Wakati akifunga kampeni za CHADEMA (siku moja kabla ya uchaguzi) kwenye viwanja vya Tanganyika Packers, Kawe; Lissu alisema kuwa matokeo ya uchaguzi wa urais yameshapikwa.
Akadai kwamba amedokezwa na watu walio ndani ya mfumo kuwa Magufuli atapata kura milioni 12 na wengine wataambulia kura milioni 3 (Jumla ya kura, milioni 15). Na kweli kwenye taarifa rasmi ya matokeo ya uchaguzi wa rais, Magufuli alitangazwa mshindi kwa kupata kura 12,516,252 kati ya kura 15,091,950.
TUTAFAKARI.