John Haramba
JF-Expert Member
- Feb 4, 2022
- 365
- 1,374
Ukifuatilia mitandaoni kwa sasa watu wa soka kuna kelele fulani hivi zimekuwa zikiendelea kwa kasi, ilianza kimya kimya, lakini taratibu zinaenda zinashika kasi.
Timu fulani kubebwa au timu hii inatengenezewa mazingira ya ubingwa ni maneno ambayo yanasikika sana mtaani na mitandaoni.
Awali, moja kati ya wadhamini wa Yanga walikuwa wakitajwatajwa kuwa wanahusika katika kupitia mlango wa nyuma kutengeneza mazingira ya timu yao kushinda. Hakuna aliyejitokeza hadharani kulizungumzia hilo kama ni kweli au la.
Baada ya mchezo wa Simba dhidi ya Tanzania Prisons, jana, Haji Manara akaposti picha ya refa wa mchezo huo na kuandika: Vp GSM anahusika au? Caption haina uhusiano na Picha ya juu, huwa napenda tu kuwapost Waungwana Marefarii wetu 🤪.”
Kwa tafsiri ya kawadia ni kuwa anamaanisha wale waliokuwa wakidai wao wanashinda kwa mkono wa GSM wana maoni gani kwa ushindi wa Simba hasa kwa refa wa mchezo husika.
Upande wa pili, Ahmed Ally naye akaweka post akidai kuwa kuna waamuzi wanne msimu huu wamefungiwa au kupewa adhabu katika michezo ambayo maamuzi yao yalionekana kuwabeba Yanga.
Kuna mifano mingi lakini hiyo ndiyo ya karibu.
Hoja yangu ni kuwa inamaana hiki kinachoendelea kwa sasa ni ununuaji wa mechi au ununuaji wa ubingwa? Hata kama ni utani, utani gani wa kuambiana kuwa kuna mazingira ya rushwa.
TFF na Bodi ya Ligi wapo kimya, wanasubiri mambo yawe mabaya ndiyo watoe tamko au wachukue hatua?
Ni kweli kuna timu au kuna watu wananunua mechi? Wanawahonga waamuzi au waamuzi wanafanya makosa kwa kuwa uwezo wao ni mdogo? Kitendo cha Manara na Ahmed Ally kutoa kauli tata kama hizo inamaanisha wanajua michezo michafu wanayofanya pande zote au ni nini kinaendelea?
Kuna kitu hapo hakipo sawa, TFF waamke kabla hali haijawa mbaya.