Inawezekana una hoja nzuri yenye mashiko. Punguza jazba kidogo, kisha kwa utulivu andika hoja yako ama zako kuhusiana na unavyoelewa ama unavyoamini juu ya tukio hili baya Sana.
Kwa mfano:
1.Kuna wanaodhani serikali imehusika, kwasababu ya Mh.Lisu kuipa changamoto kubwa.
2.Wapo wanaodhani, kuna baadhi ya watu wasiofurahishwa na utendaji wa serikali, mathalani tumbuatumbua inayoendelea. Hivyo, wameamua kumfitinisha Mh.Rais kwa wananchi kwa namna yoyote ikiwamo kama hii pamoja na nyingine.
3.Wapo wanaodhani, huenda ni inside job. Yaani baadhi ya wanachama wa CHADEMA wametishwa na umaarufu pamoja na Courage ya Mh. Lisu na kwamba anatishia nafasi zao hivyo kuazimia kumuondoa.
4.Mh.Lisu ni wakili mahiri, anajihusisha na kesi nyingi. Huenda katika utendaji kazi wake wakatokea watu walioumizwa hivyo kuazimia kulipiza kisasi. Na kwakuwa tayari watu hao wanajua the prime suspect itakuwa serikali, huenda ikawa rahisi wao kutekeleza azma yao.
Hayo ni kwa uchache, na kutokana na mkanganyiko huo, ndiyo sababu y'all busara kutuelekeza kusubiri taarifa ya vyombo vya ulinzi na usalama. Baada ya taarifa kutoka ndipo tutakuwa kwenye nafasi nzuri kukosoa na hata kuchukua hatua zaidi pale tutakapokuwa hatujaridhika.
Kuhukumu upande mmoja kunasaidia kupoteza mhalifu wa kweli pale inapokuwa anayetuhumiwa si mhusika wa tukio. Mbaya zaidi mhusika halisi atakapoptikana huenda akatetewa kwasababu tayari focus imekuwa kwa aliyetuhumiwa awali.
Kama Serikali/jeshi la polisi haliaminiki basi mwenye tuhuma zenye uthibitisho aziweke hadharani ili uma uone. Tusiongee kwa hisia tu ama kwa kuconnect dots. Hata wahalifu wengine wanaweza tumia nafasi ya hisia ama kuconect dots kama kichaka cha kutekeleza uhalifu wao wakijua wazi kuwa, kwa hisia na kuconect dots ni serikali itakayohusishwa.
Tuwe watulivu tukisubiri taarifa ya jeshi la polisi. Na pia kwa wenye uwezo wafanye uchunguzi binafsi ili taarifa wanazoleta ziwe na ushahidi.
Sent using
Jamii Forums mobile app