Tugeuze uwanja wa ndege Chato kuwa Chuo cha Urubani

Tugeuze uwanja wa ndege Chato kuwa Chuo cha Urubani

Yeap wazo zuri sana hili .pale wangefundishia marubani ni eneo zuri sana kwa kuwa hamna traffic Sana au obstacles kubwa kama milima n.k as compared na viwanja kama HTKJ na HTDA.
 
Ile vile vyandarua vya msaada vina kazi sana. Wanazuia kuku wasile bustani, wanabebea makopo na kamba zake ngumu balaa na haichafuki kirahisi.
Kweli mkuu, hizo kamba ni imara sana.
Zimeokoa watu wa vijijini mno
 
Wengi tunafahamu kuwa kujenga uwanja wa ndege Chato lilikuwa ni jambo la ajabu kiuchumi na ukanda mbaya sana. Jambo lisilopaswa kutokea tena.

Lakini uwanja ule tusiuache uoze, ni pesa nyingi zimetumika. Napendekeza tuufanye kuwa chuo cha urubani. Serikali na watu binafsi wajenge shule za urubani maeneo hayo. Nchi inahitaji marubani, kuanzia ndege ndogo za kunyunyiza dawa mashambani na kuua nzige hadi wa kurusha dreamliner.

Naona hilo litakuwa ni matumizi mazuri ya uwanja ule.
Wakati huyo bwana anatapanya pesa, hatukuona, CCM haikuona? Bunge halikuona?

Taifa limeingia hasara tayari, tusikubali kuongeza hasara nyingine. Uwanja pekee, siyo kigezo kikubwa cha kuweza kuanzisha chuo cha marubani. Hicho kimoja kilichopo Dar, mpaka leo hakina miundombinu ya kutosha, tunalazimika kuwapeleka wanachuo Nairobi kwa baadhi ya kozi, halafu tukaanzishe chuo kingine huko kijijini?
 
Wazo Bora, chuo Cha urubani ama wakabidhiwe JWTZ.
Huyu Mzee angetawala 20 yrs SGR ingepita Chato then to Mutukula
 
Gbadolite of Tanzania..

Wasted taxpayers money!

That was simply a white elephant project due to Jiwe's arrogance

Still counting, we shall revisit
Ila bora ya Chato kuliko ya Gbadolote mkuu. Walau wa huku alijenga sehemu nyingi maeneo mengine ya nchi pia..
 
Wengi tunafahamu kuwa kujenga uwanja wa ndege Chato lilikuwa ni jambo la ajabu kiuchumi na ukanda mbaya sana. Jambo lisilopaswa kutokea tena.

Lakini uwanja ule tusiuache uoze, ni pesa nyingi zimetumika. Napendekeza tuufanye kuwa chuo cha urubani. Serikali na watu binafsi wajenge shule za urubani maeneo hayo. Nchi inahitaji marubani, kuanzia ndege ndogo za kunyunyiza dawa mashambani na kuua nzige hadi wa kurusha dreamliner.

Naona hilo litakuwa ni matumizi mazuri ya uwanja ule.

9B422EAA-4927-4440-B986-8A5C86FDA0F6.jpeg
 
Chuo cha pilots, siyo kama chuo cha Ualimu ambapo unafikiria tu darasa na mahali pakulala.
Vitu gani mbali na uwanja vinahitajika ambavyo vitatushinda kuvipata. Kitu kigumu na gharama kuliko vyote ni uwanja. Training aircraft za kufundishia zipo kibao tena kwa bei rahisi. Wakufunzi hawatushindi kupata. Jengo la chuo na hostel. Sijui zile simulators nk. Ni nia tu. Kama Nairobi na Ethiopia wana vyuo vya marubani sisi tutashindwa nini?
 
Kabisa. Mifugo ipate pahala bora pa kupumzika. In fact itaongeza thamani ya ng'ombe, mbuzi, na kondoo wa Tanzania soko la dunia.
Ndege inatua ananunuliwa ng'ombe anapandishwa ndege, kwenda kuliwa, hivyo lazima wauzike kea bei nzuri zaidi.
 
Gbadolite of Tanzania..

Wasted taxpayers money!

That was simply a white elephant project due to Jiwe's arrogance

Still counting, we shall revisit
Inasimikwa kuwa mkoa kesho kutwa.
 
Nina ndoto ya kununua ndege naomba uwanja ubaki nikirudi Nyumbani chato nipate pakufikia
 
Uzi kama huu umekuwa nadra sana JF siku hizi, Siku hizi zimejaa shombo tupu.

Hatuna chuo cha kufunza urushaji wa ndege, chato Airport ni pakuanzia. Serikali sikivu ifanye hima, tuna ndege nyingi sasa.
 
Wengi tunafahamu kuwa kujenga uwanja wa ndege Chato lilikuwa ni jambo la ajabu kiuchumi na ukanda mbaya sana. Jambo lisilopaswa kutokea tena.

Lakini uwanja ule tusiuache uoze, ni pesa nyingi zimetumika. Napendekeza tuufanye kuwa chuo cha urubani. Serikali na watu binafsi wajenge shule za urubani maeneo hayo. Nchi inahitaji marubani, kuanzia ndege ndogo za kunyunyiza dawa mashambani na kuua nzige hadi wa kurusha dreamliner.

Naona hilo litakuwa ni matumizi mazuri ya uwanja ule.
uko sahh bro
 
Back
Top Bottom