SAYVILLE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 7,895
- 12,975
Tanzania tumekuwa tunahangaika kutafuta dawa ya matatizo yetu ya mpira. Uzuri mmoja katika soka letu tuna desturi nzuri ya timu za Simba na Yanga ambapo ni mtaji mzuri sana. Kwenye timu ya taifa au mashindano ya kimataifa ya vilabu tumeendelea kuwa dhaifu ukiacha mafanikio ya mara kwa mara ya Simba 🤣😂
Leo nitagusia dawa mojawapo kwa upande wa timu ya taifa.
Nchi hii inabidi turudi square one kwenye soka letu. Tubadilishe kabisa ufahamu wetu wa jinsi tunavyocheza mchezo huu. Kuangalia mpira wa EPL umetuharibu zaidi, Waingereza wanapenda sana mpira ila ligi yao na style yao siyo sahihi kwetu.
Ushauri wangu tuingia mkataba na nchi kama Ujerumani (SIYO UINGEREZA) na waanzishe Academy yao hapa.
Ujerumani ndiyo nchi iliyofanikiwa kubadilisha kabisa style yao ya mpira na sasa wako level ya juu kabisa hadi anaeeza kumpiga Brazil goli 7.
Hii leo tunaleta kocha wa Ufaransa, kesho tunaleta Mwingereza, keshokutwa Mbrazil ni kuwachanganya tu wachezaji. Tukumbuke wachezaji wetu hawana foundation nzuri ya mpira kuweza kumeza mabadiliko haya yote ya kimfumo.
Ikiwezekana, hata vilabu vyetu vyote visisitizwe kuchukua programs zitakazoletwa na wataalamu hao wa Kijerumani ili kujenga style inayoshabihiana. Inakuwa rahisi mchezaji anapofikia timu ya taifa, anakuwa zile basic concept ameanza kuzipata. Hili liendani na kupeleka makocha na wakufunzi Ujerumani ( au hiyo Academy iwe pia na program ya makocha).
Ningesema Spain au Uholanzi ila naenda na Ujerumani maana tuna historia nao zaidi na wameonyesha uwezo wa kubadilisha mpira wao. Pia naona kama Ujerumani alichukua sehemu ya style za Spain na Uholanzi.
Kutokea hapo tutakuwa na wachezaji wa kuuza kwenye ligi kubwa duniani (ingawa wengine watabadili uraia ila hilo haliepukiki) na mwisho wa siku tutapata wachezaji wazuri wa timu ya taifa.