Tuijue Katiba: Rais akifia madarakani, basi makamu wake aliyegombea naye akapigiwa kura anarithi. Je, vipi kama makamu hakupigiwa kura?

Hakuna cha serikali ya mda au muda! Hapo mtu anayeitwa Makamu wa Rais anachukua uongozi.
Kundi la akina Britannica wanataka kumuondoa muha wa watu kwenye keki kibabe, kwa kisingizio eti Katiba haijasema
 
Lini makamu wa rais anapigiwa kura ? Hakuna form in picha au jina la makamu wa rais. Abaepugiwa kura ni mgombea urais tu.
Makamu wa Rais anapigiwa kura pamoja na Rais katika uchaguzi mkuu.

Unapopiga kura humchagua Rais tu, unachagua ticket ya Rais na Makamu wake.

Kwa mfano, kwenye uchaguzi wa 2020 kulikuwa hakuna namna ya kumchagua John Pombe Magufuli kuwa Rais bila ya kumchagua Samia Suluhu Hassan kuwa Makamu wa Rais. Kwa sababu ilikuwa unawachagua wote wawili kwa pamoja.

Watanzania wengi hawakuelewa na bado hawaelewi dhana hii ya kuchagua ticket, kumchagua Rais na Makamu wake kwa pamoja.

Ndiyo maana wengi mpaka leo wanamuona Samia si rais halali, hakuchaguliwa, wakati hawaelewi kuwa ukichagua ticket ya Magufuli/Hassan kimsingi umemchagua Samia Suluhu Hassan kuwa Makamu wa Rais na siku Magufuli akifariki umempitisha Samia Suluhu Hassan awe Rais bila ya uchaguzi mwingine.

Watanzania wengi wanadai katiba mpya wakati hata hii ya sasa hawaielewi.
 
Kundi la akina Britannica wanataka kumuondoa muha wa watu kwenye keki kibabe, kwa kisingizio eti Katiba haijasema
Tukijadili katiba tuweke na vifungu na ibara za katiba tujadili kwa detail, si kusemasema tu "katiba haijasema".

Mimi nimeweka ibara ya 50 inaonesha Makamu wa Rais ambaye hajachaguliwa anaweza kuwa rais pindi kiti cha rais kikiwa wazi.

Mpaka sasa hakuna aliyepinga ibara hiyo ya katiba.
 
Kundi la akina Britannica wanataka kumuondoa muha wa watu kwenye keki kibabe, kwa kisingizio eti Katiba haijasema
Hawataweza! Wamdanganye bibi yao ajifishe waone ki Mha chetu kitakavyochukua usukani kuelekea kwenye uchaguzi
 
Lakin rais wa sasa aliyekuwa makamu alihusiwa kuwa alichaguliwa. Bado mtoa mada anamantiki. Kura ya urais unaweza kupata kwa sababu ya ushawishi wa makamu wako.

Pengine bila yeye kura zisingiletosha. Sasa huyu ambaye wananchi hatujamuunga mkono ni vipi aweze kuwa rais?
 
Hiyo iko wazi anapitishwa na wabunge ambao ni wawakilishi wetu. Kwa hiyo akishapitishwa na bunge anakuwa amepata idhini kwa wananchi wote wa Tanzania sawa na aliyepigiwa kura.
Zile kura 538 za marekani? Katiba yetu inamshimo mengi sana.
 
Hivi huwa mnasomaje Katiba nyie watu? Utaratibu wa Makamu wa Rais kuchukua madaraka ya uongozi pindi Rais anapofariki au kupoteza sifa za kuwa Rais umeainishwa kwenye ibara ya 37 isome yote tu kuanzia mwanzo utakutana na hiyo ibara ndogo inayoelezea utaratibu huo. Hivyo lolote likitokea la kutokea Isidory Mkulima anakuwa Rais kwa kipindi kilichosalia.
 
Nakuelewa sana mkuu
Keep it up
 
Ila twende mbele turudi nyuma mwaka jana makamu wa rais alipotea kwa muda gani vile?
Mwaka huu RC Makonda alitoweka kwa muda gani?
Huwa wanaenda wapi?
 
Chuki ni kitu kibaya sana, nd maana wachawi wengi historia zao zinaonyesha ni watu waliokuwa na chuki ya kupitiliza. Rais Samia ataendelea kuwa Rais upende usipende, uumie uvumilie, ataendelea hadi pale Muda wake utapoisha kikatiba au pale Mungu atapopotisisha hukumu yake kama ambavyo ataipitisha kwangu na kwako na kwa mwengine yoyote.
 

CDF aache usenge ,abebe majukumu kibabe afumue hili genge la majambazi na maharamia waliohijack hii nchi kwa miaka 60 ,afungue criminal court ya kudeal nao mmoja baada ya mwingine apige martial law na baada ya kufumua na kuset mifumo upya ndio aruhusu civilian rule Kwa kuitisha uchaguzi mpya ,na huu ndio utakuwa mwanzo wa kuzaliwa kwa Tanzania mpya .
Na kuondokana na hii UTI Sugu inayoitwa CCM
Tatizo macdf wa hii nchi ni vilaza tu na machawa wa UTI sugu ya taifa (ccm) waliochaguliwa bila merits ,so no puppets watiifu wa UTI sugu
 
Katiba haisemi hivyo.
 
Kwani wapi nimesema hawi rais? Unajua hata hoja yangu ni ipi au unapinga kwa kuhemka tu?

Unajua kusoma kwa ufahamu?

Hiyo post yangu uliyoinukuu umeisoma na kuielewa au una changamoto ya kusoma na kuelewa?
 
Naishi humu tu sitoki nipo na katiba ya JMT nakomaa na ibara ya 37 tu. Ni hayo tu wajameni. Asanteni
 
We jamaa wewe humu sitoki nimejaladia kabisa ibara ya 37 ya katiba ya JMT kwa msaada zaidi wa kisheria endapo utata utajitokeza hapo mbeleni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…