Tuhuma za rushwa ya ngono kwa madaktari bingwa Hospitali ya Rufaa ya kanda Mbeya

Tuhuma za rushwa ya ngono kwa madaktari bingwa Hospitali ya Rufaa ya kanda Mbeya

Status
Not open for further replies.
Hili lalamiko
Unaweza kuliwazilisha kwa wizara Afya chini ya waziri Ummy Mwalimu, nafikiri litafanyiwa kazi mara moja .Haya maswala ya sexual harassment hayatakiwi kabisa kwenye maofisi ya serikali maana yanawakatisha tamaa wanafunzi wengi ktk jamii
 
Umeandika kwa hisia sana, pole sana Daktari.

Madaktari mliotajwa na ambao hamjatajwa acheni ushenzi huu, mnakwama wapi kufuata maadili ya kazi baina ya mfanya kazi na mfanya kazi....!

Mamlaka husika fanyieni kazi habari hii ili mtokomeze tabia hii chafu.
 
Tatizo mabinti na nyie mnawashawishi Wasimamizi wenu, mabinti wengi wanapenda kusaidiwa kufaulu na muda mwingine mnaumalizia kwenye smartphone zenu ikifika muda wa mitihani mambo hayaendi mnakuwa mnataka slope, Hafu napo mjiangalie mahusiano yenu mnapenda sana kuchekacheka na Lecturers na kuwatega na wao ni binadamu.
 
Ni kweli kabisa,mimi pia nimependa,hakuna haja ya kumficha mtu kama anafanya ujinga.
Katika andiko hili nimependa vitu viwili.

1. Umeandika kwa mtiririko mzuri

2. Hujaona haya kuwataja MAJINA. Nadhani mpaka sasa Familia, Ndugu, Jamaa na Marafiki watakuwa wamezifahamu tabia zao mbaya.

Hongera sana
 
Kwanza nakupa pole sana maana mimi ni mdau mzuri wa pale hospitali inshort ni mkazi wa Mbeya mjini.
Peleka malalamiko yako ofisi ya takukuru kimyakimya au ikiwezekana nitafute mimi tusaidiane kuwawekea mitego pamoja na maafisa wa takukuru.
Mbona simple sana yani ulitakiwa kusema mapema maana mimi mwenyewe ni baba wa watoto 2 wakike wanasoma kwahiyo nimeumia sana.
Awamu hii ya 5 itawanyosha kama bado upo hapo rufaa nicheck inbox tuanze kazi.
Hahaha akutafute au sio?
 
Unyanyasaji wa kingono haukubaliki. Vyombo husika vifanyie kazi haya malalamiko
 
Bila ushahidi hakuna atakayekuelewa ulitakiwa kwenda takukuru ungeeleweka zaidi, la sivyo unawasingizia
 
Pia kuwa makini na wanaotaka kukusaidia. Kumbuka JF veryfied members ni wachache.

Unaweza kudhani kuwa wanataka kukusaidia kumbe ni haohao wanataka kujua mleta tuhuma ni nani.

TRUST NO BODY
Siwezi kufanya hilo kosa. Nimetafakari sana kabla ya kufikia uamuzi wa kulileta hili humu ndani. Naelewa pia hata baadhi ya hao washenzi niliowataja ni members humu.

Kitu pekee ambacho i hope kitatokea ni kwamba serikali/wizara ya afya itapata tuhuma hizi na kufanya uchunguzi wake huru na kuchukua hatua.

Najua nguvu ya JF.
 
1. Umeandika kwa mtiririko mzuri
Pamoja na kiswahili fasaha.

Ila ukikutana kwenye anga zake za mwandiko wa mkono kwenye mafile, lazima upate kwikwi[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] maana hutaambulia kuelewa hata neno moja
 
Nilichosikitika zaidi ni hao TAKUKURU, wanafanya mambo ya kisenge sana, yaani hawa jamaa hata wao ni tatizo kubwa sana. Viongozi mnaopita pita hum, fanyieni kazi inshu kama hizi
 
Ahsante sana.

Lakini sio rahisi kama unavyosema, wakati bado nikiwa hapo hospitali tuliwahi ripoti TAKUKURU tukaweka na mtego vizuri, lakini mtego ulifyatuka,haukufanikiwa na inasemekana walikua tipped off na mmoja wa maafisa wa TAKUKURU aliekua anafahamu huo mchezo.

Kumbuka hawa ni madaktari bingwa,wamefanya kazi hapo Mbeya muda mrefu,wana connections za kutosha, kama ujuavyo tena kwa madaktari nadhani utaelewa kuwa ni rahisi wao kuwa na connections kiasi hiki. Inahitaji uchunguzi wa haki na wa uhakika na mipango dhabiti ili haki itendeke.

Nimeamua kulileta hapa nikiamini kuwa humu JF wahusika wa serikali na/au wizara ya afya wapo, wanaweza kufanya uchunguzi wao wa kimya kimya na kuchukua hatua.
Pole sana, kama kweli uliliport pccb na wakaweka mtego ukafyatuka kwa Afisa kuvujisha siri, please nakuomba ufike pccb makao makuu ukiwa na malalamiko yako, wachunguzi watatoka HQ kulifanyia kazi so nakushauri malalamiko yako yasiishie hapa!
 
Ndio mana magu alisema,TAKUKURU pia inahitaji TAKUKURU jamaa ni wapigaji kama wapigaji wengine tu.
Nilichosikitika zaidi ni hao TAKUKURU, wanafanya mambo ya kisenge sana, yaani hawa jamaa hata wao ni tatizo kubwa sana. Viongozi mnaopita pita hum, fanyieni kazi inshu kama hizi
 
Aisee inasikitisha sana, wakati wengine wanahangaika kusomesha vijana wao wengine wako busy kuwaharibia maisha yao!

ni hatari sana!
 
Bila ushahidi hakuna atakayekuelewa ulitakiwa kwenda takukuru ungeeleweka zaidi, la sivyo unawasingizia
Ahsante kwa mawazo yako.

Kama ni mtu ambae uko resonable, naamini unaelewa changamoto iliyopo juu ya ushahidi wa ishu za aina hii, pia kuna comment nimeeleza kuwa tuliwahi kujaribu kusuka mtego na TAKUKURU, ila afisa mmojawapo aliwa tip off watuhumiwa na mtego ukaharibika, haukufanikiwa.

Pili, soma vizuri thread yangu, kuanzia heading nimeanza na neno "tuhuma"; Vyombo husika wana nna yao ya kufanyia uchunguzi tuhuma za hivi na hata kuchukua hatua kwa kadri wanavyoona inafaa.

Nashukuru.
 
Kama huyu dogo wa upasuaji yumo humu
Hahahaha, ujumbe utakuwa umemfikia.....hapo anajitahidi kumjua mleta mada.
Familia inapata aibu kisa kichwa kidogo, noma sana 😲😲
 
Nakushauri fika PCCB HQ DSM itafanyiwa kazi na kama pccb mbeya waliipuuza itawafyatukia wao kwasababu kufyatuka kwa mtego sio mwisho wa uchunguzi!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom