The East African walifanya serialisation ya kitabu matoleo matatu.

Nikaalikwa kuzungumza University of Iowa na Northwestern University, Marekani.

Nikaalikwa pia Zentrum Moderner Orient, Berlin.

Tanzania baada ya kukitafsiri kitabu kwa Kiswahili kitabu kikachapwa mara mbili.

Wasomaji wamekipenda.

Kama wewe hutaki kusoma kitabu chenye sifa hizi basi kinachokuzuia ni husda.
 
Yaani Babu yangu mzee Mohammed kwa udini wewe huwezekani na bahati mbaya umeshazeeka hata kushaurika ni ngumu.

Mungu akusaidie utambue thamani ya watu kupitia utu wao na sio dini maana hakuna namna unaweza shauriwa kwa umri wako huo.
 
Kwahiyo Makafr Wameleta Clip Yao Ambayo Imetunyima Usingizi
Wagalatia Acheni Wenzenu Wapumue Vizuri Msiwabane Hawana Raha
 
Yaani Babu yangu mzee Mohammed kwa udini wewe huwezekani na bahati mbaya umeshazeeka hata kushaurika ni ngumu.

Mungu akusaidie utambu thamani ya watu kupitia utu wao na sio dini maana hakuna namna unaweza shauriwa kwa umri wako huo.

Utampa Mzee Pressure Bure Kumbuka Analoliamini Ndiyo Linalompa Tabu
 
Mohamed Said Said anaonekana anajua mengi sana kuhusu Historia ya Tanzania especially ya Dar na Pwani yote, tatizo lazima aingize dini yake ya uislam na kuibadilisha story nzima kuonekana ya udini
 
Kuna clip inazunguka mitandaoni ikieleza mengi kuhusu Tanganyika.
Kubwa linaloshtua watu wengi ni kusema imani kuu nchini ni Ukristo.
Nimeandika makala hiyo hapo chini kutanabaisha kuhusu historia ya Tanganyika nikijaribu kueleza imekuwaje tumefikia hali hii:

MEETING OF THE MINDS​

Alikuwa Dr James Kwegyir Aggrey, Mwafrika kutoka Ghana ndiye mtu aliyemtia Kleist hamu ya kuingia katika siasa. Dr Aggrey alikuja Tanganyika mwaka 1924.

Dr Aggrey alikuwa katika Phelps-Stokes Commissions iliyokuwa imeundwa kuchunguza elimu ya Waafrika.

Ilikuwa katika kipindi hiki akiwa ndani ya kamisheni hii ndipo alipokuja Tanganyika. Dr Aggrey alikataliwa kupanga New Africa Hotel kwa kuwa alikuwa mtu mweusi.

Ikabidi Gavana Donald Cameron amtafutie chumba Government House ajisitiri kwa malazi.

Wakati huu alipokuwa Dar es Salaam ndipo Dr Agrrey alipokutana na Kleist.
Dr Aggrey alimtunukia Kleist moja ya vitabu vyake na akakitia sahihi yake.

Hakuna hata mtoto mmoja wa Kleist ambae anakumbuka jina la kitabu hiki.

Kleist alikithamini kitabu hiki na kilipamba shubaka lake la vitabu kwa miaka mingi.

Mwaka wa 1929 Kleist na baadhi ya rafiki zake wa karibu kama Mzee bin Sudi, ambaye wazazi wake walikuwa Wamanyema kutoka Belgian Congo, Ibrahim Hamis - Mnubi ambaye baba yake alitoka Daffur nchini Sudan, Zibe Kidasi, Ali Said Mpima - Mzaramo, Suleiman Majisu, Raikes Kusi, Rawson Watts na Cecil Matola - Myao kutoka Masasi walianzisha African Association, Matola akiwa President na Kleist Secretary.

Historia ya uhuru wa Tanganyika iligeuzwa ikawa historia ya Julius Kambarage Nyerere.

Historia ya TANU ikawa historia ya mtu mmoja.

Hili lilifanikiwa kwa kuwa tulikaa kimya lau kama walikuwapo wazalendo wenyewe walioupigania uhuru kwa hali na mali zao.

Sasa tueleze harakati za uhuru wapi zilianzia.
Tunaweka picha ya Dictionary of African Biography (DAB).

Kinawekwa kipande kifupi kinachomweleza Dr. Kwegyir Aggrey (1875 - 1927) kisha ndani ya Kamusi hilo hilo tunatoa na kumwekea mtazamaji wa clip yetu kipande kifupi cha Kleist Abdallah Sykes (1894 - 1949).

Wazalendo hawa waliotajwa ndani ya Kamusi hilo tunaeleza hawamo katika historia rasmi ya Tanganyika.

Mazungumzo kati ya Waafrika hawa wawili Dar-es-Salaam mwaka wa 1924 ndiyo yalisababisha Kleist kuunda African Association mwaka wa 1929 kisha kuunda Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika (Umoja wa Waislam wa Tanganyika) mwaka wa 1933.

Vyama vyote hivi viwili vilitawaliwa na Waislam.

Watafute wazalendo hawa katika historia ya Tanganyika hutowakuta popote.
Jambo la kusikitisha ni kuwa watu waliamini kuwa ile historia iliyokuwa ikisomeshwa ndiyo historia ya kweli.

332955155_3398442657098751_5156298518240527622_n.jpg

Kleist Abdallah Sykes
333027833_3114434315528253_5075425198623726105_n.jpg

Dr. Kwegyir Aggrey

332914989_1164916214133995_6225086038975879163_n.jpg

Dictionary of African Biography
(DAB)​

Picha ya juu ni Kleist Abdallah Sykes, inayofuata ni Dr. Kwegyir Aggrey na chini ni Dictionary of African Biography.

Ninaposomesha historia ya utaifa wa Tanganyika huanza kwa kuwapa wanafunzi wangu rejea katika Dictionary of African Biography (DAB) niwaambia wamsome Dr. Aggrey wakimaliza wamsome Kleist Sykes.

Kipande hiki nimekipa jina: ''Meeting of the Minds.''
Udini
Udini
Udini
 
Fundi...
Hapana siwezi kusema hivyo.

Kitabu cha Abdul Sykes nimejitahidi kueleza mengi.

Muhimu hapa ni ikiwa wewe unaona wapo ambao mimi sikuwataja ukachukua fursa hii kuwataja wakajulikana.
Abdul Sykes alikuwa na maandiko yeyote ambayo unaweza kutuwekea hapa jukwaani ili labda tujue fikra zake bila kupitia kwa kalamu na ubongo wa mtu baki?
Maana autobiographers mara nyingine huwa hawaakisi kilicho mawazoni mwa mtu.
 
Kwa nini unadhani hao wazee unaowatetea, wao wenyewe kwa utashi wao wakaona Kambarage ndiye wa kumkabidhi mikoba ya kwenda kushawishi wazungu waipe uhuru Tanganyika?

Kwa nini haikuwa mmoja ya wazee hao ambao umekuwa ukiwataja kwa majina, kwamba wangeteuana mmoja wao na kwenda mbele ya mabaraza ya wazungu?
 
Kuna clip inazunguka mitandaoni ikieleza mengi kuhusu Tanganyika.
Kubwa linaloshtua watu wengi ni kusema imani kuu nchini ni Ukristo.
Nimeandika makala hiyo hapo chini kutanabaisha kuhusu historia ya Tanganyika nikijaribu kueleza imekuwaje tumefikia hali hii:

MEETING OF THE MINDS​

Alikuwa Dr James Kwegyir Aggrey, Mwafrika kutoka Ghana ndiye mtu aliyemtia Kleist hamu ya kuingia katika siasa. Dr Aggrey alikuja Tanganyika mwaka 1924.

Dr Aggrey alikuwa katika Phelps-Stokes Commissions iliyokuwa imeundwa kuchunguza elimu ya Waafrika.

Ilikuwa katika kipindi hiki akiwa ndani ya kamisheni hii ndipo alipokuja Tanganyika. Dr Aggrey alikataliwa kupanga New Africa Hotel kwa kuwa alikuwa mtu mweusi.

Ikabidi Gavana Donald Cameron amtafutie chumba Government House ajisitiri kwa malazi.

Wakati huu alipokuwa Dar es Salaam ndipo Dr Agrrey alipokutana na Kleist.
Dr Aggrey alimtunukia Kleist moja ya vitabu vyake na akakitia sahihi yake.

Hakuna hata mtoto mmoja wa Kleist ambae anakumbuka jina la kitabu hiki.

Kleist alikithamini kitabu hiki na kilipamba shubaka lake la vitabu kwa miaka mingi.

Mwaka wa 1929 Kleist na baadhi ya rafiki zake wa karibu kama Mzee bin Sudi, ambaye wazazi wake walikuwa Wamanyema kutoka Belgian Congo, Ibrahim Hamis - Mnubi ambaye baba yake alitoka Daffur nchini Sudan, Zibe Kidasi, Ali Said Mpima - Mzaramo, Suleiman Majisu, Raikes Kusi, Rawson Watts na Cecil Matola - Myao kutoka Masasi walianzisha African Association, Matola akiwa President na Kleist Secretary.

Historia ya uhuru wa Tanganyika iligeuzwa ikawa historia ya Julius Kambarage Nyerere.

Historia ya TANU ikawa historia ya mtu mmoja.

Hili lilifanikiwa kwa kuwa tulikaa kimya lau kama walikuwapo wazalendo wenyewe walioupigania uhuru kwa hali na mali zao.

Sasa tueleze harakati za uhuru wapi zilianzia.
Tunaweka picha ya Dictionary of African Biography (DAB).

Kinawekwa kipande kifupi kinachomweleza Dr. Kwegyir Aggrey (1875 - 1927) kisha ndani ya Kamusi hilo hilo tunatoa na kumwekea mtazamaji wa clip yetu kipande kifupi cha Kleist Abdallah Sykes (1894 - 1949).

Wazalendo hawa waliotajwa ndani ya Kamusi hilo tunaeleza hawamo katika historia rasmi ya Tanganyika.

Mazungumzo kati ya Waafrika hawa wawili Dar-es-Salaam mwaka wa 1924 ndiyo yalisababisha Kleist kuunda African Association mwaka wa 1929 kisha kuunda Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika (Umoja wa Waislam wa Tanganyika) mwaka wa 1933.

Vyama vyote hivi viwili vilitawaliwa na Waislam.

Watafute wazalendo hawa katika historia ya Tanganyika hutowakuta popote.
Jambo la kusikitisha ni kuwa watu waliamini kuwa ile historia iliyokuwa ikisomeshwa ndiyo historia ya kweli.

332955155_3398442657098751_5156298518240527622_n.jpg

Kleist Abdallah Sykes
333027833_3114434315528253_5075425198623726105_n.jpg

Dr. Kwegyir Aggrey

332914989_1164916214133995_6225086038975879163_n.jpg

Dictionary of African Biography
(DAB)​

Picha ya juu ni Kleist Abdallah Sykes, inayofuata ni Dr. Kwegyir Aggrey na chini ni Dictionary of African Biography.

Ninaposomesha historia ya utaifa wa Tanganyika huanza kwa kuwapa wanafunzi wangu rejea katika Dictionary of African Biography (DAB) niwaambia wamsome Dr. Aggrey wakimaliza wamsome Kleist Sykes.

Kipande hiki nimekipa jina: ''Meeting of the Minds.''
Nina ugomvi na wewe bwana M. Saidi
Ugomvi wangu ni huu... Kwa nini hauandiki kitabu cha historia iliyonyooka ya Tanzania?

Hizi makala ni nzuri sana lakini ipo jamii kubwa ya Watanzania haipo mitandaoni na wanaweza kuvifikia vitabu. Andika vitabu kwa sababu ndiyo hazina pekee ya mwenye hekima anayoweza kuiacha kwa vizazi vijavyo.
Andika historia kwa sababu namna yako ya tafiti na hifadhi ya kumbukumbu hususani namna ya masimulizi ni ya kipekee tofauti na wengine.

Punguza loloki fanya compilation ya makala zako, chapa kitabu sambamba na utoaji elimu kupitia makala

Tutaendeleza ugomvi bila shaka
 
Puna,
Limepita hilo ndugu yangu.
Clip hiyo hapo chini:

Hii clip iko sawa sema wamekosema kwenye language arabic sio language ya tanzania ni swahili na kiingilishi na kisukuma

Pia hii clip inaupotoshaji yani famous people JPM mwendazake hayupo,?
 
Bufa,
Kweli maneno yako mimi nimetafiti sana katika historia ya Uislam Tanzania.

Ikiwa wewe huchukulii "serious," hilo si ajabu ni wewe una hakika na ukitakacho.

Lakini nimealikwa kuzungumza vyuo vingi katika somo hilo.

Naamini unakijua kitabu changu, "The Life and Times of Abdulwahid Sykes (1924 - 1968) The Untold Story of the Muslim Struggle Against British Colonialism in Tanganyika," (1998).

We mzee pride itakuua,sometimes nakuonaga kama punguani vile uliyejaa majivuno na ubinafsi kupitia illusion za dini ya waarabu.
 
Big...
Sitetei imani nikiwa na maana Uislam kama dini.

Elimu hii sina kiasi cha kuweza kuhubiri.

Ninachotetea ni historia ya uhuru wa Tanganyika ambayo ni historia ya Waislam wa Tanganyika kwa umoja wao.

Historia hii ni historia ya wazee wangu babu na baba zangu.

Ilifutwa ikawa historia inayofundishwa ni ya Julius Nyerere peke yake.

View attachment 2532039
''The Life and Times of Abdulwahid Sykes (1924 - 1968)
The Untold Story of the Muslim Struggle Against British Colonialism in Tanganyika,''
Minerva Press, London 1998​

The winner takes all,jifunze hilo na kamwe hizo historia za wazee wako hazitafundishwa tanzania hii,wafundishe wajukuu zako huko madrasa.
 
Unatuambia kuwa wakristu, wapagani, wahindu wasio na dini hawana nafasi katika historia yako ya uhuru wa Tanganyika. Historia ya uhuru Tanganyika ni historia ya wazee wako na rafiki zao! Kwa mtazamo wako hata waislamu ambao hawakutoka Tabora na Gerezani nao hawana nafasi katika historia ya hiyo Tanganyika.

Kwa mtazamo huu una tofauti gani na wale ambao waliigeuza historia ya Nyerere kuwa ndio historia ya uhuru wa Tanganyika? Hautofautiani nao kwa sababu kwako wewe historia sahihi ya uhuru wa Tanganyika ni ya wakina Sykes.

Amandla....

Huyo mzee ni wa kupuuza,hana tofauti na hao anaosema wamepotosha,wakati naye anapotosha mengi tu kwa maslahi yake binafsi ni walio mtuma.
 
Luku...
Nakusihi niite kwa jina langu Mohamed au Mzee Mohamed.

Usinikate jina.
Mimi sasa ni mzee.

Haipendezi si kwangu wala kwako.

Unanitukania wazee wangu.
Kwa nini kaka iwe hivi?

Nimekuudhi kwa mimi kuchangia katika historia ya nchi yetu?

Kwa nini historia ya Nyerere ifutwe?

Historia ya Nyerere ipo kama ilivyoandikwa na historia ya wazee wangu imekuja na kupata umaarufu baada ya zaidi ya miaka 50 toka uhuru upatikane.

Wasomi wakubwa wa Tanzania wakiongozwa na Prof. Issa Shivji wameandika "Nyerere Biography," (2020).

Huu ni mchango mkubwa katika kuitunza historia ya nchi yetu.
Hapo kwanza ncheke. Mzee unalalamika kukosewa adabu kuitwa Mudi kifupi cha Mohammed huku wewe ukiwa ni bingwa wa kufupisha majina ya watu humu.

Mfano tu hapo Lukubuzo unayemlalamikia umemwita Luku.. ni ni unatakataa na nini unafanya?
 
Unatuambia kuwa wakristu, wapagani, wahindu wasio na dini hawana nafasi katika historia yako ya uhuru wa Tanganyika. Historia ya uhuru Tanganyika ni historia ya wazee wako na rafiki zao! Kwa mtazamo wako hata waislamu ambao hawakutoka Tabora na Gerezani nao hawana nafasi katika historia ya hiyo Tanganyika.

Kwa mtazamo huu una tofauti gani na wale ambao waliigeuza historia ya Nyerere kuwa ndio historia ya uhuru wa Tanganyika? Hautofautiani nao kwa sababu kwako wewe historia sahihi ya uhuru wa Tanganyika ni ya wakina Sykes.

Amandla....

Udini tu ndio unamsumbua.
 
Back
Top Bottom