Tuhuma za ufisadi zinazodaiwa kumpelekea Dkt. Ryoba kubwaga manyanga

Kufanya tendering ya vifaa kama hivyo wangekuwa wanaambatanisha quotations za bei za manufacturers, hata kama utafanya estimation ya retail price watajikuta wana base kwenye some percentages. Mfano, kama mzalishaji kaweka bei ya milioni 2, ni ngumu retail price kuwa milioni 6 (mara 3 ya bei ya kiwandani), labda inaweza kuwa mil. 2 na laki tano........hii inaweza kusaidia hata ambao wanaidhinisha kutoingizwa kwenye mkenge wa manunuzi yanayoonekana yana harufu ya ufisadi........
 
Ulitaka kusema nini? Hakuna ufisadi?
 
Mkuu umenena. Swala hapa ni Ryoba kuwajibika na ndio kanuni ya uwajibikaji; sasa anawajibika kizembe kwa mambo angeweza kuyazuia kwa kuchukua hatua mapema.
 
Hauzijui ama hauna uelewa wa ofisi za Umma hakuna sehemu wazembe na wajinga kama watendaji wa Umma. Haushangai Rais aliokota vichwa vya trein Bandarini! Ipo hivi hawa maboharia wanajua sana michezo hii especialy kwenye shirika kama TBC kurundika vitu na vikose wataalamu wa kuvitumia wala sio kitu kigeni. Nenda TBC taifa ndio utajua kuna mazuzu yamejaa pale. Japan wametoa equipments za maana sana lakini kuzitumia hakuna ujuzi.
 
Mkuu umenena. Swala hapa ni Ryoba kuwajibika na ndio kanuni ya uwajibikaji; sasa anawajibika kizembe kwa mambo angeweza kuyazuia kwa kuchukua hatua mapema.
Tena anawajubika kipuuzi sana. Huyu jamaa yupo very smart sijui hapa walimpita vipi?! Haiwezekani kitu cha Tshs. 1.74B kinapitishwa na kulipwa 1.72B kisha unataka Ayoub aendelee kukaa ofisini hapana. Lazima awajibike kwa kushindwa kusimamia shirika. Lakini sio kwa ufisadi. Rioba yupo pale halafu kawekewa msaidizi wake Bibi mmoja anaitwa Mama Swai Martha..sasa jaribu kuelewa fitina inayomtafuna. Mimi hainigii akili serious documents zenye huge amounts of money zinapita bila MD kuziona..kama alisinzia basi arudi UDSM akaendelee na chaki tu.
 
Du............... wakereketwa wamemwaga mboga!
Kazi kwako PM Majaliwa!

Kuna watu suruali leo hazitawatosha.
Huyo Mkurugenzi wa Manunuzi na Sattelite si mumtaje tu jina?
Tusije kunywa naye bia nasi tukadakwa!
πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…chawa kama chawa wote sukuma ndani
 
1. Mkurugenzi wa Manunuzi: Nestory Machumbe

2. Mkuu Kitengo Cha Satelite: Karim Chitenda.

au unataka na namba zao na picha kabisa?
Hapa mkuu umechafukwa hataree, maana huu umwagaji wa mboga ni wa mwendokasi tena SGR.
 
Kuna kampuni imeanza fanya kazi TBC since 1999, punguza chuki zisizo kusaidia moyoni mwako.
Kwani kampuni hata ikianza tangu 1970 mimi siwezi leo 2021 nikaweka mkono wangu hapo? Ongeza kufikiri mkuu.
 
Kuhusu ubora na mvuto wa TBC, ni bora ife kwanza kizaliwe kitu kingine ambacho kitakua huru bila kubanwabanwa na CCM, labda kitakua na ubora na mvuto. TBC imepoteza mvuto, hata wenye TBC hawaiangalii. Kodi zetu zinaliwa bure.
 
Macbook Pro 16" Laptop- Apple bei ya mtandaoni kwa sasa ni TZS 8,058,197.00. Kwenye orodha ya TBC ni TZS12 milioni na ushee! Na hiyo bei ya mwaka jana.
Kwenye tender hio ni kawaida labda kwa sababu hujawahi kufanya tendering sababu unatakiwa ulipe VAT 18% Sasa ukiweka original price utapata hasara
 
Hiki kitu kizito ulichomuangushia Evarist Chahali Mungu anakuona.
 
Duu! Hawa walimuweza kweli Mwendazake, walimsahaulisha kila kitu kwa kumpa live coverage ziara zote, barabara nzima! Wakawatangaza vibaya wapinzani na hata kuwabania taarifa zao zote muhimu huku wakimwimbia Mwendazake na ccm mapambio ya kila aina, kumbe nyuma ya pazia wanapiga chao!
Hakika uchunguzi kama huo na ufayike taasisi zote sio hapo tu usikute hata ATCL kukawa na upigaji wa kutisha!
 
Magu amefanya yake wacha apumzike ni raisi bora kabisa kutokea hapa Tanzania,upende usipende ndivyo hivyo, mnaojaribu kumchafua mnajidanganya bure kama akina february Marope na genge lake.
Hajawahi kuwa bora alikuwa rais wa ovyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…