Chizi Maarifa
JF-Expert Member
- Jul 29, 2013
- 10,931
- 24,816
Hivi ni kweli kwamba wazungu wametaka kutuua na kutufanya tusizaane kwa kupitia chanjo ya Korona?
Sidhani.
Watoto wetu nasi toka tunakuwa tumepata chanjo za tetenasi, pepopunda, sulua/surua n.k kwa miaka mingi. Na ushahidi wa chanjo ya Ndui upo begani mwa kila Mtanzania. Hizi chanjo sisi tunatengeneza wapi? Ili tuanzie hapo kwanza.
Chanjo hizi zote zinatoka Ulaya na Marekani na Madawa mengine mengi India. Kama kutufanya tuwe tasa wangetumia chanjo moja kati ya hizo wala hawana haja ya kutumia Corona.
Ni vitu vingapi tunatumia toka kwao? Asilimia 80 ya dawa zinatoka kwao.kwa nini wasituwekee humo virusi au bacteria ambao wana madhara?why waje kuhangaika sasa kwa kutumia Corona?
Tulienda nunua dawa ya Corona Madagascar kwa Kondoo/Ndama wenzetu. Maana hatukutaka za Mabeberu. Je matokeo yake imekuaje mpaka hii leo? Tuambiane ukweli.
Miaka yote matibabu hawa wakubwa wanaenda tibiwa nje ya nchi kwa nini wasidhurike huko? Wengine wana vifaa kwenye mioyo,wengine wamefanyiwa transplant, wengine wametibiwa kansa, tezi dume n.k why wasidhuriwe huko?
Mi nadhani ichukuliwe hiyo chanjo wapewe wataalam wetu wakaifanyie utafiti then waje watoe majibu ya kuonesha kuna hila kwenye hizo chanjo.
Mimi ningekuwa Beberu ngesisitiza waafrika, watanzania wazaliane sana ili tuzidi kupata soko la bidhaa zetu.population kubwa ya afrika ni mtaji kwa wafanya biashara huko kwao.
Lakini la kujiuliza lini afrika imeanza kuwa tishio kiasi cha wazungu kutaka teketeza au angamiza kizazi cha afrika? Mambo mengine tuwe na uhalisia jamani. Tusiwe tunaongea tu kama laymen.
Hawa wazungu walishakuna wakatutawala hapa hapa kwetu.wakatuchukua utumwani.wakachoka nasi wakaacha kututawala na kutuchukua utumwani. Wametuacha tuwe watumwa huku huku tuliko.
Sasa kuwaonesha sisi ni watu huru tupinge chanjo zao kitaalamu na kuonesha kasoro zilizopo kwenye chanjo zao.
Mi nakwambia wazungu wakitaka kutuua ni rahisi. Nenda kabatini kwako. Kaangalie dawa asilimia kubwa unazotumia. Angalia za kienyeji ni ngapi.
Kasome kwenye kadi yako chanjo alizopata mwanao. Kaulize tiba asili ni zipi kati ya hizo. Ukiumwa malaria,kifua,mafua,kuhara,kipindu pindu,dengue, typhoid. Uliza hosp wanakupa dawa zipi. Omba wakupe za tiba asilia kama wanazo.
Tufikie hatua tutumie akili kujenga hoja na si kunena vioja.