Tuhuma Hii: CHADEMA kuendeshwa kwa Katiba "Fake" ikithibitishwa, CHADEMA inaweza kufutwa

Mkuu Pasco

Samson Mwigamba alikuwa mpambanaji hasa siku za nyuma. Lakini usaliti wake ulianza pale alipoondolewa kwenye uhazini wa chama Taifa. Ndipo alipoanza mradi wa kuchafua chama kwa siri ama kwa kutumwa au kujituma mwenyewe!

Samson Mwigamba alitumia njia mbalimbali za siri na za wazi kulaani kufukuzwa chamani kwa masalia Mtela Mwampamba na Juliana Shonza kwa madai kwamba wameonewa!

Nilishtuka na kushangaa kuona mtu kama Mwigamba akitetea wahalifu wale.Pia Mwigamba amekuwa akitumia njia mbalimbali kumchafua mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema na ushahidi upo.

Mimi nasema Mwigamba ni mchumia tumbo na mamluki mkubwa kwa sababu kabla ya kuposti huo upuuzi wake anaoita tuhuma alisimama mbele ya wajumbe wa Kanda na kumimina kila aina ya sifa kwa uongozi wa Mbowe na Dr Slaa! Halafu alipomaliza kuhutubia akaenda kuposti ujinga ule...

Ndani ya Chadema zipo njia huru kabisa za kuwasilisha maoni na waliobahatika kuhudhuria vikao vya baraza kuu na Kamati kuu wataniunga mkono kwa hili..

Mimi niseme wazi Samson Mwigamba ana chuki kuu kufukuzwa Uhazini Chadema na mwanzoni alilalamika kafukuzwa na Dr Slaa. Tunafahamu alienda kwa Mbowe kulalamika lakini Mbowe akamuambia hawezi kutumia udikteta kumrudisha ndipo chuki dhidi ya Mbowe pia ilipoanzia!

Mwigamba anadanganywa na maadui wakuu wa chadema waliojipanga kusambaratisha Chadema kwa kila njia. Lakini kwa taarifa yake Chadema inaufahamu mchezo wake siku nyingi.

Alidiriki kujitenga na chama wakati wa uchaguzi mdogo wa madiwani Arusha na kipindi chote cha kampeni aliondoka Arusha. Kazi yote ya kampeni ilifanywa na Lema na Katibu Amani Golugwa.Nilielezwa kwamba alitaka Chadema ishindwe ili apate nafasi ya kumshambulia Lema..!!

Mtu wa aina hii nitasema ni msaliti na hastahili kuwa kiongozi wa Chadema. Angejua anachosema ni cha kweli kwenye hotuba yake ya jana angeushambulia uongozi na kuanika mabaya yote halafu wanachama waamue. Lakini kitendo cha kuusifu uongozi huku ukitoka njema unapigiana simu na maadui wa Chadema ni unafiki usiovumilika!!!!!
 
Mhusika kama anaona chama kinaendeshwa kwa katiba feki na yeye ni kiongozi alipaswa kufuata taratibu na kanuni za chama kupeleka malalamiko yake.
 
Mkuu Mpaka Kiele, kwanza sina mawasiliano yoyote na kiongozi msimamishwa!.

Pili uongo hukanushwa na kuwa replaced na ukweli!, hizi ni tuhuma tuu na bado hazina uthibitisho, nasema na nasisitiza, ikithibitishwa!, Chadema is in trouble!.

Hili la kuletwa nyaraka ndizo hoja zangu, miniti za mikutano ni public documents, ziletwe tuumalize huu utata!.
Pasco.
 
1. Wakati tukifanya mabadiliko ya katiba mwaka 2006 hatukugusa kipengele kinachomzuia kiongozi kuongoza kwenye nafasi moja kwa zaidi ya vipindi viwili vya miaka mitanomitano. Lakini wakati katiba inachapwa chini ya uongozi uliopo, kipengele hicho kiliondolewa kinyemela. Mambo yanayotokea hivi leo yanaonyesha dhahiri kipengele hicho kiliondolewa kwa makusudi kwa maslahi na kwa faida ya viongozi waliopo madarakani kwa sasa. Hiki kinaweza kuchukuliwa kama kitendo kidogo lakini kama viongozi wetu wanaweza kutokuwa waaminifu katika jambo kama hili, ni dhahiri hawawezi kuaminika na wanaweza kufanya mambo mengine makubwa nayenye athari zisizomithirika kwa chama.

Huku ni kuota kama sio kuoteshwa , maana wakati huo Mwandishi huyu hakuwa hata kiongozi wa Chadema , alikuwa mfanyakazi wa UN- ICTR Arusha kitengo cha fedha, sasa leo anaandika kama alikuwa mjumbe wakati hakuwa hata mwanachama kwa wakati huo. Pasco fanya utafiti kabla ya kuhukumu.
 
Ni application ya common sense tu.

Kwa ku-Apply common sense ni wazi kabisa imesemwa kipindi hiki kwasababu wananchi wamekuwa na mwamko mkubwa na hawataki blah! blah! tena.

Hakuna mwananchi atakayekuelewa kwasasa umwambie akaandamane kuipinga katiba na wakati huohuo katiba ya chama chako mwenyewe umeichakachua.
 
Pasco tumeshakuzoea na uvuvuzela wa kufutwa kwa chadema hii si mara ya kwanza kuja na propaganda kama hizi nakumbuka kuna habari ulikuja nayo hapa kuwa ulikutana na aliekuwa msajili wa vyama vya siasa Tendwa na akakuakikishia kuwa ataifuta CDM,Pasco unakumbuka? Leo unakuja tena na porojo kama zile zile Pasco badilika unaharibu jukwaa hili na jamii forum pia unaishushia hadhi badilika hacha ukanjanja.
 

Ushaambiwa mwaka 2006 huyo Mwigamba alikuwa UN-ICTR na hakuwa kiongozi kwa ngazi yoyote CHADEMA sasa yeye alijadili na nani hicho kifungu cha ukomo wa uongozi kwenye katiba?
 

Mmmmhhhh haya
 
Minyoo huwa haikosekani tumboni...ikizidi tunakunywa dawa ya minyoo.

Tujifunze kuishi na minyoo.

Yesu pia alisema "maskini mtakuwa nao hata mwisho wa dunia."

CDM msijali, kuna baadhi ya watu wataendelea kuwepo ndani ya cdm siku zote. Mmojawapo ni Zitto.
 
Timu Edward, si upo kwenye huo mradi ama unataka nyaraka ndio ujue kuwa mambo sasa ni hadharani? Nimekwambia Samson hakuwa hata mwanachama mwaka 2006 wakati katiba inarekebishwa , sasa wewe kumtumia kama reference yako na kuanza kutoa hukumu unaona ni sawa? Fanya utafiti nyaraka zipo , tafuta wajumbe wa mkutano mkuu wa Chadema wa mwakac2006 wakupe nyaraka husika walizopitisha .
 
hivi tangia lini umeanza kuimba huu wimbo wa chadema kufutwa?
 

Interesting, kwa hiyo mtuhumu amegeuka mtuhumiwa na kusimamishwa ili kufanya uchughuzi wa tuhuma zake huku mtuhumiwa ndio mwendesha uchunguzi na kesi.... Yana mwisho wake haya!
 
Safi sana Molemo,

Ukiacha yeye kujitenga uchaguzi wa madiwani Arusha hata uchaguzi wa marudio ya ubunge wa Arumeru Mashariki alishiriki kwa kinyongo, utakumbuka wakati huo tuhuma za akina TUNTEMEKE dhidi ya Slaa zilikuwa zimepamba moto, wakati huo ndipo Mwigamba aliposimamishwa uhazini wa chama kwa kutoa siri za chama kwa masalia.

Mimi nafikiri hata ikithibitika ndivyo sivyo Mwigamba asiaminiwe tena kwenye ngazi kubwa kama ya Mwenyekiti wa Mkoa.
 
Pasco kaingizwa choo cha kike. Na huyu Mwigamba alipewa uhazini kwa sifa zipi? Upungufu wenu kwenye umakini ndio chanzo cha matatizo yote haya. Tegemeeni dhahma kubwa mbele kwa vyeo mnavyogawana kama zawadi na kwa kujuana pasipo kujali sifa na uwezo.
 
CHADEMA ni chama cha demokrasia na maendeleo nchini!. My foot.

They can't even talk the talk let alone walk the walk.

CHADEMA siyo chama cha siasa ndani ya demokrasia kwa manufaa ya demokrasia bali ni private-owned enterprise through political project.

Chama kilichojengwa kwa misingi ya kilaghai hata uendeshaji wake utakuwa niwa kilaghai.

Kama wewe ni kiongozi wa CHADEMA ukijitambua na kuhoji uendeshaji na malengo yake kisiasa lazima utapatwa na mambo matatu kiuongizo,

1) Kusimamishwa na baadaye kufukuzwa kama huna nguvu ya kisiasa nje ya chama.
2) Kutengwa kikazi ili usiendelee kufahamu madudu yanayofanyika zaidi kama una nguvu za kisiasa nje ya chama
3) Kama ukiendelea kupanuka kisiasa baada ya kutengwa ndani ya uongozi, basi unapelekwa ahera ili jina lako libakie kama historia kwenye makabrasha ya chama.

Hawa viongozi wanaokiongoza chama kwa iron fist huku wakitumia kangaroo committee watawanyamazisha viongozi waliojitambua ndani ya uongozi mpaka lini ili watimize malengo yao ya financial mission through political mission.
 
Pasco and your team THIS IS JUST A WIND BLOWING FROM LUMUMBA. It is going to pass like others which passed.

Msimamizi wa vyama ni msajili kama na yeye hakuliona hili basi nchi ina tatizo kubwa kuliko tunavyoiona. Nasubiri mchango wa Nape na Mwigulu kwenye hili.
 
Chadema ni chama kinachoendeshwa katika misingi ya kilaghai.

Mambo mengi yanafanyika kimagumashi bila kufuata katiba, kwa mfano:
1. Matawi nje ya nchi yamefunguliwa kinyume cha katiba na matawi yao hayaelezewi kikatiba yana nafasi gani ndani ya chama.
2. Kanda zimenzishwa kimagumashi bila mabadiliko ya katiba.
3. Mwenyekiti anajifanyia maamuzi bila kuheshimu maamuzi ya vikao kama katiba inavyotaka. Mfao pale aliposema wanaohamia Chadema wasipewe uongozi, jambo ambalo ni kinyeme na katiba inayosema kila mwanachama ana haki ya kuogmbe uongozi.

Kujiunga chadema kichwakichwa ni kupotoka...
 
Pasco

Badilika mkuu usiwe na mawazo ya kudhani Chadema kitafutwa bila kuwa na sababu za msingi, maana sio mara ya kwanza kutuambia hivyo leo umekurupuka tena na mawazo yale yale angalia thread yako hii https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...dema-kufutwa-kwa-mujibu-wa-katiba-endapo.html

Nazidi kusema unaendeshwa kwa matukio ya kukurupuka, unakumbuka mara tu baada ya tukio la video ya Lwakatare ulituambia umeiona na ni "bonafide genuine" jaribu kuwa na ile aibu ya kawaida.
 

Hoja inayojadiliwa hapa sio Mwigamba ni nani na amefanya nini.

Hoja ni je, vikao halali viliidhinisha kufutwa kwa kipengele cha katiba kinachoweka ukomo wa vipindi vya uongozi?

Hii ndio hoja yetu. Hayo mengine ni nje ya mada.

Turudi kwenye hoja, je, una ushahidi wa uhalali wa kipengele hicho kuondolewa?

If yes, je kipengele hicho kiliwekwa kwa mantiki ipi hapo mwanzoni? Je, mantiki hiyo imebadilika vipi mpaka kiondolewe?

Vijana werevu wameshatambua kuwa chadema ni chama kinachoendeshwa katika misingi ya kilaghai.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…