Naandika uzi huu kutoa experience yangu juu ya tuhuma za baadhi ya madaktari bingwa wa hospitali ya rufaa ya kanda Mbeya. Mimi nimemaliza internship hapo hivi karibuni.
Niseme tu, kati ya madaktari bingwa waliotajwa kuhusika, Dr. XXX wa Idara ya Medical ndie ambae naweza kumzungumzia, kwani alifanya maisha yangu kuwa magumu sana hapo wakati nafanya internship. Alikuwa akinisumbua kwa kunitongoza, na kunilazimisha nifanye nae mapenzi.
Mwanzoni alianza kwa kunibembeleza na kuniahidi vitu kibao kama vile kuniunganishia kazi sehemu baada ya kumaliza intern, na kuninunulia gari. Alipoona bado nimekuwa mgumu, ndipo sasa alipoanza vitisho na kuniambia kuwa atafanya maisha yangu ya internship yawe magumu kuliko ninavyofikiria. Ilifikia hatua ya kuongezewa wiki mbili zaidi Idara ya medical kwa madai kuwa siko competent, lakini sababu hasa ilikua ni kumkatalia penzi alilotaka kinguvu.
Huyu Dr XXX anapenda sana wanawake, na ana tabia ya kutembea na mabinti wanaopita hapo hospitali kama wanafunzi au interns, na ana vimada wengi ambao walipita hapo kama interns au wanafunzi. Baadhi yao amewaunganisha na ajira taasisi kama NIMRI kwa kutumia connections zake. Niwe mkweli kuwa pia baadhi ya mabinti hutumia udhaifu wake huo na kujipendekeza kwake, hivyo kuwa na mahusiano nae kimapenzi na kufanya maisha yao ya uanafunzi/intern kuwa ni mtelezo; lakini tunaokataa ndio ambao hupata shida na manyanyaso kutoka kwake.
Inasikitisha sana pale ambapo wasomi wa aina ya Dr XXX ambao wameaminiwa na jamii na serikali, wanapotumia nafasi zao kuridhisha matamanio yao ya kingono na kuwanyanyasa wale ambao wanakataa kuendana na matakwa yao.