Kinachonishangaza Wagner Group wakienda mahali penye wanajeshi wa NATO, nato wanaanza Kulalamika alafu wanaondoka.
Nato wanawaita Wagner group kwa jina la (mamluki wa Putin) [emoji1787][emoji1787]
Mfano pale Syria, Venezuela, Afrika ya Kati, Burkina Faso, Mali, Mozambique, Na Sasa Congo na Ukraine.
NATO walipanga mpaka mwishoni mwa mwaka huu ulioisha eneo kubwa la Afrika liwe halitawaliki ili waje kwa kisingizio cha kulinda amani kumbe wanachota rasilimali za chini ya ardhi pamoja na viungo vya wanadamu.
Kitovu cha uhalifu kwa Afrika Mashariki kilipangwa kiwe eneo la Mocimboa da Praia nchini Mozambique alafu uhalifu huo ungesambazwa kwa kasi maeneo ya Mtwara kuja hadi Lindi, pwani yote ya Afrika Mashariki huku zana nzito zikishushwa Rwanda kwa kipenzi chao Kagame.
Huko Mali, Afrika ya Kati, na Burkina Faso hawa NATO walikuwa wanamtumia Mfaransa na Uingereza kutumia nguvu kubwa kusambaza makundi ya kigaidi na silaha sema bahati nzuri kuna baadhi ya mapinduzi yakawaleta vijana wanaojua michezo ya NATO ndio maana wakaomba kimyakimya usaidizi kutoka Urusi, Urusi wakapeleka wanajeshi wachache wa Wagner group.
Hata Congo Wagner group wameshaingia ndio maana unaona ufalme wa Magharibi/NATO ukilegalega juu ya yale malengo yao.
Kila wakati wanamuuliza rais wa Congo kuhusu ushirika wake na Wagner group lakini rais wa Congo anakataa.
Nakumbuka mwaka 2020 Uingereza alipanga kupeleka kikosi pale Zambia mpakani na Tanzania akishirikiana na baadhi ya mataifa mengine ya NATO, ila ilipofika muda ambao wanataka kuleta kikosi wakakuta tayari Wagner group wapo kwenye misitu ya Zambia tayari. Na tangu Wagner group wameingia Zambia, ule uhalifu wa kukata watu vichwa kwa makundi kijiji hadi kijiji umeishia. Pia media za magharibi zimebaki kulalamika sehemu zote za dunia tofauti na kipindi cha nyuma walikuwa kazi yao ni kuripoti kuhusu ugaidi na kutabiri kuhusu ugaidi.
NATO wapumbavu sana wanataka sehemu kubwa ya dunia iingie kwenye mchakamchaka wa machafuko alafu wao waendelee kuchota rasilimali na kujiimarisha ili kukija kutulia wawe na nguvu ya kulazimisha sera zao za ushoga na ufeminist kwa nguvu.