Tuifahamu Wagner Group kwa undani

Tuifahamu Wagner Group kwa undani

Hili kundi binafsi la ulinzi Wagner linapatikana wap, yaan makao yao hasa ni wap

Ni kwa nin Putin kaamua kuwatumia wao? Ni kwamba jeshi lake ni goigoi kuliko hawa Wagner au ikoje hii wakuu.

Nauliza kwa kutaka kujua siyo ushabiki
Mmarekani kawatumia sana blackwater huko mashariki ya kati....hao ni contractors, kampuni inachukua tenda ya kijeshi kwa niaba ya serikali au kikundi fulani....ilimradi uwalipe vizuri tu na waendane na falsafa zako...........dunia imeshatoka kwenye vita za kama wa vietnam enzi hizo....vita ni biashara
 
Nachojua n kikundi binafsi Cha ulinzi Kutoka Russia

Kinapokea oda yoyote toka kwa mtu yeyote kikubwa pesa yako tu wanatoa ulinzi wa mtu mmoja mmoja had eneo kubwa iwe mkoa na hata nchi mfuko wako tu

Wengi wanalihusisha kuwa na mafungamano na serikali ya RUSSIA lakn wao wanakataa na wanasema n kundi binafsi la ulinzi

Nitarud kwa ajil ya mission zao nchi zp wapo mission walizofanikiwa na walizoshindwa na uhusika wao katka vita vya Ukraine
Hv mkuu hatuwezi kujichanga
 
Wagner imeundwa mwaka gani na Ghadafi kauliwa mwaka gani?? Tumia hio teknolojia yako vizuri kujitoa uzuzu,,..................na hakuna vita ambayo inakosa casualties hata kama upande wenu ndo utakaoshinda,,vita sio michezo yenu ya ki lgbt......hata majangiri wa minato wanafilimbwa huko ukraine hadi hawana hamu na hio vita
Kila aliupande wa West ni lgbt? Utakuwa na matatizo ya akili au ulipata udhalilishwaji udogoni pole sana
 
Ghadafi ameuwawa 2011, PMC limeanzishwa 2014...

Hata hivyo katika vitu anajuta Putin ni kutoingilia kumlinda Ghadafi pale Libya.

Maana Ghadafi ilikuwa ni nguzo yenye nguvu iliyokuwa Africa ambayo ingemsaidia kuwanyoosha hawa mabeberu.

Hata baada ya hapo Putin hakukubali tena mabeberu kufanya ujinga kama wa Libya pale Venezuela...Ule mtiti wa Venezuela ulikuwa sio mchezo
venezuela huyu ambae anaomba poo kwa marekani yaishe warudishe mahusiano?
 
Kelele zenu zote mnajua Urusi akishawamaliza watetezi wa ushoga na usagaji mtakosa uhuru wa kufanya huo upumbavu wenu
Dogo unarusha mate sana Ushoga upo tangu enzi ya sodoma na gomora so hakuna kipya hapo ni Mungu mwenyewe atamaliza hii kadhia sio hao wabaguzi na majangiri
 
Najua lazima ujibu kwa hasira sababu hawa unaowatetea ndio majangili hadi walifikia kuligawanya bara la Afrika.
Urusi haijawahi kufanya ujangili sehemu yoyote isipokuwa majirani zake wakitaka kushirikiana na maadui zake huwa anawadunda na kuwaachia makovu ya kudumu.
Urusi tangu zamani amekuwa bega kwa bega katika kuyasaidia mataifa yanayoonewa na mabeberu
Wahi dawa
 
Hili kundi linafanya kazi popote penye maslahi ya Urusi tu, lilianzishwa mwaka 2014/15 likiwa na wapiganaji 250, sasa hivi linawapiganaji zaidi ya 50,000.

Jamaa nchi nyingi za Africa wapo, Africa ya Kati,Libya Mali na Burkina Faso.

Popote yalipo majeshi ya nchi za NATO, wakiingia hao jamaa NATO lazima wasepe.
Subiri kidogo mkuu utajua, Vikosi vipo US vinapata mafunzo ya Patriot halaf utakuja kutuambia tena hapa kuhusu Wagner Group, ukiona Urusi inakodi mamluki kiasi hiki ndani ya mwaka mmoja kwenye vita ujue hana tena jeshi, jeshi lake limeenda na maji sasa anaamua kukodi
 
Kinachonishangaza Wagner Group wakienda mahali penye wanajeshi wa NATO, nato wanaanza Kulalamika alafu wanaondoka.

Nato wanawaita Wagner group kwa jina la (mamluki wa Putin) 🤣🤣

Mfano pale Syria, Venezuela, Afrika ya Kati, Burkina Faso, Mali, Mozambique, Na Sasa Congo na Ukraine.
NATO walipanga mpaka mwishoni mwa mwaka huu ulioisha eneo kubwa la Afrika liwe halitawaliki ili waje kwa kisingizio cha kulinda amani kumbe wanachota rasilimali za chini ya ardhi pamoja na viungo vya wanadamu.

Kitovu cha uhalifu kwa Afrika Mashariki kilipangwa kiwe eneo la Mocimboa da Praia nchini Mozambique alafu uhalifu huo ungesambazwa kwa kasi maeneo ya Mtwara kuja hadi Lindi, pwani yote ya Afrika Mashariki huku zana nzito zikishushwa Rwanda kwa kipenzi chao Kagame.

Huko Mali, Afrika ya Kati, na Burkina Faso hawa NATO walikuwa wanamtumia Mfaransa na Uingereza kutumia nguvu kubwa kusambaza makundi ya kigaidi na silaha sema bahati nzuri kuna baadhi ya mapinduzi yakawaleta vijana wanaojua michezo ya NATO ndio maana wakaomba kimyakimya usaidizi kutoka Urusi, Urusi wakapeleka wanajeshi wachache wa Wagner group.

Hata Congo Wagner group wameshaingia ndio maana unaona ufalme wa Magharibi/NATO ukilegalega juu ya yale malengo yao.

Kila wakati wanamuuliza rais wa Congo kuhusu ushirika wake na Wagner group lakini rais wa Congo anakataa.
Nakumbuka mwaka 2020 Uingereza alipanga kupeleka kikosi pale Zambia mpakani na Tanzania akishirikiana na baadhi ya mataifa mengine ya NATO, ila ilipofika muda ambao wanataka kuleta kikosi wakakuta tayari Wagner group wapo kwenye misitu ya Zambia tayari.

Na tangu Wagner group wameingia Zambia, ule uhalifu wa kukata watu vichwa kwa makundi kijiji hadi kijiji umeishia. Pia media za magharibi zimebaki kulalamika sehemu zote za dunia tofauti na kipindi cha nyuma walikuwa kazi yao ni kuripoti kuhusu ugaidi na kutabiri kuhusu ugaidi.

NATO wapumbavu sana wanataka sehemu kubwa ya dunia iingie kwenye mchakamchaka wa machafuko alafu wao waendelee kuchota rasilimali na kujiimarisha ili kukija kutulia wawe na nguvu ya kulazimisha sera zao za ushoga na ufeminist kwa nguvu.
Subiri kidogo mkuu utajua, Vikosi vipo US vinapata mafunzo ya Patriot halaf utakuja kutuambia tena hapa kuhusu Wagner Group, ukiona Urusi inakodi mamluki kiasi hiki ndani ya mwaka mmoja kwenye vita ujue hana tena jeshi, jeshi lake limeenda na maji sasa anaamua kukodi

Kumbuka alianza na jeshi lake, baadae akakodi kutoka Islamic State, akaingiza wafungwa lakini na vijana wa mtaani wakapewa mafunzo na juzi hatima yao umeisikia 400 wameondoka na hao Wagner wape muda kiduchu uje hapa utueleze tena
 
Sawa comedian zelensky
 
Ilitakiwa wamlinde JP mwendazake😃😃😃😃😃
Nachojua n kikundi binafsi Cha ulinzi Kutoka Russia

Kinapokea oda yoyote toka kwa mtu yeyote kikubwa pesa yako tu wanatoa ulinzi wa mtu mmoja mmoja had eneo kubwa iwe mkoa na hata nchi mfuko wako tu

Wengi wanalihusisha kuwa na mafungamano na serikali ya RUSSIA lakn wao wanakataa na wanasema n kundi binafsi la ulinzi

Nitarud kwa ajil ya mission zao nchi zp wapo mission walizofanikiwa na walizoshindwa na uhusika wao katka vita vya Ukraine
 
Hawa walitokana na wakati ambao Russia inabadili mfumo wa ujamaa kwenda ubepari watu walionunua viwanda na makampuni kutoka serikali walikuwa wanauwana sana ndio yakaibuka makampuni ya kutoa mabody guard mojawapo likiwa hili mpaka sasa huwa linapewa kazi na serikali ikibidi
 
Kama habari uliyoileta ni ya kweli basi tuiombee urusi iwe na nguvu zaidi. Maana urusi haina njaa na natural resources Kama hawa nato
Urusi hana njaa ya natural resources ,Ndio Nchi pekee hapa Duniani inaaongoza kwa rasilimali nyingi za kila aina-ndio maana USA na Ulaya nzima kila kukicha mipango hao ni kuisambaratisha nia yao iwe kama Afrika isiyoojitambua.
Ukitaka uitawale hii Dunia lazima umukalishe chini Urusi na China vinginevyo ni kutwanga maji kwenye kinu.
 
Wakati gadafi anatandikwa mbona walikuwepo walisaidia nini? Kingne NATO haina maslahi tena libya lengo lao limefanikishwa hayo mengine ni porojo ulimwengu wa teknolojia kila kitu kipo wqzi danganya warusi wenzako wa tandale
Majangiri mengi wa hili kundi wamefia ukraine habari unazo?

Nawe tumia akili kundi gani hapa Duniani linaweza kupambana na Jeshi la Nchi mmoja na likaweza yani unalinganisha Kikundi cha watu na Serikali.
Pale Libya kulikuwa na Muungano wa majeshi ya Nchi zaidi ya 32+ ,hicho kikundi kimoja kitaweza vipi kupambana nao.
 
Subiri kidogo mkuu utajua, Vikosi vipo US vinapata mafunzo ya Patriot halaf utakuja kutuambia tena hapa kuhusu Wagner Group, ukiona Urusi inakodi mamluki kiasi hiki ndani ya mwaka mmoja kwenye vita ujue hana tena jeshi, jeshi lake limeenda na maji sasa anaamua kukodi

Kumbuka alianza na jeshi lake, baadae akakodi kutoka Islamic State, akaingiza wafungwa lakini na vijana wa mtaani wakapewa mafunzo na juzi hatima yao umeisikia 400 wameondoka na hao Wagner wape muda kiduchu uje hapa utueleze tena
🤣🤣🤣🤣 Marekani anaenda kujitia aibu kwa mara nyingine na michumachuma yake.
 
Back
Top Bottom