Tuhuma za matumizi mabaya ya fedha: Wabunge wa CHADEMA waanza kuhojiwa TAKUKURU

Tuhuma za matumizi mabaya ya fedha: Wabunge wa CHADEMA waanza kuhojiwa TAKUKURU

Kule Kangi na wenzake wanawaachia wakati walisema uchunguzi umeshakamilika, halafu wanajidai kupambana na rushwa.

Haya maigizo sijawahi kuyaona.
 
kuna walevi wanaoteguka miguu na kusingizia wamebakwa na wahuni
Yaani wewe kila watu wa aina hii wakisema unaamini? Au na wewe ni kama wao?

 
Naona Lisu anakuja kuchomoa betri,mtaongea vizuri hivi punde.
 
Naam, wanahojiwa tu ingawa bado sijaelemewa kwanini wanahojiwa na chombo cha makosa ya rushwa wakati tuhuma ni matumizi mabaya ya fedha! Lakini pia tukumbuke kuwa kuna wakati zilitolewa tuhuma bungeni kuwa baadhi ya wabunge wetu wamepewa rushwa ya sh. 10m/= kila mmoja kipindi cha kuelekea kujadiliwa miswada ya sheria iliyokuwa na utata mkubwa. Kiti cha Spika kulizuia tuhuma hizi zisijibiwe bungeni. Baada ya muda Rais Magufuli alipokutana na vyombo vya habari kwa mara kwanza aliulizwa swali kuhusu tuhuma hizi hizi. Rais alijibu kuwa atakabidhi TAKUKURU. Hakuna mrejesho wowote uliotolewa kwa umma kuhusu tuhuma hizi nzito mno.
Haya ni matokeo ya kuwapa nchi washamba,hawana jipya.
 
Kati ya Taasisi ambazo zitafanyiwa reformation kubwa au kuvunjwa kabisa na kuundwa upya baada ya CCM kutoka Mahakamani hapo October namba
1. TISS
2. Takukuru
3. Polisi
4. Magereza

Naona JWTZ ndo taasisi pekee itakayoepuka mkono huu maana ndo taasisi pekee iliyofanikiwa kujitenga na siasa uchwara za CCM
Mkuu labda niulize; hawa JWTZ licha ya kumilikiwa na CCM wamewezaje kujinasua na makucha yao?
 
Wabunge wa CHADEMA leo wameanza kuwasili katika ofisi za TAKUKURU jijini Dodoma kwa ajili ya kuhojiwa. Mbunge wa Mbeya mjini, Joseph Mbilinyi (Sugu) amekuwa wa kwanza kufika.

TAKUKURU ilisema itawahoji wabunge 69 wa chama hicho kufuatia malalamiko juu ya matumizi ya fedha za makato katika mishahara.

Pia soma > TAKUKURU kuwahoji Wabunge 69 kuhusu matumizi ya pesa za CHADEMA
General Mbung'o ukweli ikiwa umepata maelekezo hapa historia haitakuacha salama wewe na uzao wako.
Hatujapata kushuhudia kipindi ambacho taasisi zinazoendeshwa kwa kodi za wananchi zikiacha kufuata taratibu za kisheria na maadili ya uwazi na kujitegemea ili kutekeleza maagizo ya mtu mmoja au kikundi chenye nia ovu. Tumeshuhudia Kilangi AG akileta katika jumba la kutunga sheria maagizo ya kuhakikisha wahalifu viongozi na watoa amri na maagizo ya kihalifu hawashitakiwi na sheria za nchi hii.
Tutashuhudia mengi ila hakikisheni mnajitoa ICC mapema sana!!
 
Back
Top Bottom