Tuhuma za ufisadi zinazodaiwa kumpelekea Dkt. Ryoba kubwaga manyanga

BAADHI YA TUHUMA ZINAZODAIWA KUMPELEKEA DR. AYUBU RYOBA KUJIUZULU
  • Yeye binafsi hana tuhuma za moja kwa moja, anawajibika kwa matumizi mabaya ya ofisi yaliyofanywa na wasaidizi wake.
  • Wasaidizi hao kwa uchache ni Mkurugenzi wa Manunuzi na Mkuu wa Sattelite.
  • Tayari baadhi yao wamekuwa wakihojiwa na TAKUKURU.
  • Makampuni Zaidi ya matatu yamekuwa yakihusika katika kupata zabuni bila kufuata sheria.
  • Na Kampuni hizo zimekuwa zikiweka bei hadi mara tatu ya bei halisi za sokoni.
  • Kampuni hizo moja wapo ni ONSET ENGINEERING (ISRAEL), ENERGY & TELECOM (TANZANIA), JEMO INVESTMENT & GENERAL ENTERPRISES (TANZANIA).
  • Ipo miradi mingi imetekelezwa kwa mabilioni ya pesa za walipa kodi nab ado haifanyi kazi, nitajaribu kuelezea michache.
  • Pia Channel ya SAFARI imekubwa na matumizi mabaya ya pesa, yaani UFISADI.
Sote tunafahamu tetesi zilizosambaa juzi kati kuwa Mkurugenzi wa TBC, Dr. Ayubu Chacha Ryoba amejiuzulu. Ni kweli alijiuzulu na kuchukua likizo ya muda mfupi.

Sababu ya kujiuzulu ni kuwajibika kwa matumizi mabaya ya ofisi ambayo yamekuwa yakifanywa hasa na wasaidizi wake, wakiongozwa na Mkurugenzi wa Manunuzi, na Mkuu wa Sattelite. Wawili hawa wamekuwa wakishirikiana na kampuni za ndani na nje katika kuibua miradi na kulipa mabilioni ya pesa huko ubora wa TBC ukiwa hauboreki licha ya serikali kuwapa mabilioni kila mwaka.

KUHOJIWA NA TAKUKURU
Baada ya Taarifa kumfikia Waziri Mkuu, Mh. Majaliwa K. Majaliwa aliagiza TAKUKURU kufanya uchunguzi katika baadhi ya Tuhuma walizopelekewa na katika baadhi ya miradi iliyotekelezwa na kampuni tatu: ONSET ENGINEERING (ISRAEL), ENERGY & TELECOM (TANZANIA), JEMO INVESTMENT & GENERAL ENTERPRISES (TANZANIA).

Katika mahojiano hayo kuna mambo kadhaa wameyabaini na bado wanaendelea kuyachunguza, nitajaribu kugusua hizi kampuni zao na uhusika wake kwa ufupi.

ONSET ENGINEERING (ISRAEL), ENERGY & TELECOM (TANZANIA)
Hizi ni kampuni pacha zinazoshirikiana katika kufanya kazi za kinyume na sheria TBC. Sheria ya manunuzi ya umma inakataza kampuni ambayo imeshiriki kuandaa tender nayo kuwa sehemu ya kuomba tender.

Ambacho wamekuwa wanafanya ni kuwa; TBC wakitaka kutekeleza mradi wanamuomba ONSET ENGINEERING kutoa pendekezo la mradi, huyu ONSET anatoa vifaa na bajeti ya huo mradi, tender ikitangazwa haombi kupitia ONSET bali anaomba kupitia washirikia wake wanaoitwa ENERGY & TELECOM na wanaweka bei kubwa sababu tayari wanakuwa wameficha Technical Specifications za vifaa, hivyo waombaji wengine hata wakiwa na bei chini wanaambiwa wameshindwa kwenye Technical Specifications na mwisho wa siku mradi unaoweza kutekelezwa kwa bilioni moja kwa uhalisia wa bei ya soko unaweza kutekelezwa kwa bilioni 2 hadi 3. Na wahusika wananyamaza sababu wanafaidika. Na huyu ONSET amekuwa akifanya miradi ya TBC toka mwaka 1999. Hivyo kwa kuongezea TAKUKURU ichunguze miradi yake yote na bei ambazo amekuwa akilipwa.

WAMEKUWA WAKILIPWA KABLA YA UTEJELEZAJI WA MIRADI
Nitaweka mfano wa mradi mmoja kati ya mingi, hii kampuni ilipewa mradi wa kutengeneza Community Radio Jijini Dodoma kwa gharama ya 1.74 bilioni, kabla ya kutekeleza tayari TBC ikawalipa 1.72B Ikabaki just 20,000,000. Mradi huu ulikuwa uzinduliwe na Hayati Magufuli May 2020, lakini ulisuasua kwa muda mrefu huku Muisrael na washirika wake wa Tanzania wakisingizia Corona.

Community Radio haiwezi kugharimu 1.74 Bilioni kama hakuna upigaji kwa bei za kawaida. Zaidi ya yote ilikuwaje walipwe kabla ya utekelezaji kinyume na sheria za manunuzi ya Umma? Nafikiri TAKUKURU wamekwisha ifanyia kazi na wana majibu Zaidi.

NB: Muhimu miradi yote chini ya hawa watu ichunguzwe na watendaji wanaowajibika wote wawajibishwe.

JEMO INVESTMENT & GENERAL ENTERPRISES LTD
Hii kampuni ni kampuni inayoendeshwa kijanja kijanja, nafikiri wengi mnajua hizi kampuni zinazojiita General Enterprise, kwamba wao kila kitu wana supply, na kuna wakati serikali ilizipiga marufuku.

Kwanza hii kampuni sio ya kitaalamu katika kufanya supply ya mambo ya Broadcasting, haina wataalamu, workshop wala ofisi nzuri, ana stationery ambayo anasema ndio ofisi yake.

Hii kampuni imeingizwa kiujanja na Mkurugenzi wa Manunuzi TBC na Mkuu wa Sattelite, ambaye ndio amekuwa kama mmiliki wa hii kampuni.

Moja ya kashifa yake kubwa ni kupewa mradi wa Tender Na: PA/084/2019-2020/G/33 (attached their delivery note).

Mradi huu ulikuwa unahusisha Supply, Installation, Training and Commisioning of Studio Equipments wenye thamani ya 855,000,000.

Kampuni hii haikuwa ma mtaji, hivyo Mkurugenzi wa Manunuzi akawalazimisha watendaji wake wa chini kusaini nyaraka kuonyesha huyu Jemo tayari kafanya supply, kafanya installation na kafanya training hivyo anastahili kulipwa.

Mkurugenzi wa manunuzi akahakikisha Jemo analipwa pesa 100% ndipo akaenda kunua vifaa hivyo. Sasa baada ya kununua sababu hana utaalamu na hana wataalamu alienda akavibwaga TBC bila installation na training na hadi leo baadhi ya vifaa viko stoo havifanyi kazi iliyokusudiwa ila wao tayari maisha yao yanaenda kwa kuchezea pesa za walipa kodi.

Lakini Zaidi ni kinyume cha sheria ya manunuzi kumpa mzabuni pesa ndio akanunulie vifaa. Huyu Jemo hadi leo mtaji wake aliosajiri Brela unaonyesha kuwa ana mtaji wa milioni 5 toka alipoanzisha kampuni mwaka 2013, ina maana mtaji wake haukui wala hafanyi annual retirement na msajiri wa makampuni brela.

UFISADI SAFARI CHANNEL
Uchunguzi pia umebaini kuwa katika hii Safari Channel kuna ufisadi mkubwa sana na unamgusa moja kwa moja Mkurugenzi wa Manunuzi na Msimamizi wa Hii Channel.

HITIMISHO
Mabilioni ya pesa ambayo TBC inatumia kila mwaka hayaendani na ubora wa picha wala maudhui, kuna miradi mingi sana pale wanaiita White Elephants Project. Ni kweli Dr. Ayubu Ryoba sio mtu corrupt lakini ameshindwa kabisa kujua kuwa watendaji walio chini yake wanamzunguka na kufanya vitendo vya kifisadi.

Hivyo kama anawajibika awajibike lakini hawa watendaji wanaohujumu Shirika pindi TAKUKURU wakikamilisha Uchunguzi wao basi wapelekwe mahakamani.

View attachment 2015188
View attachment 2015189
JF imeanza kurudi katika ubora wake
 
Mkurugenzi wa satellite alafu hata kwenye dish ya futi 6. C band tbc haipatikani upuuzi mwingi sana. Wanashindwa hata na Itv
 
Ayoub Ryoba Acha avune alichopanda,maana alizidisha uchawa.
 
Kwamba accounting officer hajui hizo bei za kifisadi wakati ndio anaidhinisha malipo?
 
Vitu nilivyogundua ni kwanza matatizo ya TBC tunayoona kwenye TV chanzo chake ni utawala wa shirika,pili huu waraka una agenda ya kumsafisha Ayubu Ryoba
Hasafishiki. Nimesema mahala humu kwamba huenda waraka huu umeandikwa na Ryoba mwenyewe ili kujisafisha lakini ni mambo ya kitoto sana
 
Amejiuzulu lini wakati naona post ya tbc wameweka tangazo jana anasimamia kipindi?
Screenshot_20211118-193752_Instagram.jpg
 
JF imerudi kwenye ubora wake
Kama Ni kweli basi tbc hali Ni mbaya
 
Kwani TBC (Tazama Blaablaa za Ccm) bado ipo? Inaoneshaga nini kwasasa?
Wengine tulihamiaga Azam (burudani kwawote) na kina mzee Tido,Chalz Hilary etc. sikumingi...
huku Azam tunajifunza na kuenjoy vitu vya kiuweledi...sio vyaki coward
 
Duh! Kweli nchi yetu inaliwa sana na watu tulio wapa dhamana ya kusimamia mambo
Yaani utasikia
Tanesco upigaji..
TBC Upigaji
Elimu upigaji
Afya upigaji
Vyuo upigaji
Enyi viongozi waoneeni huruma wananchi ,inchi inachelewa mmuno kuendelea.
 
BAADHI YA TUHUMA ZINAZODAIWA KUMPELEKEA DR. AYUBU RYOBA KUJIUZULU
  • Yeye binafsi hana tuhuma za moja kwa moja, anawajibika kwa matumizi mabaya ya ofisi yaliyofanywa na wasaidizi wake.
  • Wasaidizi hao kwa uchache ni Mkurugenzi wa Manunuzi na Mkuu wa Sattelite.
  • Tayari baadhi yao wamekuwa wakihojiwa na TAKUKURU.
  • Makampuni Zaidi ya matatu yamekuwa yakihusika katika kupata zabuni bila kufuata sheria.
  • Na Kampuni hizo zimekuwa zikiweka bei hadi mara tatu ya bei halisi za sokoni.
  • Kampuni hizo moja wapo ni ONSET ENGINEERING (ISRAEL), ENERGY & TELECOM (TANZANIA), JEMO INVESTMENT & GENERAL ENTERPRISES (TANZANIA).
  • Ipo miradi mingi imetekelezwa kwa mabilioni ya pesa za walipa kodi nab ado haifanyi kazi, nitajaribu kuelezea michache.
  • Pia Channel ya SAFARI imekubwa na matumizi mabaya ya pesa, yaani UFISADI.
Sote tunafahamu tetesi zilizosambaa juzi kati kuwa Mkurugenzi wa TBC, Dr. Ayubu Chacha Ryoba amejiuzulu. Ni kweli alijiuzulu na kuchukua likizo ya muda mfupi.

Sababu ya kujiuzulu ni kuwajibika kwa matumizi mabaya ya ofisi ambayo yamekuwa yakifanywa hasa na wasaidizi wake, wakiongozwa na Mkurugenzi wa Manunuzi, na Mkuu wa Sattelite. Wawili hawa wamekuwa wakishirikiana na kampuni za ndani na nje katika kuibua miradi na kulipa mabilioni ya pesa huko ubora wa TBC ukiwa hauboreki licha ya serikali kuwapa mabilioni kila mwaka.

KUHOJIWA NA TAKUKURU
Baada ya Taarifa kumfikia Waziri Mkuu, Mh. Majaliwa K. Majaliwa aliagiza TAKUKURU kufanya uchunguzi katika baadhi ya Tuhuma walizopelekewa na katika baadhi ya miradi iliyotekelezwa na kampuni tatu: ONSET ENGINEERING (ISRAEL), ENERGY & TELECOM (TANZANIA), JEMO INVESTMENT & GENERAL ENTERPRISES (TANZANIA).

Katika mahojiano hayo kuna mambo kadhaa wameyabaini na bado wanaendelea kuyachunguza, nitajaribu kugusua hizi kampuni zao na uhusika wake kwa ufupi.

ONSET ENGINEERING (ISRAEL), ENERGY & TELECOM (TANZANIA)
Hizi ni kampuni pacha zinazoshirikiana katika kufanya kazi za kinyume na sheria TBC. Sheria ya manunuzi ya umma inakataza kampuni ambayo imeshiriki kuandaa tender nayo kuwa sehemu ya kuomba tender.

Ambacho wamekuwa wanafanya ni kuwa; TBC wakitaka kutekeleza mradi wanamuomba ONSET ENGINEERING kutoa pendekezo la mradi, huyu ONSET anatoa vifaa na bajeti ya huo mradi, tender ikitangazwa haombi kupitia ONSET bali anaomba kupitia washirikia wake wanaoitwa ENERGY & TELECOM na wanaweka bei kubwa sababu tayari wanakuwa wameficha Technical Specifications za vifaa, hivyo waombaji wengine hata wakiwa na bei chini wanaambiwa wameshindwa kwenye Technical Specifications na mwisho wa siku mradi unaoweza kutekelezwa kwa bilioni moja kwa uhalisia wa bei ya soko unaweza kutekelezwa kwa bilioni 2 hadi 3. Na wahusika wananyamaza sababu wanafaidika. Na huyu ONSET amekuwa akifanya miradi ya TBC toka mwaka 1999. Hivyo kwa kuongezea TAKUKURU ichunguze miradi yake yote na bei ambazo amekuwa akilipwa.

WAMEKUWA WAKILIPWA KABLA YA UTEJELEZAJI WA MIRADI
Nitaweka mfano wa mradi mmoja kati ya mingi, hii kampuni ilipewa mradi wa kutengeneza Community Radio Jijini Dodoma kwa gharama ya 1.74 bilioni, kabla ya kutekeleza tayari TBC ikawalipa 1.72B Ikabaki just 20,000,000. Mradi huu ulikuwa uzinduliwe na Hayati Magufuli May 2020, lakini ulisuasua kwa muda mrefu huku Muisrael na washirika wake wa Tanzania wakisingizia Corona.

Community Radio haiwezi kugharimu 1.74 Bilioni kama hakuna upigaji kwa bei za kawaida. Zaidi ya yote ilikuwaje walipwe kabla ya utekelezaji kinyume na sheria za manunuzi ya Umma? Nafikiri TAKUKURU wamekwisha ifanyia kazi na wana majibu Zaidi.

NB: Muhimu miradi yote chini ya hawa watu ichunguzwe na watendaji wanaowajibika wote wawajibishwe.

JEMO INVESTMENT & GENERAL ENTERPRISES LTD
Hii kampuni ni kampuni inayoendeshwa kijanja kijanja, nafikiri wengi mnajua hizi kampuni zinazojiita General Enterprise, kwamba wao kila kitu wana supply, na kuna wakati serikali ilizipiga marufuku.

Kwanza hii kampuni sio ya kitaalamu katika kufanya supply ya mambo ya Broadcasting, haina wataalamu, workshop wala ofisi nzuri, ana stationery ambayo anasema ndio ofisi yake.

Hii kampuni imeingizwa kiujanja na Mkurugenzi wa Manunuzi TBC na Mkuu wa Sattelite, ambaye ndio amekuwa kama mmiliki wa hii kampuni.

Moja ya kashifa yake kubwa ni kupewa mradi wa Tender Na: PA/084/2019-2020/G/33 (attached their delivery note).

Mradi huu ulikuwa unahusisha Supply, Installation, Training and Commisioning of Studio Equipments wenye thamani ya 855,000,000.

Kampuni hii haikuwa ma mtaji, hivyo Mkurugenzi wa Manunuzi akawalazimisha watendaji wake wa chini kusaini nyaraka kuonyesha huyu Jemo tayari kafanya supply, kafanya installation na kafanya training hivyo anastahili kulipwa.

Mkurugenzi wa manunuzi akahakikisha Jemo analipwa pesa 100% ndipo akaenda kunua vifaa hivyo. Sasa baada ya kununua sababu hana utaalamu na hana wataalamu alienda akavibwaga TBC bila installation na training na hadi leo baadhi ya vifaa viko stoo havifanyi kazi iliyokusudiwa ila wao tayari maisha yao yanaenda kwa kuchezea pesa za walipa kodi.

Lakini Zaidi ni kinyume cha sheria ya manunuzi kumpa mzabuni pesa ndio akanunulie vifaa. Huyu Jemo hadi leo mtaji wake aliosajiri Brela unaonyesha kuwa ana mtaji wa milioni 5 toka alipoanzisha kampuni mwaka 2013, ina maana mtaji wake haukui wala hafanyi annual retirement na msajiri wa makampuni brela.

UFISADI SAFARI CHANNEL
Uchunguzi pia umebaini kuwa katika hii Safari Channel kuna ufisadi mkubwa sana na unamgusa moja kwa moja Mkurugenzi wa Manunuzi na Msimamizi wa Hii Channel.

HITIMISHO
Mabilioni ya pesa ambayo TBC inatumia kila mwaka hayaendani na ubora wa picha wala maudhui, kuna miradi mingi sana pale wanaiita White Elephants Project. Ni kweli Dr. Ayubu Ryoba sio mtu corrupt lakini ameshindwa kabisa kujua kuwa watendaji walio chini yake wanamzunguka na kufanya vitendo vya kifisadi.

Hivyo kama anawajibika awajibike lakini hawa watendaji wanaohujumu Shirika pindi TAKUKURU wakikamilisha Uchunguzi wao basi wapelekwe mahakamani.

View attachment 2015188
View attachment 2015189
Da jamaa hata woga hawana,hizi bei karibu ni mara 2 au 3 ya bei halisi yaani wame hike kinoma na sijui walikuwa wananunua wapi hivi vifaa ,kama ni hapa nchini receipts za EFD zimetolewa kwa hizo bei?
 
... waliwezaje kufanya ufisadi wote huo kipindi cha "asiyejaribiwa; alfa na omega"? Kipindi ambacho iliaminika ni Tanzania pekee ambapo dhambi ya rushwa/ufisadi haikuwahi kufanyika chini ya Mbingu? Kwamba Bwana Mungu "akichungulia" kutokea Kiti cha Enzi ni Tanzania pekee ambapo hakuiona dhambi ya rushwa?
Mkuu naona hujui kusoma kuna kampuni imekuwa ikila shavu hapo kuanzia 1999 na je miaka hiyo mwendazake ndie alikuwa mwenye kigoda?chuki za nini? mbona wengine huwasemi,ubazazi wa tender haujaanza tu kipindi cha juzi wanange na wengine basi kama umekuwa mkweli, huwajui wala rushwa wa TZ ambao hata mtoto wa juzi anawajua.
 
Back
Top Bottom