Acha ubishi, mpira umebadilika. Mchezaji kutouzwa timu kubwa kunaweza kusababishwa na mambo mengi. Ikiwemo mkataba, umri, mipango ya timu anayochezea. Simba Wana miaka minne Sasa hawana sera ya kuuza wachezaji sio kwamba ofa hazipo. Na sio kila ofa inayofika kwa klabu lazima itangazwe.
Usifananishe Simba na Yanga miaka ya nonda shabani na Sasa. Sasa hivi Kuna watu Wana elimu ya mpira. Unaweza kuuza mchezaji bilioni afu ikasababisha hasara ya zaidi ya bilioni. Timu inakua mbovu, mauzo ya jezi yanashuka, watu kuingia uwanjani wanapungua.
Ukumbuke kupata wachezaji kiwango cha chama kwa investment yetu hapa bongo sio rahisi ukimuuza unaweza kuyumba hata miaka mitano. Angalia Yanga mwaka Jana kasajili wageni wangapi na December katimua wangapi, January kasajili wangapi afu June katimua wangapi. Unadhan mateso wanayopata wakimpata mchezaji mzuri watamuuza kirahisi? Simba na Yanga hawategemei faida ya kuuza wachezaji. Wanategemea mapato ya uwanjani na mauzo ya jezi na hela za wadhamini.
Zipo timu nyingine Africa zina kipaumbele Cha kuuza wanategemea faida ya kuuza ila sio Simba na Yanga. As Vita unaowatajataja wanakupa mukoko wao wanamchukua tshishimbi, mwaka Jana walimchukua zana coulibary. Kwako wewe zana na tshishimbi ni zaidi ya chama?.