DOKEZO Tuhuma za Siasa chafu "Law School of Tanzania" wahusika wajitokeze kuzijibu

DOKEZO Tuhuma za Siasa chafu "Law School of Tanzania" wahusika wajitokeze kuzijibu

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Kumekuwa na malalamiko ya muda mrefu kuhusiana ukiwamo utahini kwenye chuo hiki cha umma.

Takwimu hizi za matokeo ya hivi karibuni zinajionyesha:

View attachment 2381450

Hii ndiyo ilivyo hali ya pale LST kwa miaka nenda rudi.

Ada ni 1,570,000/- kwa mwaka inayotakiwa kulipwa yote kabla ya kuanza masomo.

Chuo hiki hakitambui hali halisi za watanzania na kuwa ni kwa kujinyima mno kwa wazazi kuwasomesha watoto wao kuishia kwenye siasa uchwara za hapo chuoni kwao.

Mitihani supplementary huwa haina ukomo ikilipiwa 30,000/- kwa component baada ya supplimentary ya kwanza. Course moja Ina components 3. Hivyo supplementary ni 90,000/- kwa course.

Vitabu vya walimu husika ni lazima wanafunzi kuvinunua kwa mzengwe wa kutosha. Photocopy za vitabu hivyo vinavyoruhusiwa kwenye mitihani ni batili.

Kuna pass mark 'dash'(-) zisizojulikana kwenye matokeo ya wanafunzi. Ambapo mtu mmoja katika course mbili, moja anaweza pata 'dash' kafaulu na nyingine akapata 'dash akawa kafeli.

Wanafunzi wawili pia somo hilo hilo, mmoja anaweza pata 'dash' kafaulu na mwingine 'dash' kafeli.

"Inawezekana namna gani?"

Malalamiko yako mengi yenye kuashiria fursa za rushwa za aina zote katika kujaribu kujinasua na vitanzi vya wazi vilivyopo chuoni hapo.

Ikumbukwe wanafunzi LST ni wahitimu wa shahada za kwanza, uzamili na hata uzamivu. Bila ya cheti Cha LST uhitimu wowote wa sheria ni kazi bure.

Kuna tuhuma za undugunization na ukabila. Kuna kujuana na connections. Katika wafanyakazi takribani 50 waliopo pale, wapo kadhaa wa kutokea familia moja (baba mmoja, mama mmoja) kama waajiriwa.

Wanafunzi wanaopata nafasi zaidi za kufaulu ni wale wenye unasaba na vigogo wa serikali wakiwamo mawaziri, majaji nk. Wenzangu na miye utakata rufaa katika mahakama ipi kwenye hali hii.

Chuo kimekuwa kama si taasisi ya serikali bali mali ya watu binafsi.

Kama kwa kufeli wanafunzi ni uhakikisho wa waendeshaji kujipatia mapato zaidi, watafaulu vipi wanafunzi kwa halali?

Kama walimu ni miungu watu kiasi hiki, ukimwi utakwisha kweli Tanzania hii?

"Hiki ni chuo cha umma, wenye dhamana hawawezi kuchagua kukaa kimya."

Bahati mbaya, ya namna hii si kwa LST peke yake.

Vimullikwe vyuo vyote vya elimu ya juu. Kutenganisha watunga mitihani, wasahihishaji na walimu wa course husika kuwa ni jambo la dharura sana.
Halafu unategemea majaji watoe haki: akina Siyani- Slippery and unobjective character sasa ni jaji kiongozi!
 
Upumbavu ni subjective. Kwanini hudhani mtetea upumbavu unaweza kuwa wewe?

Nikurejeshe kufahamu hata MUCHS kuliwahi kuwapo hali mbaya labda kuliko hizi.

Ilikuwa ni kelele za waungwana kama sisi zilizowaondoa wakware wa rushwa za ngono na mambo leo ni murua.

Hata enzi hizo wapumbavu wenye kutetea upumbavu kama wako walikuwapo.

Wewe Kaa kwa kutulia. Safari hii tumedhamiria kweli kweli.
Mkuu ulipoliguza kwenye mboni ya jicho! ni mmojawapo wa wala rushwa wa LST hao. Yanayotuharibikia mihimili yetu kwa kutoa vilaza wasiojiamini!
 
Mkuu ulipoliguza kwenye mboni ya jicho! ni mmojawapo wa wala rushwa wa LST hao. Yanayotuharibikia mihimili yetu kwa kutoa vilaza wasiojiamini!

Yalidhani yataendelea kuwadanganya watu wote siku zote.
 
Haiwezekani wanafunzi wengi kiasi hicho kufeli kama waalimu walitimiza wajibu wao! Waalimu hao wachunguzwe huenda wao ndiyo vilaza!
 
Mkuu miye ni mmoja labda kati ya wa wachache waliochagua kuwa impartial kwenye mada zako nyingi ukizodolewa kuwa opportunist.

Kwenye hili la LST naweza kusema rangi zako kamili zime dhihirika. Hayupo examiner au mamlaka yoyote ya utahini popote yenye kuweza kukubaliana na uozo huu:

View attachment 2383192

Kila mwaka na wewe una shadadia kwa bashasha kuwa ni sawa?

Kwa hakika hata primary school achilia mbali kindergarten kama wanafunzi wamefundishwa na kuwa examined fairly, haikubaliki.

Kumbe nini tofauti yako na wajumbe walio na capacity za kujadili Simba na Yanga au mapigano ya kina Mandonga peke yake ambao kiuhalisia huwa tunawasajili kwenye ignore list wanako stahili?

Fuatilia kokote kujiridhisha matokeo ya mitihani hayawezi kuanguka nje ya standard curve hii:

View attachment 2383202

Kwamba wewe ulisoma kwa Bino ukiwa na sifa kuu ya ulevi uliopindukia hadi wa kuangusha magari na kuokolewa na ma Aqwi wa huko ni kweli huyajui haya?

"Dar wanafahamika kuwavua walevi waangusha magari na kuwavunjia mayai Ili kuwatia adabu. Hivi utalaamu huo ulikuwa haujafika Arusha enzi hizo?"

Tuna bisha kwa sake ya kubisha tu? Kweli tumefikia huko?

Tuhuma zilizopo huzioni kuwa zinastahili majibu kamili? Kama majibu huna, wanafunzi wa St. Mary's Mazinde wanahusika vipi hapa?

Zingatia wanafunzi 600 wa LST ni graduates wa vyuo vyote nchini bila exception. Kwa hakika hata graduate wa Havard University asingetoboa.

Kwamba ukweli huo huujui au unadhani kuna fursa ya uteuzi uki side na establishment?

Kama huna hoja mkuu, mbona ustaarabu si ni kuufyata ndugu?
Kama na wewe ni 'wakili msomi' naona na wewe ni walewale. Huwezi kuargue bila matusi!
 
Kama na wewe ni 'wakili msomi' naona na wewe ni walewale. Huwezi kuargue bila matusi!

Matusi unayasoma wapi ndugu? Mbona ni ustaraabu wa kawaida tu kutokuweka tafsiri zako binafsi kama ambavyo ungetaka kwenye maneno ya mwingine.
 
Upumbavu ni subjective. Kwanini hudhani mtetea upumbavu unaweza kuwa wewe?

Hata enzi hizo wapumbavu wenye kutetea upumbavu kama wako walikuwapo.

Kifupi ajue tu kuwa upumbavu ulianza zamani sana, hatumshangai kwa yeye anapouonesha maana sio jambo jipya.
 
Haiwezekani wanafunzi wengi kiasi hicho kufeli kama waalimu walitimiza wajibu wao! Waalimu hao wachunguzwe huenda wao ndiyo vilaza!
Wahamishwe, LST waje walimu wengine kutoka taasisi mbalimbali za elimu za serikali, walimu wa LST wasijipe umuhimu kihivyo. Wameonea watu, INATOSHA sasa
 
swali ambalo huwa najiuliza, kama hawa waalimu wa lawschool ni wazuri sana, mbona huku mahakamani tunawazidi akili? au ni hasira za wivu wa maendeleo?
Wanapanic balaa. Wanajifanya wanajua sheria kuliko watu wote, huku uwezo huo haupo kiuhalisia. Wanaficha aibu zao kwa kufelisha wanafunzi
 
swali la kujiuliza, wanajitetea kwamba wanafunzi hawaandaliwi kwenye vyuo wanavyotoka, that means including UDSM. na huo ujinga waalimu wa udsm ndio wameuleta. mtakufa na roho mbaya zenu, mbona tukikutana mahakamani ni kama sisi ndio waalimu wenu?
 
Taaluma ya kijambazi ambayo humnyang'anya haki mwenye haki kwa kutumia ujuzi wa kusema kwa kumhofisha mwenye haki.
Taaluma ya kumtetea mwizi ili aonekane hana hatia ili hali huyo mtetezi (wakili) akijua huyo anaemtetea kaiba kweli.
Taaluma ya uwakili haina hata chembe ya ubinadamu kutokana na tabia yake ya kupindisha ukweli hata kama huyo wakili analijua hilo cha msingi kwake ni kupata pesa tu.hawa jamaa sijui makanisani na misikitini huwa wanafuata nini
 
Kumekuwa na malalamiko ya muda mrefu kuhusiana ukiwamo utahini kwenye chuo hiki cha umma.

Takwimu hizi za matokeo ya hivi karibuni zinajionyesha:

View attachment 2381450

Hii ndiyo ilivyo hali ya pale LST kwa miaka nenda rudi.

Ada ni 1,570,000/- kwa mwaka inayotakiwa kulipwa yote kabla ya kuanza masomo.

Chuo hiki hakitambui hali halisi za watanzania na kuwa ni kwa kujinyima mno kwa wazazi kuwasomesha watoto wao kuishia kwenye siasa uchwara za hapo chuoni kwao.

Mitihani supplementary huwa haina ukomo ikilipiwa 30,000/- kwa component baada ya supplimentary ya kwanza. Course moja Ina components 3. Hivyo supplementary ni 90,000/- kwa course.

Vitabu vya walimu husika ni lazima wanafunzi kuvinunua kwa mzengwe wa kutosha. Photocopy za vitabu hivyo vinavyoruhusiwa kwenye mitihani ni batili.

Kuna pass mark 'dash'(-) zisizojulikana kwenye matokeo ya wanafunzi. Ambapo mtu mmoja katika course mbili, moja anaweza pata 'dash' kafaulu na nyingine akapata 'dash akawa kafeli.

Wanafunzi wawili pia somo hilo hilo, mmoja anaweza pata 'dash' kafaulu na mwingine 'dash' kafeli.

"Inawezekana namna gani?"

Malalamiko yako mengi yenye kuashiria fursa za rushwa za aina zote katika kujaribu kujinasua na vitanzi vya wazi vilivyopo chuoni hapo.

Ikumbukwe wanafunzi LST ni wahitimu wa shahada za kwanza, uzamili na hata uzamivu. Bila ya cheti Cha LST uhitimu wowote wa sheria ni kazi bure.

Kuna tuhuma za undugunization na ukabila. Kuna kujuana na connections. Katika wafanyakazi takribani 50 waliopo pale, wapo kadhaa wa kutokea familia moja (baba mmoja, mama mmoja) kama waajiriwa.

Wanafunzi wanaopata nafasi zaidi za kufaulu ni wale wenye unasaba na vigogo wa serikali wakiwamo mawaziri, majaji nk. Wenzangu na miye utakata rufaa katika mahakama ipi kwenye hali hii.

Chuo kimekuwa kama si taasisi ya serikali bali mali ya watu binafsi.

Kama kwa kufeli wanafunzi ni uhakikisho wa waendeshaji kujipatia mapato zaidi, watafaulu vipi wanafunzi kwa halali?

Kama walimu ni miungu watu kiasi hiki, ukimwi utakwisha kweli Tanzania hii?

"Hiki ni chuo cha umma, wenye dhamana hawawezi kuchagua kukaa kimya."

Bahati mbaya, ya namna hii si kwa LST peke yake.

Vimullikwe vyuo vyote vya elimu ya juu. Kutenganisha watunga mitihani, wasahihishaji na walimu wa course husika kuwa ni jambo la dharura sana.
Serikali iajiri wazungu wakiendeshe chuo hicho ili kuondoa malalamiko
 
Wanasheria sio watu wa kuonewa huruma ni fani ya kitapeli, iliyojaa rushwa, Dhuluma, hawana utu ni washenzi tupu, wanajikuta sana hao mende. Acha wakulane wenyewe kwa wenyewe.

Hao mende maeneo yao ya kazi na huduma zao ni miungu hao.

Wateseke zaidi na zaidi.
Umemaliza kazi vijana hao wanajiona mno wacha wapambne wenyewe kwa wenyewe
 
Taaluma ya kijambazi ambayo humnyang'anya haki mwenye haki kwa kutumia ujuzi wa kusema kwa kumhofisha mwenye haki.
Taaluma ya kumtetea mwizi ili aonekane hana hatia ili hali huyo mtetezi (wakili) akijua huyo anaemtetea kaiba kweli.
Taaluma ya uwakili haina hata chembe ya ubinadamu kutokana na tabia yake ya kupindisha ukweli hata kama huyo wakili analijua hilo cha msingi kwake ni kupata pesa tu.hawa jamaa sijui makanisani na misikitini huwa wanafuata nini
Hapana ndugu nyangindo, taaluma ya sheria na fani ya uwakili bado ina mchango mkubwa katika kutetea haki katika jamii.
Ni mambo mangapi unadhani watu wameweza kusingiziwa, kubambikiwa, kuhujumiwa na hata kudhulumiwa lakini waliweza kutetewa na hao hao mawakili.
Fani ya uwakili hujaribu kumtetea yeyote yule ambae anahitaji msaada. Sheria zipo wazi kazi ya kuitafsiri sheria hiyo ni mahakama wakili kazi yake ni kuielekeza mahakama katika kutafsiri kuliko bora kabisa na sahihi ki ujumla.
Je, wewe unadhani tukiwaondoa mawakili mifumo yetu ya mahakama iendeshwe kwa mfumo gani ambao utakuwa ailimia mia moja salama na kujitosheleza kiasi cha kwamba hakutahitajika wakili?
 
Mnataka kilaa mtu awe wakili kwa kulazimisha big result now ili mje muwaite mawakili wa mchongo...Ukifel law school soma postgraduate ya education ujikite na ualimu
 
Back
Top Bottom