Tuhuma za Ukabila: Wasukuma si Miongoni mwa Makabila yenye Ukabila, tatizo ndio walio wengi!

Swali zuri sana,ubarikiwe.
 
Sijasoma maelezo yako marefu ambayo naamini yamejaa pumba, lakini hivi ni kweli huuoni huo ukabila anaofanya huyo rais wenu wa sasa ?, acha basi kujitoa akili Paskali umekuwa mtu mzima sasa, kukaa kimya nako ni busara pia, wasukuma ndio mabingwa wa ukabila zaidi hata ya wahaya ambao tuliaminishwa siku za nyuma, kama Taifa tumepoteza sana kuweka nchi yetu mikononi mwa huyu mtu,
Paskali,
Hivi hukusikia siku ile rais wenu alipotamka hadharani kwamba wakazi wa barabara ya airport mwanza hawatakiwi kuvunjiwa nyumba zao (pamoja na kawamba zimejengwa kwenye hifadhi ya barabara) kwa sababu tu ni wasukuma waliompa kura, wakati huo watanzania wengine wakiwa wamevunjiwa nyumba zao !!
 
Hatari Sana. Ukiona MTU mwenye Akili timamu anazungumza habari za makabila muogope kama ukoma. Sorry unajishushia adhi Bora ungekaa kimya. Ni serikali hii wasukuma ndio wengi au ni serikali hii imegunduwa wasukuma ndio wengi. Aibu aibu Sana. Hata wanao kujuwa naiman wanashangaa.
 
Usione kimya na vigelegele ukafikiri watanzania ni wapumbavu kiasi hiko. Time will tell Sali Sana kuwe na kifungu chaku delete haya ma ukabila yako huku mtandaoni.
 
Niliishi shinyanga miaka ya zamani kulikuwepo na kamsemo "Ng'wanambate" kule shirecu bila kuwa msukuma unayejulikana hupati kazi. Jamaa yangu mhaya alifukuzwa uweka hazina wa wilaya ya shinyanga kwa tuhuma za kubumba madiwani "wakamuazimia" mojawapo ya maneno yaliyosemwa kwenye kikao cha full council ni " huyu aende halmashauri za kwao". Haya yote magufuli anayofanya yanathibitisha mengine na zaidi!
 
Kipindi cha zamani niliishi na wasukuma sana yan kama ni mgeni watakukirimu sana nilipenda maisha Yale kwa kweli,ila kwa sasa hiv wanasema wamebadilika au kwa kuwa niliokuwa naishi nao hawakuwa wasomi auhawa wasomi ndo wenye huo ukabila mmh,Ila kama ni kweli athari zitajionyesha muda mfupi tu ujao
 
Nataka nisikie Paskali akikanusha kuhusu iliyokuwa shirecu enzi hizo, uzuri ni kwamba kutokana na ukabila wa kishamba uliokuwepo pale shirecu wa kutotaka mawazo ya watu wengine mwisho wa siku waliyaua mashirika na viwanda vyote, ukianzia kule chato ambako huyu raisi wa sasa ndio waliokuwa wamejazana pale, lakini pia zipo jineri nyingine nyingi zilizokufa kwenye mikono ya ukabila
 
Huyu Rais ana siri kubwa moyoni. akipata nafasi atawamaliza kabila moja analolichukia hata kwa mass massacre haoni shida. Silihitaji hilo kabila itoshe kusema huyu anatupeleka shimoni"
 
Huyu Rais ana siri kubwa moyoni. akipata nafasi atawamaliza kabila moja analolichukia hata kwa mass massacre haoni shida. Silihitaji hilo kabila itoshe kusema huyu anatupeleka shimoni"
So unataka kusema huyu rais anaweza kufanya mauaji ya maangamizi ?, mass killing.
 
Sitashangaa kusikia next President ni msukuma tena!!.
Maadam kwenye uchaguzi wa rais wa Tanzania, hatuchagui kabila ya mtu, bali tunamchagua mtu mwenye sifa na vigezo, ikitokea mwaka 2020, mtu mwenye sifa na vigezo ni Msukuma, tutamchagua!. Hatutamchagua kwa Usukumani wake, bali kwa sifa na vigezo vyake.

Hili Mwalimu Nyerere amelifafanua vizuri sana, kama "mtu hana sifa, hatutamchagua kwasababu ni kabila langu", au mtu ana sifa zote, hatukataa kumchagua kwasababu ya kabila lake!", kumchagua mtu kwasababu ya kabila lake ni ubaguzi, na kumkataa mtu kwasababu ya kabila lake pia ni ubaguzi!, ikitokea kwa sasa wenye sifa ya urais ni Wasukuma tuu, let it be!.
P
 
Mkuu Coaster2015 , naomba nisijibu specific case ya SHIRECU, lakini lets be realistic, enzi zile za kuanzishwa vyama vya ushirika, kila chama kilikuwa dominated na watu wa eneo husika, KNCU, walikuwa Wachagga, NCU, na Shirecu, Wasukuma, Bukop, Wahaya, etc, sina uhakika kama watu wa makabila mengine walikuwa wanabaguliwa. Ukabila mbaya ni pale wewe ukiwa Top Boss, unaajiri watu wa kabila lako tuu!. Fanya utafiti wa ma mashirika yenye ma Top Boss Wasukuma, angalia idadi ya Wasukuma kwenye shirika hilo, compared to kama top boss ni Mchagga au Mhaya!.

Enzi zile, kuna Mhaya mmoja alikuwa Top, shirika fulani, amini usiamini, Kihaya ndio kilikuwa lugha ya ofisi, kuanzia walinzi, wafagiaji, wahudumu, ma masanja, madereva, ma secretary, wote ni kabila moja, na walikuwa very proud kuzungumza Kihaya ofisini, kuna ofisi yoyote ya umma umewahi kwenda ukakuta Wasukuma wanazungumza Kisukuma hapa jijini Dar or Dodoma?.

Sio wengi wamejibu hoja za msingi za bandiko hili, ikitokea wewe ni Mkuu wa nchi, kuna nafasi ya uteuzi, akatokea mtu wa kabila lako ana sifa ya uteuzi, utaogopa kumteua kwasababu watu watasema ni ukabila?.

Acheni hizo!.

P
 
Mbona hujajibu hoja ya rais kuagiza kusitishwa kwa bomoabomoa pale barabara ya airport mwanza ??, swali hilo lilikuwa kipimo kwako
Paskali uwezo wako wa kujenga hoja unaporomoka kadri siku zinavyokwenda mbele, natamani ungelibaini tatizo linalokutafuna ili ujirekebishe,
kama unathubutu kukwepa kukubali jinsi ambavyo pale shirecu walikuwa hawaongei kisukuma na kuajiri wasukuma peke yao basi utakuwa una shida kubwa sana, pale shirecu alikuwa hawezi kuajiriwa mtu asiye msukuma, sijasimuliwa nafahamu kwa sababu mimi nimeshi pale, na kusema kwamba vyama vya ushirika vilitengwa maalumu kwa ajili wakazi wa maeneo husika ni ujinga, aliye anzisha hakuwa na lengo hilo, na ndio maana viwanda vyote vya usukumani vilikufa ilhali malighafi (pamba) ikiwa bado inapatikana kwa wingi hapahapa nchini kwa sababu ya ushamba na undugunaizesheni, kuhusu ukuu wa nchi kwa kweli tutamkumbuka sana Kikwete, sio kweli kwamba hao wote aliowateua rais wenu huyu wanaotoka kanda ya ziwa wana sifa, wengi kama sio wote ni watu wa hovyohovyo sana, anzia IGP, Jaji Mkuu, Mwendesha mashitaka mkuu Fereshi (kumbuka huyu alifukuzwa kazi na Kikwete kwa utendaji mbovu), akina Kalemani, Doto Biteko, (kwangu mimi hili ndilo baraza la mawaziri la hovyo kuwa kutokea) na ndio maana amekuwa akiwafukuza muda mfupi baada ya kuwateua (kumbuka yule mbunge Kitwanga), watu makini kama akina January Makamba, Makame Mbalawa hawakuwekwa kwenye kundi kwa sababu tu sio wasukuma,
Paskali, kuna watu wengi sana makini kwenye nchi wangeweza kushika nafasi za uongozi na Taifa likaona manufaa yao, lakini bahati mbaya ukabila na ubaguzi wa kikabila na kikanda unapelekea kuteua watu wa hovyo kama Luhaga Mpina, Kigwangala eti kuwa mawaziri, umeona walichokifanya mwa kipindi cha miaka mitano ??, inaweza kuwasaidia sana mkifuata mfumo aliotumia Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere.
 
Kila kitu ni Shatto
 
DPP, IGP, CDF, AG, Pay master, wote hawa wanatoka wapi?
 
Vyama vya ushirika vilikuwa maalum kwa wakazi husika. Ukiniambia Januari Makamba yuko Makini kwa kipi hasa umempima ? Mbona wakati wachagga wamejazana CRDB na TRA hukuleta bandiko kama hili ? Huo ni wivu tu unawasumbua kwa sababu mlizoea kupendelewa hata kama hamna vigezo. Tulieni kila kitu na wakati wake na kumbuka kanda ya Ziwa ina 1/3 ya watanzania wote. Miaka ya nyuma kanda hii ilinyanyasika sana. Sasa hivi zimwi lililolala limeamka ! Muwe wapole tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…