T14 Armata
JF-Expert Member
- Mar 7, 2017
- 12,362
- 41,886
Hii sayansi ya gravity, energy, speed, force ni ngumu sana kuliko maelezo na nguli kina Einstein wakitoa formula zao hivyo siijui.Hapa nimetoka kapa
Ila kwa ninayojua iko hivi, gravit forces hurudisha vitu chini ya uso wa dunia. Ukirusha jiwe unalipa kinetic energy ya kufanya movement na ikiisha linarudi chini.
Ile energy inayotumika kurusha chombo angani inakinzana na gravitational forces ili chombo kieleee, kadri inavyokuwa kubwa & speed kubwa ndivyo na gravity nayo inakuwa kubwa kukizuia kisitoroke. Mwili wa binadamu kwa kawaida unahimili 5 G forces ukizidi hapo mara nyingi you pass out, hii hutokea kwa watumiaji wa rollercoaster za watoto.
Ndege za abiria zinakuwa na pressurised cabin kwa sababu ya pressure, za kijeshi zenye kasi kubwa kuanzia kama 1.8 Mach hivi huwa na ujanja fulani umetumika kupunguza makali ya G forces rubani asihisi kizunguzungu, kuumwa kichwa, kutokwa damu puani na kutapika. Mojawapo ya ndege iliyokuwa na kasi sana inaenda hadi 3,500km per hour ni SR-71 Blackbird ya Marekani kwa sasa imestaafu. Marubani wake walikuwa na mambo mengi ya tofauti na training kubwa, viatu vyao kama unavyoona hapa vimefungwa kwa nyuma miguu isicheze na kuvunjika
Ndege hiyo inafika zaidi ya 200°C ikiwa angani hivyo inataka coating kwa rubani asihisi joto ndani. Sasa ukianzia ride kwenye airport lazima kifaa chako kiwe na sifa zaidi ya SR-71 Blackbird.
Alternatively, unatumia launcher/mothership carrier inaweka speed kubwa alafu inakirusha kifaa chako kikiwa na momentum na kipo angani mbali kinawahi kuchanganya injini nadhani ni ramjet. Hapa unapunguza makorokoro ya kuanzia chini na unafanya kifaa kiwe compact kama hii product ya US Air Force nayo ni Retired
Otherwise uwe na spaceship kama kawaida ilivyo uende anga za juu. Bado G forces zitakukatalia ila unavaa G-suits unazoona astronauts wanavaa. Zile zinapunguza, sasa kwenye speed of light ndio nasema hakuna teknolojia ya kutengeneza suits za kuwezesha hilo.
Nimeanzia mbali sababu umesema huelewi. Ukitaka kwenda na speed ya light fanya makubwa kuzidi hizi ndege mbili na hizo spaceships na rockets sababu friction itasababisha joto na hicho chombo kinachoenda kitazalisha joto kubwa zaidi kwenye skin ambalo hakuna lubricant itafanya kitu kwenye vifaa, hakuna heat sink duniani itahimili, hakuna material ya kuhimili joto kali vile na hakuna karibia kila kitu cha kuendana na mazingira hayo. Uanzishe sayansi yako mpya na gunduzi mpya metallurgy, conductors, insulators, etc.
Hii ni speculation ambayo ni sawa na hamna, sababu hakuna uwezekano wa kufanya chombo kiende speed ya mwanga. Ila sayansi haijawahi kugoma kujiuliza "WHAT IF?" kisa kitu fulani hakiwezekani.